Hivi ni ujinga, wivu au ni roho mbaya wanandoa waliotengana kuwazuia waliokua wenza wao kuwa na wenza wengine?

Hivi ni ujinga, wivu au ni roho mbaya wanandoa waliotengana kuwazuia waliokua wenza wao kuwa na wenza wengine?

NDOA INAEXPIRE
Na viongozi wa dini wakifuatilia sheria na maandiko ndoa nyingi sana ni batili maana zimejaa zinaa.
Ukizini talaka ruksaaa

Mathayo 5:32​

Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Kumbuka Yesu pia alisema asamehe 7×70!

Na hakusema kosa lipi !
 
Kutengana wana ndoa ni huzuni kubwa.

Huyu baba ni kama wale ma papaa wa zamani, mjanja mjanja sana, ila mwanamke naye yuko vizuri.

Wana ndoa huwa wanaoneana wivu hata baada ya kutengana.

Nina good experience,
 
Biblia inakataza kuachana isipokua kwa sababu ya zinaa.
Maachano yote yanakatazwa wala huruhusiwi kuoa au kuolewa tena.
Achano la kusababishwa na zinaa halijasema wewe uliyemwacha mzinzi ubaki hivyohivyo bila kuoa ila limesema atakayemuoa yule mzinzi uliyemwacha kwa talaka anazini. Kwahiyo adhabu ya mzinzi ni kutalikiwa na kubaki bila mwenza

Mathayo 5:32​

Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Hiko kijisection kikizingatiwa vyema ungejikuta hata mume hujaqualify kuwa nae asilimia ya watoto waliozaliwa kuanzia late 7O's waligongwa kabla ya kuolewa😂😂😂
 
Kumbuka Yesu pia alisema asamehe 7×70!

Na hakusema kosa lipi !

Msamaha unakuwepo. Ukimpa mtu nafasi nao ni msamaha

Malipo ya zinaa ni mauti tuu

Mauti ya mbili, mauti ya roho, mauti ya nafsi, mauti upendo......

UFUNUO 2:20-21
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

MITHALI 6:32
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

WALAWI 20:10
10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
 
Hiko kijisection kikizingatiwa vyema ungejikuta hata mume hujaqualify kuwa nae asilimia ya watoto waliozaliwa kuanzia late 7O's waligongwa kabla ya kuolewa😂😂😂

😅😅😅😅
 
Shida zipo kwenye Mahakama zetu. Kesi za ndoa zinachukua Hadi Miaka 7+ kuisha. Hivyo ndoa yeyote inakayofanyika inakuwa batili mpk kesi husika iishe kabisa. Watu wanashidwa kuvumilia maana muda unakuwa mrefu sana.
 
Hapa sijakuelewa umesema jack lazima apate tu, kwa vigezo gani? Walitafuta pamoja na mzee mengi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mke ni mrithi kwenye mali za mume wake. Awe amezitafuta ama hajazitafuta. Ingekuwa kwenye divorce na Mengi jack angekosa mali. Ila sababu hakuna divorce hivyo jack ni mke halali wa marehem hivyo Ana haki ya kurithi mali za marehemu iwe ametafuta naye ama hajatafuta naye
 
NB: ili mwanaume uwekewe pingamizi ya kuoa na mwanamke uliyeachana nae lazima uwe na fedha otherwise hyo situation utaisikia tu.
 
NB: ili mwanaume uwekewe pingamizi ya kuoa na mwanamke uliyeachana nae lazima uwe na fedha otherwise hyo situation utaisikia tu.

Hivi eeh!?
 
Back
Top Bottom