Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

Pizza magharita kitu original kutoka Sicily Italy. Nyanya tu na cheese original sio zenu hizi artificial.
a9f091583dc21da213948d3575332c98.jpg
 
umeona eeh.. Chapati kama kaukau. Mkuu wapi wanauza Elfu kumi? dar huwa wanauza kuanzia elfu 18 hadi 25 baadhi ya sehemu, kisha wanakuuzia soda buku au buku mbili. Mimi nakunywa soda, Pizza nanunua tu. Mara nyingi nina rafiki yangu anapenda hivyo nanunua ili afurahi nami nakula kipande kimoja lakini sisikii chochote. Baga ndo poa. Halafu baga unamwambia akuwekee pilipili.
Mdau hiyo elfu 25 nanunua kuku wangu swaafi wa kienyeji ndizi zangu na viungo najipikia sio kujilamba huko hadi watoto wanafaidi sasa piza small 25000 kama sio uchoyo nini
 
Mi hio midude huwa siielewi kwanza ina mafuta sana halafu ni source ya kansa tu.

Nikitaka piza natengenesa my local pizza

Ingredients

1.Mayai ya kienyeji 7

2.Karoti kubwa moia .

3.Nyanya kubwa 1

4. Kitunguu kimoja

5.Pilipili moja

6.Mafuta kidogo sana

7.Hoho moja

Nakaanga kidogo kwa frying pan kwa moto ea kadri nakuweka chumvi kidogo tu

Bonge la Pizza linatokea [emoji12]

Nikitaka Lowe hivyo hivyo inakuwa pizza

Nikitaka I we baga natafuta mkate Wa slice ule Wa njano kabisa slice 4 juu mbili chini mbili

Nachukua my local made pizza naweka katikati ya hivyo vipande vya mkate.

Natafuta my local made fruit juice(passion or mango) ya bariiiiidi nashushia aaaaaaaaaah!!!!

Namtafuta shemeji yenu tunazama ndani

Halafu............ . . ...

Chaji imeisha wakuu ntaendelea baadae[emoji14] [emoji12]
 
Oooogh! Nimeweka historia ya kutapika kwenye ngazi za Subway huko mnakozuiwa kwenda na Trump...sipendi pizza jamani
 
We figganigga, umenikumbusha wakat nasomea Upadri nchini Uholanzi (1999 - 2004).
Ebana masista wa pale Amsterdam Cathedral walikua wanatengenezea mipiza mitamu hiyo... Unaweza kufa.
Padri tumsif yesu kristo. Mi naitwa sister Eutropia.
 
Aisee wimbo usioujua hauimbiki, mie hivyo vyakula navisikia kwenye nyimbo za wanamuziki havinitoi mate....
Niambie Dona na dagaa ama matembele aisee hapo utaita njaa
Unasahauje maziwa ya mtindi hapo kwenye hiyo Dona + Dagaa + Tembele
 
Back
Top Bottom