Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,014
Reaction score
4,600
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..

SWALI:
Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

JIBU

HATUA YA UNYAKUO.
Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Hivyo anazidi kusema…

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.

Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani, na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye baada ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.

HATUA YA DHIKI KUU.
Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote (wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.

Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo. Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikira wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote wasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16). Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga (Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.

(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani. Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).

HATUA YA UTAWALA WA MIAKA 1000.
Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),

VITA YA GOGU NA MAGOGU
japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),

Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.

HUKUMU YA KITI CHEUPE CHA ENZI.
Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.

HATUA YA ZIWA LA MOTO.
Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…

Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9). Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.

Ubarikiwe sana.
MASOMO MENGINE YA BIBLIA UTAYAPATA HAPA CHINI
WINGU KA MASHAHIDI WA YEHOVA
 
Hata wakati wa NUHU anajenga SAFINA watu walimuona mgonjwa wa akili..Hata Nabii NUHU alipowaambia waingie kwenye SAFINA walimcheka na kumuona mwehu..HATA SASA WATU WANAKEJELI KUHUSU UNYAKUO..NA SIO AJABU watu watabeza watadhihaki.watacheka...sana ,lakini SIKU SI NYINGI,KATIKA KALENDA YA KIROHO NI KAMA MUDA UMETIMIA,ITS TIME NOW, KILA GOTI LITAPIGWA NA KILA ULIMI UTAKIRI UKUU WA YESU KUWA NI BWANA MKUU SANA .

View: https://youtu.be/aIdlKjEDe0M?si=DW_GT5sG-IwDkNUm
 
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..
Mzee hakuna watakatifu dunia hii all are sinners including me ...
 
Hata wakati wa NUHU anajenga SAFINA watu walimuona mgonjwa wa akili..Hata Nabii NUHU alipowaambia waingie kwenye SAFINA walimcheka na kumuona mwehu..HATA SASA WATU WANAKEJELI KUHUSU UNYAKUO..NA SIO AJABU watu watabeza watadhihaki.watacheka...sana ,lakini SIKU SI NYINGI,KATIKA KALENDA YA KIROHO NI KAMA MUDA UMETIMIA,ITS TIME NOW, KILA GOTI LITAPIGWA NA KILA ULIMI UTAKIRI UKUU WA YESU KUWA NI BWANA MKUU SANA .

View: https://youtu.be/aIdlKjEDe0M?si=DW_GT5sG-IwDkNUm

You have hallucinations.

You need mental rehabilitation therapy.

You are suffering from Schizophrenia.
 
W
Mzee hakuna watakatifu dunia hii all are sinners including me ...
Maandiko yanasema WATAKATIFU walioko duniani ndio Mungu anaopendezwa nao(hivyo kumbe watakatifu wapo duniani).
Pia ili kuingia mbinguni lazima uwe na mavazi meupe yasiyokuwa na madoa doa ,hakuna kinyonge kichafu kitakachoingia mbinguni.
Tiketi ya kuingia mbinguni ni usafi wa moyo matendo masafi..utakatifu..ukiongozwa na kujazwa Roho mtakatifu.
KIFUPI KANUNI YA KUINGIA MBINGUNI ni LAZIMA uwe MTAKATIFU uwe umejazwa roho mtakatifu..
MBINGU NI TAKATIFU NA WALIOKO MBINGUNI NI WATAKATIFU AMA WATAKAOINGIA NA KUWEPO /KUISHI MBINGUNI NI LAZIMA WAWE WATAKATIFU..
Hakuna kinyonge /chenye dhambi kitakachoingia na kuishi mbinguni..sheria ya kuiona pepo mbingu ni kuwa mtakatifu.(kupitia KRISTO na kusaidiwa kujazwa nguvu ya Roho mtakatifu na kuishinda dhambi katika yeye atutiaye nguvu huyo Roho mtakatifu/Yesu.
WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NDIO HAO MUNGU ANAPENDEZWA NAO.NA NDIO HAO WATAKAONYAKULIWA.
ILE neema bado ipo,hata wewe na mimi tuna alikwa katika safari ya mbinguni hapa duniani tunapita ,tuishi maisha kama RAIA wa mbinguni tunaoishi duniani,TUACHE NJIA ZETU MBAYA DHAMBI ZOTE..tumkiri na kumpokea huyu mwakozi wa ulimwengu Yesu.Tupate ubatizo wa ROHO MTAKATIFU tujazwe Roho mtakatifu..hii ni chapa ya kuingia mbinguni.YOH 3:5 YESU akajibu Amin amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na Roho hawezi kuingia ufalme wa MUNGU".
.tumtafute sana huyu Roho mtakatifu madaamu anapatikana..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”;

Isaya 35: 8 “Na hapo patakuwa na NJIA KUU, na njia, NAYO ITAITWA, NJIA YA UTAKATIFU; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; WASAFIRIO, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO”.

YESU anasema "YOH 14:6 MIMI NDIMI NJIA NA KWELI NA UZIMA, MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI". YESU pekee ndiye njia/tiket ya kutufikisha mbingun mbali na hapo ni kupoteza muda.

"UTAKATIFU". Utakatifu ni tiketi namba mbili(2) ya kuingia mbinguni. Mkristo anapomwamini YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake kinachofuata ni kujifunza Neno la MUNGU ambalo litamsaidia kuishi maisha matakatifu.
Ili upate nafasi mbinguni lazima uwe mtakatifu, maana hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia ktk uzima wa milele. Biblia inasema wenye dhambi wote sehemu yao ni ktk lile ziwa liwakalo moto na kiberiti yaani "Jehenamu" (UFUNUO 21:8).
Je duniani kuna watakatifu?. Ndio duniani kuna watakatifu. "ZABURI 16:3 WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NDIO WALIO BORA, HAO NDIO NILIOPENDEZWA NAO".
MUNGU mwenyewe anadhibitisha kuwa duniani kuna watakatifu. Lakin kuna baadhi ya watu wanasema kuwa duniani hakuna watakatifu na kwamba haiwezekani kuokoka duniani. duniani watu wanaokoka sawasawa na WARUMI 10:9 na watakatifu wapo sawa sawa na ZABURI 16:3
Kuishi maisha matakatifu ni mhimu sana kwa mkristo ili aweze kukamilisha safari ya kuingia mbinguni, ukimwamini YESU halafu ukaendelea kuishi maisha ya dhambi haitakusaidia kitu
 
"Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi..." hili ndio unapaswa kulifanya na hayo ya unyakuo watu watayajua baadaye...
 
Back
Top Bottom