Hivi nini hatma ya mtumishi wa Serikali ambaye amekopa benki Tsh. mil. 15 na akaamua kutoweka kazini?

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Kuna mtumishi mwenzetu ambaye amekopa benki kiasi cha Tsh. milioni 15 na baada ya wiki akatoweka hakuonekana tena kazini ni mwezi wa pili sasa tangia atoweke na wala hapatikani kwa mawasiliano yoyote yale

Je, nini hatma ya pesa aliyokopa benki, namaanisha marejesho?

Nini hatma yake kama siku anapatikana?

Ipi inaweza kuwa hukumu yake endapo atapatikana?
Muulize Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Anaziwezea sana issue kama hizi
 
Lipa Deni. Kwa Sasa Kuna credit bureau zinakusanya taarifa za wadaiwa wote mpaka bili za maji, Kisha zinatunzwa. Hivyo unakuwa umejichagulia profile yako nchini
Mi nilikopa TIGO NIWEZESHE mbona nipo nadunda tu. Au labda ndiyo wananitafuta kimyakimya kama Kigogo wa Twitter. Acha tusikilizie tuone.
 
Hii kauli huwa inaniudhi, dawa ya deni ni kulipa.
 
Hapana hata mfanyakazi akikimbia huwa bima inalipa watu wa benki sio wajinga hivyo.

Isipokuwa kinachofanyika ni kwamba ukikimbia bima inawalipa lakini pia na wewe ukijipeleka wanakulipisha inakuwa wamepata faida mara 2.

Nina uzoefu wa rafiki zangu walichukua mikopo wakaacha kazi na hadi leo hawajatafutwa ishapita miaka 5 hadi sasa kimya.
Kama ni hivyo iweje wafanyakazi hewa/vyeti feki walipofuzwa kazi Ma bank yanadai Tsh.49.5bil walizowakopesha hao wafanyakazi kwa mujibu wa barua ya Tanzania Bankers kwenda serikalini wakiulizia hatma ya mpunga wao.

Bima si walipe huo mpunga ili serikali isiandikiwe hizo barua.
 
Je na wale walisimamishwa kazi Kwa vyeti feki inakuwaje.
Wapo mbona kitaa wanadunda Kuna mtu huku alikopa m 20 yupo sema alikimbiaga Sasa ameludi na hakuna anayemtafuta kifupi alijilipa mafao yake
 
Hapana hata mfanyakazi akikimbia huwa bima inalipa watu wa benki sio wajinga hivyo.

Isipokuwa kinachofanyika ni kwamba ukikimbia bima inawalipa lakini pia na wewe ukijipeleka wanakulipisha inakuwa wamepata faida mara 2.

Nina uzoefu wa rafiki zangu walichukua mikopo wakaacha kazi na hadi leo hawajatafutwa ishapita miaka 5 hadi sasa kimya.
Mim nliacha kazi serikalin kwa kufuata taratibu na nikaandika barua benki ili wanipe utratibu wa kumalizia deni....hawakunijibu, na waliendelea kukata kwenye salary yangu mpaka imeisha, ila tu kile kiwango ambacho nlikua nakipata baada ya makato kikawa sikioni, ila kila mwezi napata notification ya mshahara hadi deni limeisha..mwaka wa 5 sasa kimya! Mara nyingi mwajiri kama ni serikali huendelda kubeba mzigo mana ndio mdhamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa walikuwa wanakata mshahara gani wakati umesema kazi uliacha?
Ina maana serikalini ukiacha kazi bado mishahara yako inaendelea?

Tuelimishane kidogo

✓Kuna hela ya mtumishi wa umma anaktwa kwenye hifadhi za kijmii, mfano LAPF
✓Huyu mtumishi anapoenda kukopa Benki, Cha kwanza benki ataangalia kwenye LAPF yako umefikisha kiasi gani
✓Afu Benki watakukopesha kutokana na kiasi kilichopo kwenye LAPF
✓Endapo utatoroka na kuondolewa kwenye payment wao watapeleka barua huko LAPF kuonyesha deni lako na baada ya kujiridhisha,,pesa yako itahamishiwa kwenye account ya benki inayokudai
LAPF hadi ufikishe milion 15 hadi miaka kibao ya kazini, Mara nyingi deni huendelea kulipwa na mdhamini ambae ni mwajiri. Mim nliacha nikiwa na mkopo na bado nikaenda kulamba LAPF michango yangu nlikuata tumilion tutatu 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa walikuwa wanakata mshahara gani wakati umesema kazi uliacha?
Ina maana serikalini ukiacha kazi bado mishahara yako inaendelea?
Ukienda kukopa kama mdhamini ni serikali, mshahara haufungwi hata siku moja, benki hawapati hasara hata siku moja na ndio maana wanamsainisha form mwajiri wako. Kinachotokea wanapiga withheld tu wew unakua hupati ila payroll inakwenda na jina lako na benki wanakata chao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda kukopa kama mdhamini ni serikali, mshahara haufungwi hata siku moja, benki hawapati hasara hata siku moja na ndio maana wanamsainisha form mwajiri wako. Kinachotokea wanapiga withheld tu wew unakua hupati ila payroll inakwenda na jina lako na benki wanakata chao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo sawa nimekupata.
Maana yake unapoenda kukopa serikali anakuwa ni mdhamini wako.
Kwenye baadhi ya makampuni binafsi huwa wanakubali kuwa mdhamini kama hivyo na wengine hawakubali kuwa mdhamini kwa hiyo watu wa mabenki wana take risks.
 
Yeah mkuu, ukiwa umeajiriwa halmashauri mkurugenzi au afisa utumishi lazima ndie anaeidhinisha upewe mkopo. Kama sector binafsi vilevile na ndio maana sehem nyingi binafsi hawafanyi hayo mambo hata kama salary wanipitishia benki. Hawakudhamini kamwe wanaogopa risk, mana hilo deni wataendelea kulilipa hadi liishe, benki hata siku moja hawapati hasara, hayo mambo yote washapiga hesabu zao....na sio kukata kwenye mafao kama mdau mmoja alivyosema..mtu anafanya kazi miaka 2 anakopa milion 20, atakua kachangia laki 8 tu unakuta!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda kukopa kama mdhamini ni serikali, mshahara haufungwi hata siku moja, benki hawapati hasara hata siku moja na ndio maana wanamsainisha form mwajiri wako. Kinachotokea wanapiga withheld tu wew unakua hupati ila payroll inakwenda na jina lako na benki wanakata chao

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wakiendelea kukuweka kuweka mshahara while haupo kazini na bado unadaiwa bank ni nini watakufanya .
Kuna jamaa yangu ni bado wanaweka mshahara. Mwaka wa 2 huu
 
Hapo uzembe huwa wa afisa utumishi hakuna madhara yyte, hata mim nlikula kama miez 5 hivi baadae ndio ukakatwa...inatakiwa anapeleka taarifa benki, payroll ikienda wanakata cha kwao na kile kilichobaki mtumishi haingiziwi, bali huwekwa kwenye account maaalum ya serikali! Ila watakuja kumkatia tu kupitia uhakiki, au sometimes unakuta mtumishi amecheza dili na afisa utumishi wanakula wote hizo hela

Kwa mfumo wa Sasa HV ukiacha kazi kabla ya tarehe tano hutapata huo mshahara..taarifa zinafika fasta hazina wanakutoa kwenye system
 
Tuelimishane kidogo

✓Kuna hela ya mtumishi wa umma anaktwa kwenye hifadhi za kijmii, mfano LAPF
✓Huyu mtumishi anapoenda kukopa Benki, Cha kwanza benki ataangalia kwenye LAPF yako umefikisha kiasi gani
✓Afu Benki watakukopesha kutokana na kiasi kilichopo kwenye LAPF
✓Endapo utatoroka na kuondolewa kwenye payment wao watapeleka barua huko LAPF kuonyesha deni lako na baada ya kujiridhisha,,pesa yako itahamishiwa kwenye account ya benki inayokudai

Inamaana mfano nikiajiriwa leo mimi kukopesheka mpaka huko LAPF kujaejae pesa kidogo.

Siwezi kopa Mkopo mwaka mmoja tu au unaofata baada ya ajira.
 
Mkopo ajira ukitokomea mwenye dhamana ni mwajili wako tu na sio ww maana ndo alikudhamini na kusaini ukapewa pesa.

Yeye atatoa taarifa bank kuwa uko fired na bank itapewa pesa yako kutoka mifuko ya jamii kama haitatosha, Bima wanamalizia, ingawa kwenye mashart wameandika mlipaji akitokomea atatafutwa hadi kutangazwa redioni na tv

Ila kama ni personal huu labda ufe ndo hutodaiwa
 
Back
Top Bottom