Mchungaji Daniel mgogo aliwahi Kusema;wanaume ni watu wa ajabu sana,hasa linapokuja swala la kumtongoza mwanamke
Akasema,ukivunja ungo na kuanza kuwa na mvuto watamiminika wengi sn kukutongoza
Siku ukipata mchumba na kuvalishwa Pete watapungua pengine Hadi kufikia 10.wengine watakata tamaa
Siku unaolewa kuna wengine watano watakata tamaa watabaki watano wanaendelea kukuimbisha uwape mzigo.
Umefunga harusi,upo ndani ya ndoa wanabaki wawili ambao wao kazi Yao ni kuendelea kukukumbusha ombi la miaka yote hiyo na Kwa nn unakuwa mgumu kiasi hiko,wakati yeye yupo tayari hata kuwa kidumu(mchepuko)
Sasa hawa wawili waliobaki ndy hao unaozungumzia wewe mleta mada..Hawa watu labda wasikie umekufa ndy wataacha kukusumbua,wao hawajali umevalishwa Pete,Una ujauzito wa mumeo,umezaa sijui Umefunga ndoa,watakutongoza Tu hata ufanyaje wao hawajali..kiufupi wewe wavumilie Tu watu dizaini hii maana hata ufanyaje hawaelewagi naving'ang'anizi km Luba