Hivi Nyerere lengo lake haswa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar lilikuwa nini?

Hivi Nyerere lengo lake haswa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar lilikuwa nini?

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
8,748
Reaction score
18,096
Yani aliwaza nini yani? yani lengo lake lilikua lipi yani kwa upande wa kufaidika na muungano ( au ndio zile tetesi kua dar,pwani,Tanga,Mtwara,Lindi na Mombasa zilikua sehemu ya Zanzibar??)

Maana mpaka sasa sioni maana ya Muungano, yani Mzanzibar anaweza kua Raisi bara halafu Mtanganyika hawezi kua Raisi Zanzibar, imekaaje hii?

Labda mimi kichhwa changu kimelewa harufu za damu hembu nyie wasomi nipeni faida zinazoonekana hadi sasa za huu Muungano, Tanganyika inafaidikaje? au Mwalimu alitapwliwa??
 
Nahisi aliangalia zaidi
1. Masuala ya bandari na
2. Sultan asiludi kiurahisi pale zenj.
 
Hiyo ya 2 asiporudi ndio nini yani yeye anapata nini hapo zanzibar, bandari zipi kwa mfano
1. Zanzibar ingeweza kuwa kitovu cha biashara ya baharini kama Singapore au Mauritius, hivyo Tanganyika ingeweza kulazimika kulipia huduma za bandari.

2. Changamoto za usalama wa baharini, magendo, ushindani wa kijeshi, kisiasa ikiwa zenji ingekuwa na msimamo tofauti wa kisera (mfano, Zanzibar kujiunga na mataifa ya Kiarabu wakati wa Vita Baridi.

Kwa hiyo kuna mambo kadhaa yaliangaliwa.. 🤝🤝
 
Back
Top Bottom