Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,753
In fact, Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo ambaye ndiye Mungu pekee wa kweli, amegharimia mazingira/opportunity zote kumwezesha mwanadamu kuokolewa ili aurithi Ufalme wa Mungu pamoja naye milele, gharama yenye thamani kuliko vitu vyote ni ya Damu ya Yesu Kristo, dini haiwezi kukuokoa, elimu, au chochote, ila Imani kwa Yesu Kristo pekee. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae pekee ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..
Siku ile hapatakuwa na la kujitetea, mlango wa wokovu upo sasa wazi, ukitaka ingia, kama hutaki suburi moto wa milele. Na, ni wale tu waliooshwa kwa Damu ya MwanaKondoo ndio watauendea Mji ule.
1 Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.