Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Birth pangs / Utungu / Maumivu ya kujifungua

China


View: https://youtu.be/3f0gbeyUCE8?si=-vcjSZNk9knX8ZZp


Nigeria


View: https://youtu.be/6FcqrT9DKRk?si=1TDh7jewkqx8_btr



View: https://youtu.be/1lAbIXaA9Wc?si=Pjyaq1c4CDcUL4Yy



View: https://youtu.be/ofoejr2vB9M?si=rqRVZTTCf3lCSbxJ


Syria


View: https://youtu.be/85U8GqRSoGE?si=xOjn-sQ28iwhzPmU


View: https://youtu.be/iP-Qn03cSTY?si=6eS0j14ZPhZJNevL


"Hivyo, ni lazima watu wa Mungu, yaani wale wanaotii amri za Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu."

Kisha, nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”"

Ufunuo.14.12-13.BHN

"Aliye na masikio, na asikie!

Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani."

Ufunuo.13.9-10BHN"

"Kwa kuwa wewe umezingatia neno langu la kuwa na uvumilivu thabiti, mimi nitakutegemeza salama wakati ule wa dhiki inayoujia ulimwengu mzima, kuwajaribu wote wanaoishi duniani."
Ufunuo.3.10.BHN
 
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..

SWALI:
Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

JIBU

HATUA YA UNYAKUO.
Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Hivyo anazidi kusema…

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.

Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani, na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye baada ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.

HATUA YA DHIKI KUU.
Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote (wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.

Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo. Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikira wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote wasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16). Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga (Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.

(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani. Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).

HATUA YA UTAWALA WA MIAKA 1000.
Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),

VITA YA GOGU NA MAGOGU
japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),

Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.

HUKUMU YA KITI CHEUPE CHA ENZI.
Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.

HATUA YA ZIWA LA MOTO.
Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…

Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9). Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.

Ubarikiwe sana.
MASOMO MENGINE YA BIBLIA UTAYAPATA HAPA CHINI
WINGU KA MASHAHIDI WA YEHOVA


View: https://youtu.be/WwkbADQNQ6Q?si=tPDDtfL1LrJpxXlB

Japo sikuangalia ni post ya lini, hizo ni ndoto na kuamka utakuta dunia inasonga mbele. Hakuna wa kunyakuliwa zaidi ya kifo.
 
Hii Biblia ya Kiswahili ni version ya chini kabisa. Nenda version za juu kabisa za Kiaramu, Kigiriki au Kiebrania upate maana ya neno Mtakatifu.
Msifanye mambo kuwa magumu.
Yeyote aliyemkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi huyo ni Mtakatifu ataingia mbinguni.
Roho wa Mungu alikuwa kabla ya Yesu.
Amri zote zilikuwa kabla ya Yesu.
Hivyo ingekuwa amri zinatosha kufanya mtu awe holy hapakuwa na sababu ya Yesu kuja kuukomboa ulimwengu
Nakubali apo umeongea fact kabisa Yeyote aliendani ya Yesu ni mtakatifu,tatizo la.watu Ile yohana 3:16 wanaisoma juu juu sana yaan pale ndo imemaliza kila.kitu mbinguni ni kumuamini kristo tu hakuna ticketi nyingne
 

View: https://youtu.be/hkReRp1xJLk?si=UqlR720eJqtNh0Pv

1)Kuingia mbinguni sio rahisi njia ile ni nyembamba na imesonga,ila kupitia Yesu yote inawezekana.
2)Kumkiri Yesu pekee haitoshi ,kuwa na imani pekee haitoshi..MATENDO imani bila matendo imekufa.
Pia tuendende tukiongozwa na roho mtakatifu kujazwa roho mtakatifu na matunda yale ya roho mtakatifu yaobekane ..ROHO MTAKATIFU ndio tiketi yani utakatifu na matunda ya roho mtakatifu yale upendo,utu wema,n.k


View: https://youtu.be/hkReRp1xJLk?si=UqlR720eJqtNh0Pv
 
Gal 5:19-21
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Gal 5:16-26
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

1 Kor 6:9-11 SUV
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
 
Kama kumkiri yesu haitoshi Mimi kuingia mbinguni Kwa nini afe Kwa ajili ya dhambi zangu?
 
Zaburi 32 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.
² Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.
 
Kama kumkiri yesu haitoshi Mimi kuingia mbinguni Kwa nini afe Kwa ajili ya dhambi zangu?
Kwa sababu imeandikwa hata nikiwa na imani ya kuhamisha milima kama sina UPENDO mimi si kitu kabisa,sasa Upendo unaozungumziwa hapa ni upendo wa dhati ambao hausebau mabaya hautafuti mambo yake wenyewe,hauhukumu..upendo wa kiMungu 1)MPENDE JIRANI YAKO(penda watu wote hata wanao kuudhi au maadui) 2) Mpende Mungu wako..SASA UPENDO HU NI TUNDA LA ROHO MTAKATIFU..yani baada ya mtu kujazwa Roho mtakatifu ndani yake ndio hata nje matendo yake yanaonekana kwa sababu ya ile nguvu ya roho iliyoko ndani yake ndio inayoonekana mpaka nje
KWA KIFUPI ROHO MTAKATIFU/UTAKATIFU NDIO TIKETI YA KWENDA MBINGUNI

Ni kama ubatizo mpya ubatizo wa Roho mtakatifu

Sio wote waitao Bwana Bwana ,Yesu Yesu watauona ufalme wa Mungu.
Kuishi katika utakatifu matendo MATAKATIFU ni mazao yanayotokea matunda ya Roho mtakatifu baada ya kujazwa Roho mtakatifu.

View: https://youtu.be/C0x8mP1cvkI?si=eTgtJLS0Ea1-W3cC
 
Zaburi 32 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.
² Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.
Yesu alikuwa anawaponya watu na kuwasamehe dhambi zao lakini pia baada ya Yesu kuwaponya watu aliwambia ,umeponywa nenda LAKINI USITENDE DHAMBI TENA(sin no more)

maana ya usitende dhambi tena (SIN NO MORE) = UTAKATIFU.
Yn 5:14 SUV
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

KWANI LENGO LA YESU KUTUOKOA NA KUFA MSALABANI NI NINI?
Si ili atuponye na kutuokoa ROHO zetu,?anatuokoa/tuponya kutoka kwenye nini? si kutoka kwenye DHAMBI..Yesu anataka nini,si anataka TUACHE DHAMBI.
Yesu si anavuna Roho za watu anaokoa Roho ,mavuno ni kuacha dhambi tuishi maisha ya UTAKATIFU.
 
1 Kor 13:4-8
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

1 Kor 13:1-3
1 Kor 13:1-3 SUV

Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.


Gal 5:22-26 SUV
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana


Zab 16:3 SUV
Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

1 Pet 1:15-16
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.


View: https://youtu.be/C0x8mP1cvkI?si=rwrtt_vSOgkv_vs6
 
NGOJA TUZIKEE NAOMBAA
TUTARUDI TENA HUKU
 
Back
Top Bottom