Hivi PSRS mnasubiri nini kutoa shortlists ya hizi taasisi TRA, NAOT, HESLB na MDs & Local government?

Mpuuzi sana,kulialia tu sijui anataka nini!!!inaonekana ni MLALAMISHI tangu akiwa mchanga
Ooh mkuu...... mbona maneno makali hivi u know,kila mtu anahobbies zake meenzako labda kushusha nyuzi JF za kulalamika ndio hobbies zake asa why unamjia juu kiasi hiki??

Kwa navyojua hi,i nyuzi za mtoa mada kuna watu wakiziona wanafarijika au kuelimika kwa njia moja au nyingine. Pia uku.buke ridhiki hutoa mwenyezi MUNGU sio mwanadaamu so sio vema kumhukumu au kuhukumu kila kitu


Mwisho angalia mkono ako je vidole vyako vinalingana? Najua havilingani na binadamu tupo hivohivo simply HATUFANANI. kyagata may the LORD your GOD see you through 🙏
 
unawapangia kazi PSRS eti wanangoja nini kuwaita kwenye Interview[emoji1787][emoji1787][emoji1787]uchoko wako ni wa kiwango cha juu sana
Ningependa kukushauri kitu mzee mwenzangu.
Nimeangalia mtiririko wa conversations zenu na mleta mada naona mnashushiana heshima kwa vitu vya kijinga tu.
Humu vijana wengi hawana ajira,hivyo wamevurugwa.kwa hiyo wewe kumuattack mtu kwa kumuita sijui kilaza haipendezi.nilitegemea sisi kaka zao tuliokwisha watangulia tutumike kama njia ya kuwasaidia na sio kuwabeza.
Kwa kifupi mzee mwenzangu umekosea na ni bora hata ukaacha kujibishana nao kabisa.
 
Ushauri wangu mimi ni huo tu mzee mwenzangu.kuendelea kujibizana na watu walio desperate ni kujishushia heshima tu.
 
Duh
Punguza ukali wa lugha jamani mtoa riziki ni Mungu na akiamua anaweza ichukua muda wowote!
 
Wise answer sasa hebu ishia hapa ili amani na upendo vitawale.
 

Mkuu, japo sikujui vya kutosha, una kila kiashiria cha jamii kutegemea mitazamo chanya kutoka kwako. Huu sasa ni mfano mzuri wa aina ya komenti wengi tulitegemea kuziona kutoka kwa mtu wa hadhi yako.

Maandishi yako yana hoja nzuri za kumjenga ndugu kyagata, lakini namna ulivyoyawasilisha yanamkwamisha kupata ujumbe.

Uzuri au ubaya wa kitu uko kwenye kona mtazamaji aliyoamua kuitazama, wewe uko sahihi kwa upande wako na kuna watu tuko pamoja na wewe na yeye amelenga kuwakilisha wengine wanaojiuliza maswali anayojiuliza na nauona usahihi pia, pamoja na hilo kuna watu tuko pamoja nayeye.

Kabla ya kumuona yeyote anakosea, ni vizuri kuelewa kilichomsukuma afanye alichofanya, hii ndiyo sababu naona wote wawili hoja zenu ziko sahihi shida ni hasira zimeingilia kati mkaanza kutumia lugha za matusi.

Nashauri tuusitishe huu mvutano, unakoelekea faida zake ni ndogo kuliko hasara.

Naomba radhi kama andiko hili litamkwaza yeyote kati yenu.

Waswahili husema, muungwana akivuliwa nguo, huchutama.

Usiache kumwagia vijana connection Mkuu.

Kila la kheri kwenye mchakato wako wa kuwania Ubunge, utakutana na mawazo hasi mengi sana, nakuombea yasikurudishe nyuma.
 
Huu ushauri ungeutoa mwanzo tusingetukanana.ila ulianza kwa madharau na kashfa.
Yaishe na tusameheane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…