Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Hivi punde tu Yesu anachukua/nyakua watakatifu wake walioko duniani..in no time..watu watanyakuliwa. Muda umefika

Zab 53:1
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.
 

Attachments

  • images - 2025-08-25T220710.368.jpeg
    images - 2025-08-25T220710.368.jpeg
    19.4 KB · Views: 14
1 Wathesalonike 4:16-17

16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele.


Matayo 24:37

37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.
 
Mkuu unaamini Kuna mzungu mwenye manywele mengi na mindevu yake atashuka mawinguni aje akunyakue mtu mweusi wewe!!
Mkuu unaamini Kuna mzungu mwenye manywele mengi na mindevu yake atashuka mawinguni aje akunyakue mtu mweusi wewe!!
Ufu 1:7-8
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
 
KATIKA KALENDA YA KIROHO MUDA UMETIMIA ,Unabii wote umeshatimia,ishara zote zimeshatimia...muda sasa umefika.sekunde yotote sasa watu wa Mungu walioko duniani watanyakuliwa kwenda mbinguni kuishi na Mungu,wenye dhambi wote wataachwa hapa duniani..

SWALI:
Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

JIBU

HATUA YA UNYAKUO.
Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema

Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Hivyo anazidi kusema…

Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.

Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani, na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye baada ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.

HATUA YA DHIKI KUU.
Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote (wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.

Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo. Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikira wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”

Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote wasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16). Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga (Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.

(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani. Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).

HATUA YA UTAWALA WA MIAKA 1000.
Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),

VITA YA GOGU NA MAGOGU
japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),

Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.

HUKUMU YA KITI CHEUPE CHA ENZI.
Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.

HATUA YA ZIWA LA MOTO.
Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…

Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9). Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.

Ubarikiwe sana.
MASOMO MENGINE YA BIBLIA UTAYAPATA HAPA CHINI
WINGU KA MASHAHIDI WA YEHOVA


View: https://youtu.be/WwkbADQNQ6Q?si=tPDDtfL1LrJpxXlB


View: https://youtu.be/k9sL2waYglg?si=-h6H6lJuwBlEDaiY

View: https://youtu.be/C0x8mP1cvkI?si=rwrtt_vSOgkv_vs6


View: https://youtu.be/euW2H-1fQ04?si=pb9UViABxH-9J5ri

unless uogea na Yesu. Kitu ambaco huwezu kuwa nachgi......acna hana na mambo ambayo huyajui. Usimchukulie yesu kifalalafala. Wenzako wamefeli na kuanguka
 
1 Wathesalonike 4:16-17

16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele.


Matayo 24:37

37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.
Amina Mtumishi
 
Dah Bora iwe hivyo aisee,tumechoka kukaa huku duniani
Hiyo siku ni nzuri tu kwa wale waliotayari wameshatafua mavazi yao kwa maana wamesafisha matendo yao na mioyo yao..

Amo 5:18

Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwani kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.

ILA NI SIKU MBAYA KWA WATAKAOACHWA DUNIANI...Dhiki kuu inakuja ..siyo kwamba kuna kupumzika ila NI MWANZO WA ULE MWISHO...,heri wanaofua nguo zao sasa na kuoshwa na kujisafisha .

View: https://youtu.be/k9sL2waYglg?si=3JqLfxcgt5Y8QpS7
 
Wenzenu wananyakua Mali zenu nyie mmepewa Unyakuo wa Mbinguni ambayo hata hamjui iko wapi...
Mambo ya mwilini ni hayo ya kupata chakula cha mwili na mali za duniani. MWILINI ,na siasa...AMBAYO SIYO MADA YA LEO.

ILA Mada iliyopo mezani LEO inahusu mambo ya ROHONI chakula cha ROhoni ,afya ya ROHONI/MAMBO YA KIROHO..

Mk 8:3
Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

Mathayo 6:20-21
Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba. Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.

Zab 37:1-18
Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili. Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka. Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri. Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila. Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya. Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi. Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo. Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake. BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja. Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, Wamwangushe chini maskini na mhitaji, Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu. Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe, Na nyuta zao zitavunjika. Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi. Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki. BWANA anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.

Kut 14:14

BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya
 
1 Corinthians 15:52
King James Version
52 In a moment, in the twinkling of an eye, at the last trump: for the trumpet shall sound, and the dead shall be raised incorruptible, and we shall be changed.

at the last Trump....some believes rapture will happen within this time when Donald TRUMP* is at his last second term of ruling US.(at the last TRUMP).
 
Back
Top Bottom