Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

ndio kaka kwa sababu kwa Mungu miaka 1000 ni sawa na siku 1, hata paulo aliishi akijua Yesu angekuja mapema sana,sasa kwa vile pia hatujui ni lini tutakufa NI BORA TUWE TAYARI MUDA WOTE ..mfano wa wale wana wali 10 waliokuwa wanamngoja Bwana harusi.(kama vile leo tunavyongoja kuja kwa UNYAKUO WA YESU)..kuna waliokuwa wamejiandaa na watano wapumbavu ambao hawakujiandaa..Tuishi maisha ya kama vile ni raia wa Mbinguni tuliopo safarini duniani,TUWE TAYARI hatujui lini tutakufa hatujui lini UNYAKUO utatokea japo dalili zinaonyesha UNYAKUO UMEKARIBIA SANA MNOO.
Amen mkuu.
Mim mwenyewe tu huwa nikikaa moyo wangu unakuwa hauna amani, najua hapa mamabo yataharibika.
Mungu anisaidie.
 
W
Maandiko yanasema WATAKATIFU walioko duniani ndio Mungu anaopendezwa nao(hivyo kumbe watakatifu wapo duniani).
Pia ili kuingia mbinguni lazima uwe na mavazi meupe yasiyokuwa na madoa doa ,hakuna kinyonge kichafu kitakachoingia mbinguni.
Tiketi ya kuingia mbinguni ni usafi wa moyo matendo masafi..utakatifu..ukiongozwa na kujazwa Roho mtakatifu.
KIFUPI KANUNI YA KUINGIA MBINGUNI ni LAZIMA uwe MTAKATIFU uwe umejazwa roho mtakatifu..
MBINGU NI TAKATIFU NA WALIOKO MBINGUNI NI WATAKATIFU AMA WATAKAOINGIA NA KUWEPO /KUISHI MBINGUNI NI LAZIMA WAWE WATAKATIFU..
Hakuna kinyonge /chenye dhambi kitakachoingia na kuishi mbinguni..sheria ya kuiona pepo mbingu ni kuwa mtakatifu.(kupitia KRISTO na kusaidiwa kujazwa nguvu ya Roho mtakatifu na kuishinda dhambi katika yeye atutiaye nguvu huyo Roho mtakatifu/Yesu.
WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NDIO HAO MUNGU ANAPENDEZWA NAO.NA NDIO HAO WATAKAONYAKULIWA.
ILE neema bado ipo,hata wewe na mimi tuna alikwa katika safari ya mbinguni hapa duniani tunapita ,tuishi maisha kama RAIA wa mbinguni tunaoishi duniani,TUACHE NJIA ZETU MBAYA DHAMBI ZOTE..tumkiri na kumpokea huyu mwakozi wa ulimwengu Yesu.
unabii umeshatimia danieli 7 anasema aliona jiwe likija kugonga udongo na chuma kwenye unyayo baada ya rumi inamaana yesu angerudi wakati wowote tangu sasa dora la rumi limeskwisha kuwepo kifuatacho ni jiwe.

Watu wengi ikiwemo wasabato wamepotoshwa wanasubiri mpinga kristo wakati mpinga kristo ni pembe ndogo na iliibuka kwenye kichwa cha mnyama wa nne yani katika utawala wa rumi iliuwa watakatifu kipindi kile hivyo una ii ulishatimia leo badala ya kutazamia ujuio wa kristo wao wanatazamia ujio wa utawala wa rumi mpya ukiongozwa na mpinga kristo hakuna unabii unaosema kuwa pembe ndogo ingekuja mara mbili.

watu watakao okolewa hawatakuwa watu wakawaida. mimi sistahili lakini nitasimama katika kura yangu
 
Hata wakati wa NUHU anajenga SAFINA watu walimuona mgonjwa wa akili..Hata Nabii NUHU alipowaambia waingie kwenye SAFINA walimcheka na kumuona mwehu..HATA SASA WATU WANAKEJELI KUHUSU UNYAKUO..NA SIO AJABU watu watabeza watadhihaki.watacheka...sana ,lakini SIKU SI NYINGI,KATIKA KALENDA YA KIROHO NI KAMA MUDA UMETIMIA,ITS TIME NOW, KILA GOTI LITAPIGWA NA KILA ULIMI UTAKIRI UKUU WA YESU KUWA NI BWANA MKUU SANA .

View: https://youtu.be/aIdlKjEDe0M?si=DW_GT5sG-IwDkNUm

Tujiandae wakuu tusipuuze.
 
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..
Ungeweka na dalili zake,
 
Haya ni miaka 2000 sasa mnasema Yesu anakuja wakati umefika ni kwa sababu hamjui tafsiri ya Maandiko. Yesu alishakuja na yupo kwa njia ya Roho Mtakatifu msimsubiri wakati yupo nasi tayari.
 
Haya ni miaka 2000 sasa mnasema Yesu anakuja wakati umefika ni kwa sababu hamjui tafsiri ya Maandiko. Yesu alishakuja na yupo kwa njia ya Roho Mtakatifu msimsubiri wakati yupo nasi tayari.
1.Ni kweli YESU alishakuja na alikuwepo kabla,yupo na atakuwepo milele.

2.Ni kweli baada ya Roho mtakatifu pia alikuwepo na Yupo na atakuwepo ,na huyo ndio msaidizi wetu

3.Msimsubiri...alisema mwenyewe tumsubiri anakuja upesi katika physical form na siyo hii spiritual form na kila jicho litamuona,kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa ni BWANA....hiibitakuwa ni ujio wa mara ya tatu..miaka 1000 baada ya unyakuo.
***Mara ya pili atakuja atakuja kupitia unyakuo wa watakatifu ndio huu wakati tuliopo ni kitendo cha kufumba na kufumbua within a second watakatiifu watanyakuliwa kwenda mbinguni/RAPTURE ndio hii mada ya leo..UNYAKUO UMEKARIBIA.
wenye dhambi wote wataachwa duniani LEFT BELOW.NEEMA itaondolewa YA KUOKOLEWA bure kwa kupitia jina la Yesu.itafuatiwa na miaka 3 na 1/2 ya DHIKI KUU chini ya NEW WORLD ORDER utawala wa Shetani,ile nguvu iliyopo leo na neema ya Yesu inayozuia mabaya yasiwapate watakatifu wake itaondolewaa,hakutakuwa na kizuizi cha kumfunga shetani,wala cha kuzuia mabaya yake,hata sasa MABAYA hayatupati kwa sababu ya neema ya Yesu na kwa ajili ya maombi ya WATAKATIFU WALIOPO LEO DUNIANI siku wakiondoka hawa watakatifu wa Yesu DHIKI KUU INAKUJA,Mpinga Kristo anatawala bila kuzuizi,DHIKI KUU inakuja ambayo haijawahi kuwepo kabla ya duniani na haitakuja kutokea tena ,wapo wachache ambao watavumilia mateso ya dhiki kuu bila kumsujudia shetani bila kukubali kupokea CHAPA YA MPINGA KRISTO 666.
nao watakao vumilia mateso ya miili na damu yao wenyewe bila kuasujudu kwa mpinga kristo na kukataa kupigwa chapa mkononi na kwenye paji la uso katika kipindi chote cha miaka 3 na nusu nao
wataingia mbinguni kuungana na wale watakatifu walionyakuliwa..
Huko mbinguni wataishi miaka 1000 kutoka unyakuo,wakifurahi na kisherehekea wakila KARAMU pamoja na Yesu mbinguni.
Baada ya miaka 1000 kuisha Yesu atahukumu ulimwengu kwenye ziwa liwakalo moto lililoandaliwa kwa ajili ya shetani na wafuasi wake anayetenda dhambi ni wa ibilisi ni wa shetani ataingia pamoja naye motoni.
TUTUBU ,TUACHE DHAMBI ZOTE,tumkiri huyu Yesu ambaye ndiye mwakozi wa ulimwengu wote.
 
Maisha tunayoitiwa ni ya kiroho na sio ya kimwili, hayo ndio maisha ya umilele. Yesu hatakuja tena katika mwili tayari alishafanya hayo. Sasa Yesu yupo pamoja nasi ndani ya Roho Mtakatifu na watu wakiacha maisha ya mwili kisha kufa huenda Mbinguni kama wana mastahili hayo na hukutana na Yesu na watakatifu wengine.
 
Amna mkuu ni kwamba imeandikwa watu watakuwa wamelala au wanalima au kutwanga mmoja atatwaliwa mwingne ataachwa, hii itakavyotokea watu watashangazwa wengne wataona ndugu zao wamepotea na kutangaza maredioni.

SASA wale jamaa waleee 666 itakuwa waletee 😂😂
Nikajua ndiyo sasa mkuu😄😄
 
1.Ni kweli YESU alishakuja na alikuwepo kabla,yupo na atakuwepo milele.

2.Ni kweli baada ya Roho mtakatifu pia alikuwepo na Yupo na atakuwepo ,na huyo ndio msaidizi wetu

3.Msimsubiri...alisema mwenyewe tumsubiri anakuja upesi katika physical form na siyo hii spiritual form na kila jicho litamuona,kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa ni BWANA....hiibitakuwa ni ujio wa mara ya tatu..miaka 1000 baada ya unyakuo.
***Mara ya pili atakuja atakuja kupitia unyakuo wa watakatifu ndio huu wakati tuliopo ni kitendo cha kufumba na kufumbua within a second watakatiifu watanyakuliwa kwenda mbinguni/RAPTURE ndio hii mada ya leo..UNYAKUO UMEKARIBIA.
wenye dhambi wote wataachwa duniani LEFT BELOW.NEEMA itaondolewa YA KUOKOLEWA bure kwa kupitia jina la Yesu.itafuatiwa na miaka 3 na 1/2 ya DHIKI KUU chini ya NEW WORLD ORDER utawala wa Shetani,ile nguvu iliyopo leo na neema ya Yesu inayozuia mabaya yasiwapate watakatifu wake itaondolewaa,hakutakuwa na kizuizi cha kumfunga shetani,wala cha kuzuia mabaya yake,hata sasa MABAYA hayatupati kwa sababu ya neema ya Yesu na kwa ajili ya maombi ya WATAKATIFU WALIOPO LEO DUNIANI siku wakiondoka hawa watakatifu wa Yesu DHIKI KUU INAKUJA,Mpinga Kristo anatawala bila kuzuizi,DHIKI KUU inakuja ambayo haijawahi kuwepo kabla ya duniani na haitakuja kutokea tena ,wapo wachache ambao watavumilia mateso ya dhiki kuu bila kumsujudia shetani bila kukubali kupokea CHAPA YA MPINGA KRISTO 666.
nao watakao vumilia mateso ya miili na damu yao wenyewe bila kuasujudu kwa mpinga kristo na kukataa kupigwa chapa mkononi na kwenye paji la uso katika kipindi chote cha miaka 3 na nusu nao
wataingia mbinguni kuungana na wale watakatifu walionyakuliwa..
Huko mbinguni wataishi miaka 1000 kutoka unyakuo,wakifurahi na kisherehekea wakila KARAMU pamoja na Yesu mbinguni.
Baada ya miaka 1000 kuisha Yesu atahukumu ulimwengu kwenye ziwa liwakalo moto lililoandaliwa kwa ajili ya shetani na wafuasi wake anayetenda dhambi ni wa ibilisi ni wa shetani ataingia pamoja naye motoni.
TUTUBU ,TUACHE DHAMBI ZOTE,tumkiri huyu Yesu ambaye ndiye mwakozi wa ulimwengu wote.
yesu bado hajarudi mara ya pili angalia usidanganywe imeandikwa atakuja kwa nguvu nyingi na ufalme wote wa mbinguni jua litakuwa giza kama singa na mwezi hauta toa mwanga wake nyota za mbinguni zitaanguka nguvu za mbinguni zitatikisika ndipo kila mtu atajua mtamuona akija kwa nguvu nyingi na utukufu.

Angalia usidanganywe hakuna yesu aliyerudi bado ujuio wake hautakuwa kwa siri kulingana na hizo ishara nilizo zitaja lazima kila mtu atajua.
 
SIJASEMA YESU AMESHARUDI MARA YA PILI ,ILA UFUNUO UMETUPA ISHARA NA DALILI ZA ZA MAMBO YATAKAYOTOKEA YATAKAYO TUJULISHA KUKARIBIA KWA UNYAKUO.
ishara zote na dalili zote na ufunuo umeshatimia kwa asilimia 200% hivyo UNYAKUO UTATOKEA DAKIKA NA SIKU YOYOTE TUSIYOIJUA HATA SASA,TUWE TAYARI ,UNYAKUO UNATOKEA WAKATI WOWOTE.
 
1.Ni kweli YESU alishakuja na alikuwepo kabla,yupo na atakuwepo milele.

2.Ni kweli baada ya Roho mtakatifu pia alikuwepo na Yupo na atakuwepo ,na huyo ndio msaidizi wetu

3.Msimsubiri...alisema mwenyewe tumsubiri anakuja upesi katika physical form na siyo hii spiritual form na kila jicho litamuona,kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa ni BWANA....hiibitakuwa ni ujio wa mara ya tatu..miaka 1000 baada ya unyakuo.
***Mara ya pili atakuja atakuja kupitia unyakuo wa watakatifu ndio huu wakati tuliopo ni kitendo cha kufumba na kufumbua within a second watakatiifu watanyakuliwa kwenda mbinguni/RAPTURE ndio hii mada ya leo..UNYAKUO UMEKARIBIA.
wenye dhambi wote wataachwa duniani LEFT BELOW.NEEMA itaondolewa YA KUOKOLEWA bure kwa kupitia jina la Yesu.itafuatiwa na miaka 3 na 1/2 ya DHIKI KUU chini ya NEW WORLD ORDER utawala wa Shetani,ile nguvu iliyopo leo na neema ya Yesu inayozuia mabaya yasiwapate watakatifu wake itaondolewaa,hakutakuwa na kizuizi cha kumfunga shetani,wala cha kuzuia mabaya yake,hata sasa MABAYA hayatupati kwa sababu ya neema ya Yesu na kwa ajili ya maombi ya WATAKATIFU WALIOPO LEO DUNIANI siku wakiondoka hawa watakatifu wa Yesu DHIKI KUU INAKUJA,Mpinga Kristo anatawala bila kuzuizi,DHIKI KUU inakuja ambayo haijawahi kuwepo kabla ya duniani na haitakuja kutokea tena ,wapo wachache ambao watavumilia mateso ya dhiki kuu bila kumsujudia shetani bila kukubali kupokea CHAPA YA MPINGA KRISTO 666.
nao watakao vumilia mateso ya miili na damu yao wenyewe bila kuasujudu kwa mpinga kristo na kukataa kupigwa chapa mkononi na kwenye paji la uso katika kipindi chote cha miaka 3 na nusu nao
wataingia mbinguni kuungana na wale watakatifu walionyakuliwa..
Huko mbinguni wataishi miaka 1000 kutoka unyakuo,wakifurahi na kisherehekea wakila KARAMU pamoja na Yesu mbinguni.
Baada ya miaka 1000 kuisha Yesu atahukumu ulimwengu kwenye ziwa liwakalo moto lililoandaliwa kwa ajili ya shetani na wafuasi wake anayetenda dhambi ni wa ibilisi ni wa shetani ataingia pamoja naye motoni.
TUTUBU ,TUACHE DHAMBI ZOTE,tumkiri huyu Yesu ambaye ndiye mwakozi wa ulimwengu wote.
Do you see the way you mix the 3.5yrs and the 1000years?

Umesema mwenyewe mpinga Kristo atatawala kwa miaka 3.5, miaka ya dhiki kuu.

Baada ya hiyo miaka what happens?

Wakati wanasubiri miaka 1000 Yesu arudi mara ya tatu (! ! !) what is happening? Yesu mwenye alisema hizo siku za dhiki kuu zisipofupishwa hakuna atakayesalia duniani.
 
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..
Labda ukweli ila ni swali tu mbona hujanyakuliwa upo hapo bado unaandika post itakuwa nawewe umeachwa
 
Kanuni: Kila kitu kiwe na ushahidi wa waandishi wawili hadi watatu. Angalau vitabu viwili viseme kitu kilekile.

a)
“Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko."
2Wakorintho.13.1.BHN

b) "Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa."
Kumbukumbu.19.15.BHN

c) "Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe."
mathayo.18.16.BHN

i) Miaka 3.5 ya mpinga Kristo / Dhiki Kuu inahitimishwa na kurudi kwa Yesu na kusimamishwa kwa Ufalme wake hapa duniani. Yesu mwenyewe atamuangamiza mpinga Kristo.

a)
"Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile. Maana siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule uasi utokee na yule Mwovu aonekane, ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.

...Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mngao wa kuja kwake."
2Wathesalonike.2.3-8.BHN

b)
"Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.”
Ufunuo.17.14.BHN

c)
"Kwa ujanja wake, atafanikiwa katika mipango yake ya hila, naye atajikweza. Atawaangamiza watu wengi bila taarifa, na atataka kupigana na Mkuu wa wakuu, lakini ataangamizwa pasipo kutumia nguvu za kibinadamu."
danieli.8.25.BHN

d)
"Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake."
Ufunuo.19.19.BHN

ii) Yesu akija atatia mguu Yerusalemu, (nje kidogo na Jerusalem), kwenye ule mlima mzeituni alipoondokea.

a)
"Kisha Mwenyezi-Mungu atatoka na kuyapiga vita mataifa hayo, kama afanyavyo daima siku za vita.

Siku hiyo, atasimama kwenye mlima wa mizeituni ulio mashariki ya mji wa Yerusalemu. Mlima huo utagawanywa sehemu mbili na bonde pana sana litatokea toka mashariki hadi magharibi. Nusu moja itaelekea kaskazini na nusu nyingine kusini.

Nyinyi mtakimbia kupitia bonde hilo, katikati ya milima miwili ya Mwenyezi-Mungu. Mtakimbia kama wazee wenu walivyokimbia tetemeko la ardhi wakati wa utawala wa mfalme Uzia wa Yuda. Kisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye."
zekaria.14.3-5.BHN

b)
"wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.”

Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka ule mlima uitwao Mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
Matendo.1.11-12.BHN

iii) Muda mfupi kabla ya Yesu kutua Jerusalem, ndipo kutakuwa na unyakuo / ufufuo (kupewa miili mipya). Hivyo viwili vinatokea wakati mmoja.

Muda mfupi ni dakika / masaa / siku kadhaa? Mjadala mwingine. Lakini ni wakati tayari dunia imekumbwa na dhiki chungu nzima, wakati wa ile tarumbeta ya 7.

Hapa harusi bado maana wageni waalikwa wameachwa duniani.

a) "wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana tarumbeta ya mwisho itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa."
1Wakorintho.15.52.BHN, (Ufunuo 11:15-19)

b)
"Hili tunalowaambieni ni fundisho la Bwana, kwamba sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.

Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.

Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.

Basi, farijianeni kwa maneno haya."
1Wathesalonike.4.15-18.BHN

c)
“Basi, siku hizo, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.

Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.

Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.

Kisha atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu."
marko.13.24-27.BHN

d) "Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, “Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva.”

Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa."
Ufunuo.14.15-16.BHN

(Kuna wanaosema haya ni mavuno ya magugu. Mavuno ya magugu ni yanayofuatia, Ufunuo.14.17-20)

e) "Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari.

Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu).

Kisha malaika akaniambia, “Andika haya: Heri wale walioalikwa kwenye karamu ya harusi ya Mwanakondoo!” Tena akaniambia, “Hayo ni maneno ya kweli ya Mungu.”"
Ufunuo.19.7-9.BHN

iv) Ndipo Yesu anashuka, mpinga Kristo ananyang'anywa mamlaka na kutupwa kwenye ziwa la moto, na shetani aliye nyuma yake atafungwa kwa miaka 1,000.

a)
"Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake).

Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti."
Ufunuo.19.20.BHN

b)
"Lakini mahakama itafanya kikao; watamnyanganya utawala wake, nao utafutwa na kuangamizwa kabisa."
daniel.7.26.BHN

c)
"Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake.

Akalikamata lile joka – nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani – akalifunga kwa muda wa miaka 1,000.

Malaika akalitupa kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka 1,000 itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu."
Ufunuo.20.1-3.BHN

(Ni ufunuo pekee anayetaja miaka 1000)

v) Ndipo inafuatia sherehe / harusi. Huku huku duniani.

Bwana harusi: Yesu

Bibi harusi: Kanisa

Wageni waalikwa: Mataifa (Kuhusu mataifa: namba ix)

a) "NawaambiLeni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”
mathayo.26.29.BHN

b)
"Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.

Katika mlima huuhuu, Mwenyezi-Mungu ataliondoa wingu la huzuni lililowafunika watu wote, kifuniko cha uchungu juu ya mataifa yote.

Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote. Bwana Mwenyezi-Mungu ametamka.

Siku ile, watu wote watasema, “Huyu ndiye Mungu wetu! Tumemngojea atuokoe. Huyu ndiye Mwenyezi-Mungu tuliyemtazamia. Njoni tufurahi na kushangilia kwa kuwa ametuokoa.”"
isaya.25.6-9.BHN

vi) Watakatifu wanaoshuka na Yesu kuleta ghadhabu ya Mungu ni malaika, sio kanisa! Kanisa litakuwa huko juu.

a)
"na kuwapeni nafuu nyinyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake wenye nguvu"
2Wathesalonike.1.7.BHN

b)
"Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.

Kama vile magugu yanavyokusanywa na kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati;

Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu,

na kuwatupa katika tanuri ya moto, na huko watalia na kusaga meno."
mathayo.13.39-42.BHN

c)
"Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: Malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema"
mathayo.13.49.BHN

d)
"Mtu akinionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibu mtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu."
luka.9.26.BHN

vii) Utawala wa Yesu / Ufalme wa Mungu na watakatifu wake unakuwa umeanza hapa duniani. Watakatifu (kanisa) watatawala na Yesu kwa miaka 1000 ambayo shetani amefungwa
. Sala yetu mapenzi yako yatendeke duniani kama mbinguni inakuwa imejibiwa.

a)
“Lakini mahakama itafanya kikao; watamnyanganya utawala wake, nao utafutwa na kuangamizwa kabisa.

Ufalme, utawala na ukuu wa falme zote duniani watapewa watu wa watakatifu wa Mungu Mkuu. Ufalme wao utakuwa wa kudumu milele, na tawala zote zitawatumikia na kuwatii."
daniel.7.26-27.BHN

b)
"Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu.

Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka 1,000.

(Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka 1,000 itimie). Huu ndio ufufuo wa kwanza."
Ufunuo.20.4-5.BHN

c)
“Mshindi na mwenye kuzingatia mpaka mwisho mambo ninayotaka, nitampa mamlaka juu ya watu wa mataifa:

Atawaongoza kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama vyombo vya udongo."
Ufunuo.2.26-27.BHN

viii) Yesu na watakatifu wake watatawala mataifa kutokea Jerusalem.

a)
"Nitaurudia mji wa Siyoni na kufanya makao yangu mjini Yerusalemu. Mji wa Yerusalemu utaitwa ‘Mji Mwaminifu,’ na mlima wangu mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, utaitwa ‘Mlima Mtakatifu.’"
zekaria.8.3.BHN

b)
"Wakati huo, maji ya uhai yatabubujika kutoka mji wa Yerusalemu, na nusu ya maji hayo yatatiririkia kwenye bahari ya mashariki, na nusu nyingine kwenye bahari ya magharibi. Maji hayo yataendelea kububujika wakati wa kiangazi kama yalivyo wakati wa masika.

Wakati huo, Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye mfalme pekee wa dunia yote; naye atakuwa ndiye Mwenyezi-Mungu pekee, mmoja tu, na jina lake litakuwa ndilo jina pekee."
zekaria.14.8-9.BHN

c)
"Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko,

mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”

Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.

Kila mtu atakaa kwa amani chini ya mitini na mizabibu yake, bila kutishwa na mtu yeyote. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ametamka yeye mwenyewe.

....Nami Mwenyezi-Mungu nitawatawala mlimani Siyoni, tangu wakati huo na hata milele.”
Mika.4.1-7.BHN

(Isaya.2.2-4, Zekaria.2.10-13, Yoeli.3.16-17, Mika.4.8)

ix) Mataifa ni wale watakaooka dhiki kuu, yaani watakaomuamini Yesu wakati wa dhiki kuu. Watu hawa wataingia kwenye ufalme wa Mungu bila miili mipya, na ndio watakaokuwa wanazaliana na kutengeneza mataifa ndani ya ile miaka 1000. Watoto wao watapaswa kufundishwa kuhusu Yesu kama sisi leo.

a)
"Kisha, kila mtu aliyesalimika kati ya mataifa yote yaliyokuja kuushambulia mji wa Yerusalemu, atakuwa akija Yerusalemu mwaka hata mwaka, kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi aliye mfalme, na kuadhimisha sikukuu ya vibanda.

Iwapo taifa lolote duniani halitakwenda Yerusalemu kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi aliye mfalme, basi, mvua haitanyesha katika nchi yao."
Zekaria.14.16-17.BHN

b)
"Mwenyezi-Mungu asema, “Siku ile nitawakusanya walemavu, naam, nitawakusanya waliochukuliwa uhamishoni, watu wale ambao niliwaadhibu.

Hao walemavu ndio watakaobaki hai; hao waliochukuliwa uhamishoni watakuwa taifa lenye nguvu. Nami Mwenyezi-Mungu nitawatawala mlimani Siyoni, tangu wakati huo na hata milele.”
Mika.4.6-7.BHN

x) Kutajengwa hekalu Jerusalem. Kutakuwa na utaratibu wa ibada na kutakuwa a kutoa dhabihu.

a) Ezekieli 40-48
: Muongozo wa ujenzi wa hekalu, utaratibu wa kutoa dhabihu, siku kuu za kusherehekewa na mgawanyo wa ardhi kwa watakatifu wa Mungu,

hadi Yesu mwenyewe ana ardhi imetengwa kwaajili yake (Ezekieli 45).

b) Zekaria 14
imesema maji ya uhai yatatiririka kutoka Yerusalemu. Ezekieli 47 inaonyesha yanatokea ndani ya hekalu. Maji haya ya uhai ndo yatafanya watu wa mataifa waishi maisha marefu ingawa hawana miili mipya, kijana kabisa atakufa na miaka 100, na atakayekufa chini ya miaka 100 ni aliyelaaniwa. (Isaya 65:20) Hapa kifo bado kipo lakini itakuwa nadra.

xi) Kutakuwa hamna hatari yoyote wakati wa utawala wa Yesu wa miaka 1000. Itakuwa kama mbingu imeshuka duniani. Paradiso.

a) "Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, naye chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.

Ngʼombe na dubu watalisha pamoja, watoto wao watalala pamoja, na simba atakula majani makavu kama maksai.

Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka, naye mtoto mdogo ataweka mkono wake kwenye kiota cha fira.

Hawatadhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana kama maji yajazavyo bahari."
isaya.11.6-9.NEN

b)
"Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani, na viumbe vile vitambaavyo ardhini. Upinde, upanga na vita, nitaondolea mbali katika nchi, ili kwamba wote waweze kukaa salama."
Hosea.2.18.NEN

xii) Hapa bado dunia mpya haijaumbwa, lakini kutakuwa na mabadiliko kwenye dunia hii, hasa baada ya uharibifu mkubwa utakaotokea wakati wa dhiki kuu.

a)
"Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utaimarishwa kupita milima yote, utainuliwa juu ya vilima vyote. Mataifa yote yatamiminika huko,"
Isaya.2.2.BHN

b)
"Nilipofika huko niliona miti mingi sana kwenye kingo za mto.

Akaniambia, “Maji haya yanatiririka kupitia nchini hadi Araba; na yakifika huko yatayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji mazuri.

Kila mahali mto huu utakapopita, kutaishi aina zote za wanyama na samaki. Mto huu utayafanya maji ya Bahari ya Chumvi kuwa maji baridi. Kokote utakakopita utaleta uhai.

Wavuvi watasimama ufuoni mwa bahari, na eneo kutoka Engedi mpaka En-eglaimu litakuwa la kuanikia nyavu zao. Kutakuwa na aina nyingi za samaki kama zilivyo katika Bahari ya Mediteranea.

Lakini sehemu zake zenye majimaji na mabwawa kando ya bahari, hazitakuwa na maji mazuri. Bali hayo yatabaki kuwa maji ya chumvi.

Kisha ukingoni mwa mto huo kutaota kila namna ya miti itoayo chakula. Majani yake hayatanyauka wala miti hiyo haitaacha kuzaa matunda. Itazaa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu inapata maji yanayotiririka kutoka maskani ya Mungu. Matunda yake yatakuwa chakula na majani yake yatatumika kuponya magonjwa."
Ezekieli.47.7-12.BHN

c)
"Siku hiyo, atasimama kwenye mlima wa mizeituni ulio mashariki ya mji wa Yerusalemu. Mlima huo utagawanywa sehemu mbili na bonde pana sana litatokea toka mashariki hadi magharibi. Nusu moja itaelekea kaskazini na nusu nyingine kusini."
zekaria.14.4.BHN

xiii) Baada ya miaka 1000, shetani atafunguliwa kwa muda mfupi, na kama kawaida yake atakimbilia kuyapotosha yale mataifa yatakayokuwa yamezaliwa. Baadhi yao watadanganyika (yale yale Eden tutayashuhudia), watajaribu kumpindua Yesu.

Kile kitachotokea mwishoni mwa miaka 3.5 ya mpinga Kristo kitatokea tena mwishoni mwa miaka 1000, safari hii Shetani anatupwa kwenye ziwa la moto wa milele, we can call him the Eternal Loser.

a) "Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake,

naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani.

Nao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji unaopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza.

Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele."
Ufunuo.20.7-10.NEN

(Hapa nina andiko hili tu. Ezekieli 38,39 sio vita ya baada ya miaka 1000. Ile ni ya baada ya miaka 3.5 ya mpinga Kristo, na ni kivuli cha yatakayojirudia baada ya ile miaka 1000, kama ambavyo kuzingirwa kwa Yerusalemu mwaka wa 70AD na kuharibiwa kwa hekalu ni kivuli cha jinsi Yerusalemu itazingirwa mpinga Kristo atakapofunuliwa.

Labda swali linakuja: kwanini Mungu amfunge shetani kisha amfungulie?)

xiii) Baada ya shetani kushindwa tena na kwa mara ya mwisho kwenye historia ya uumbaji, na kutupwa kule anakostahili, ndipo kutakuwa na Hukumu ya wote waliowahi kuishi duniani, Hukumu ya kiti cha enzi cheupe.

Hapa ndio wakati kifo kinakomeshwa, hakuna wa kufa kijana wa miaka 100 tena baada ya hapa. Wale watu wa mataifa ambao hawakuasi watapewa miili mipya.

a) "Kisha, nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena.

Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.

Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; Kifo na Kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.

Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.

Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto."
Ufunuo.20.11-15.BHN

b)
"Maana sote ni lazima tusimame mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apokee anayostahili kwa matendo aliyoyafanya wakati alipokuwa anaishi duniani, mema au mabaya."
2Wakorintho.5.10.BHN

c)
"Hivyo kila mmoja wetu ataeleza kuhusu matendo yake mbele za Mungu."
Waroma.14.12.TKU

d)
"Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo. "
1Wakorintho.15.26.BHN

xiv) Baada ya hukumu ndipo dunia na mbingu mpya zinaumbwa, ambazo shetani na wafuasi wake na dhambi havijawahi kugusa.

a)
"Kisha, nikaona mbingu mpya na dunia mpya. Mbingu ile ya kwanza na dunia ile ya kwanza vilikuwa vimetoweka, nayo bahari pia haikuwako tena.

Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Kisha yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi akasema, “Tazama, nafanya yote mapya.” Tena akaniambia, “Andika jambo hili, maana maneno haya ni ya kuaminika na ya kweli!”

Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho."
Ufunuo.21.1-8.BHN

b)
“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya. mambo ya zamani hayatakumbukwa tena.

Furahini, mkashangilie milele, kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba. Yerusalemu nitaufanya mji wa shangwe, na watu wake watu wenye furaha.

Nami nitaufurahia mji wa Yerusalemu, nitawafurahia watu wangu. Sauti ya kilio haitasikika tena, kilio cha taabu hakitakuwako."
isaya.65.17-19.BHN

c)
"Lakini mbingu na dunia ya sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.

Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu."
2petro.3.7-13.BHN

(Nakaribisha masahihisho. Tumia kanuni hapo juu.)
 
SWALI:
Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

JIBU

HATUA YA UNYAKUO.
Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Hivyo anazidi kusema…

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.

Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani, na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye baada ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.

HATUA YA DHIKI KUU.
Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote (wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.

Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo. Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikira wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote wasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16). Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga (Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.

(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani. Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).

HATUA YA UTAWALA WA MIAKA 1000.
Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),

VITA YA GOGU NA MAGOGU
japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),

Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.

HUKUMU YA KITI CHEUPE CHA ENZI.
Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.

HATUA YA ZIWA LA MOTO.
Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…

Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9). Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.

Ubarikiwe sana.
MASOMO MENGINE YA BIBLIA UTAYAPATA HAPA CHINI
WINGU KA MASHAHIDI WA JEHOVA
 
Back
Top Bottom