Hivi nini hatma ya mtumishi wa Serikali ambaye amekopa benki Tsh. mil. 15 na akaamua kutoweka kazini?

Hivi nini hatma ya mtumishi wa Serikali ambaye amekopa benki Tsh. mil. 15 na akaamua kutoweka kazini?

Bima inacover tu kama mkopaji akifariki au akipata ulemavu ambao umepelekea kutoendelea na kazi hayo ya kuacha kazi na kukimbia bima hainacover hilo deni atalilipa.
Sio kweli, dhamana ya mkopo aliokopea ni nini?
 
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?
Nini hatma yake kama siku anapatikana?
Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
Hilo alilolifanya huyo staff mwenzako, benki wanalifahamu.

Kuna vifo nk nk, vikwazo vyote benki wanavifahamu vizuri sana, kwa hiyo mkopo wowote wautowao lazima uwe na bima na hapo ndipo bima hufanya kazi yake.

Kwa hiyo benki hawahangaiki na kumtafuta wala kumfanya lolote.

Watakaohamgaika naye ni waajiri wake ili kumchukulia hatua za kinidhamu na si benki.
 
Huyo hatakuwa wa kwanza kukopa akatokomea mitini wako wengi na bank hawakufanyi chochote zaidi ya kukuingizia kwenye system zao za pamoja za kibenki (credit bureau ) ili usikopesheke na bank yoyote ile milele.

Nina shahidi nyingi kwenye hili, Kumbuka mtumishi wa umma dhamana ya mkopo wake ni mshahara na si vinginevyo.

Nikipata mda nitaandika kwa kirefu.
 
Mi nilikopa TIGO NIWEZESHE mbona nipo nadunda tu. Au labda ndiyo wananitafuta kimyakimya kama Kigogo wa Twitter. Acha tusikilizie tuone.
 
Sio kweli, dhamana ya mkopo aliokopea ni nini?
Salary Mkuu!! Kuna Type mbili za Loan ,Kuna Personal Loan na Scheme Loan! Scheme Loan ni Kampuni wanakubaliana na Bank wawape mkopo so salary ndio inakuwa kama dhamana, Personal loan hapo ndio unaenda wewe kama wewe hapo dhamana inaweza kuwa MJENGO au Biashara yako!
 
Salary Mkuu!! Kuna Type mbili za Loan ,Kuna Personal Loan na Scheme Loan!! Scheme Loan ni Kampuni wanakubaliana na Bank wawape mkopo so salary ndio inakuwa kama dhamana ,Personal loan hapo ndio unaenda wewe kama wewe hapo dhamana inaweza kuwa MJENGO au Biashara yako!!
Huyo anayezungumziwa ni mtumishi boss na dhamana yake ni mshahara
 
Huyo hatakuwa wa kwanza kukopa akatokomea mitini wako wengi na bank hawakufanyi chochote zaidi ya kukuingizia kwenye system zao za pamoja ili usikopesheke na bank yoyote ile milele.

Nina shahidi nyingi kwenye hili, mtumishi wa umma dhamana ya mkopo wake ni mshahara na si vinginevyo.

Nikipata mda nitaandika kwa kirefu
Tutashukuru kwa elimu zaidi,hii ndio raha ya Jamii forum
 
Enzi za JK ingewezekana! Ila kwa awamu hii, lolote linaweza kutokea. Kama ni wewe mwenyewe mwenye mpango huo, ni vyema ukavumilia tu mpaka hilo deni litakapo kwisha!

Achana na hayo mambo ya kukopa sherehe, kulipa matanga.
Kwa awamu hii mdeni akifariki inakuwa aje? Awamu hii kiboko, hata sheria na taratibu za kibenki duniani zimevumbuliwa awamu hii!

Sent from my LM-Q710(FGN) using JamiiForums mobile app
 
Kijana njoo tu mezani tukubaliane namna utakavyolipa deni letu! Vinginevyo hutachukua mkopo kwenye benki yoyote maana wakopeshaji watakuwa wanaangalia kumbukumbu zako za ukopaji huko nyuma! Sasa wakikukuta wewe ni defaulter hawatakukopesha, sasa ya nini ujinyime fursa? Njoo tuzungumze!
 
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?

Nini hatma yake kama siku anapatikana?

Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
Si ana nssf yake huwa wanakata. Usidhani jamaa wajinga kiasi hicho
 
Hapana hata mfanyakazi akikimbia huwa bima inalipa watu wa benki sio wajinga hivyo.

Isipokuwa kinachofanyika ni kwamba ukikimbia bima inawalipa lakini pia na wewe ukijipeleka wanakulipisha inakuwa wamepata faida mara 2.

Nina uzoefu wa rafiki zangu walichukua mikopo wakaacha kazi na hadi leo hawajatafutwa ishapita miaka 5 hadi sasa kimya.
Bima sio wajinga kiasi hicho. Ukiacha kazi unalipa deni lako mwenyewe. Na si ajabu likaenda hadi kwa next of keen wako.
 
Mafao yake yote yatalipia deni.

Usishangae mafao yasipotosha wakafuata referees wako wakawafilisi.

Kwa nini msiwe waaminifu, mtaharibia na wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?

Nini hatma yake kama siku anapatikana?

Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
Usitoroke kazini mkuu kama una deni, subiri umalize deni halafu uache kazi kwa utaratibu ndugu mil15 kwa maisha ya kujificha sio nyingi mkuu
 
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?

Nini hatma yake kama siku anapatikana?

Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
Je na wale walisimamishwa kazi Kwa vyeti feki inakuwaje.
 
Back
Top Bottom