Uchaguzi 2020 Hivi pamoja na "promo" yote ya mabango yaliyotapakaa nchi nzima, ni kwanini CCM inapelekwa mchamchaka na Tundu Lissu?

Uchaguzi 2020 Hivi pamoja na "promo" yote ya mabango yaliyotapakaa nchi nzima, ni kwanini CCM inapelekwa mchamchaka na Tundu Lissu?

Namkataa shetani, na kazi zake zote na mambo yake yote........... Najitoa kwa mtu wa watu ili nimpigie kura na kumuombea kwa Mungu amlinde hadi atakapoingia Ikulu ila akasafishe nyumba yetu iliyogeuka pango la wanyangányi.
Hakika katika awamu hii, Ikulu imegeuka kuwa pango la wanyang'anyi
 
Kuna msemo wa wahenga usemao kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza......................

Kwa namna CCM ilivyosambaza mabango nchi nzima, wakati wapinzani wao wa kisiasa, vyama vya upinzani, wakiwa hoi bin taabani, naweza ulinganisha usemi huo na hali halisi ya hivi sasa.

Hivi unawezaje kulinganisha mapokezi makubwa mno anayoyapata Tundu Lissu, ukimlinganisha na John Magufuli, wakati akiwa hana bango hata moja nchi nzima?

Ni wazi kuwa watu wao wa "marketing" wanafanya kazi ya ziada katika kufanya hiyo "promo" kwa kumtangaza kwa nguvu zote huyo mgombea wao wa kiti cha Urais, John Pombe Magufuli na ya wagombea wengine wa CCM.

Nimekuwa pia nikijiuliza hivi nguvu yote wanayotumia CCM ni ya nini wakati walishautangazia ulimwengu, kuwa vyama vya upinzani vimeshajifia "natural death" kutokana na utendaji wa kutukuka wa Magufuli!

Nimejiuliza pia hivi ni serikali ya CCM hii hii ambayo imekuwa ikisema kwa miaka 5 mfululizo, ikiwagomea kabisa kabisa kuwaongezea mishahara ya wafanyakazi wa Umma kwa madai kuwa serikali haina fedha hizo za kuwaongezea mishahara watumishi hao, lakini wakati huo huo wananchi tukishuhudia chama tawala cha CCM kikitapanya mali ya Umma kwa kusambaza mabango kila mahali hadi kubandika mabango hayo kwenye miti na kwenye sehemu za "kujisaidia" watu uchochoroni?

Hivi wananchi wanajisikiaje kuhusu matumizi haya mabaya kabisa ya pesa, wakati hospitali zetu nyingi, wananchi wengi wanakufa, kwa kukosa dawa muhimu za panadol?

Hivi nyinyi maccm mnawezaje kufanya "promo" kwenye mikutano yenu ya CCM, kwa kuwalipa mamilioni ya pesa wasanii maarufu akina Diamond, wakati watoto wetu wanakalia matofali, kwa kukosa madawati mashuleni?

Imenenwa na wahenga kuwa kupanga ni kuchagua..............

Kwa hiyo kwa CCM kwao wamepanga, kipaumbele chao ni kufanya "promo ya kufa mtu" kwa mgombea wao Magufuli nchi nzima hadi yanakinaisha na kuleta kichefu chefu!
Pumba tupu, unadhani watanzania wajinga. Utaona muziki wake Oct 28.
 
LISSU (NA VIONGOZI WA CHADEMA) ASIACHE KUWAOMBA WANANCHI KWENYE MIKUTANO YAKE, KUREKODI MATUKIO YOTE YA UVUNJIFU AMANI YATAYOFANYWA NA VYOMBO VYA DOLA AU VIKUNDI VYOVYOTE. WANANCHI WAREKODI TUKIO NA SURA ZA WAHUSIKA. TUTAJUA MBELE KWA MBELE HIZO VIDEOS ZITATUSAIDIA WAPI.

cc CHADEMA
 
LISSU (NA VIONGOZI WA CHADEMA) ASIACHE KUWAOMBA WANANCHI KWENYE MIKUTANO YAKE, KUREKODI MATUKIO YOTE YA UVUNJIFU AMANI YATAYOFANYWA NA VYOMBO VYA DOLA AU VIKUNDI VYOVYOTE. WANANCHI WAREKODI TUKIO NA SURA ZA WAHUSIKA. TUTAJUA MBELE KWA MBELE HIZO VIDEOS ZITATUSAIDIA WAPI.

cc CHADEMA
Hakika ni lazima matukio yarekodiwe kwa ajili ya kumbukumbu, vile vile kwa ajili ya kuwaburuza kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague
 
FB_IMG_1602601143207.jpg

Stupidity
 
Ccm Haikujiandaa Kwa Uchaguzi Mkuu Mgumu Namna Hii
Ndiyo Maana Unaona Imekata Pumzi Muda Mrefu
 
Nasubiri kusikia tumeibiwa kura...

Viva Magu 2020 to 2030
Ccm imezidiwa sana na chadema kimkakati ndo maana ccm wameamka kuomba msaada toka polis ili kubambikizia kesi wapinzani na kuvamia ngome zao na kuwabambikizia kesi zisizo na dhamana kama walivyofanya kwa heche.
 
Back
Top Bottom