Hivi Rais Samia ameunda Wizara 2 tu?

Hivi Rais Samia ameunda Wizara 2 tu?

Ukiondoa Wizara zinazoongozwa na Nape na Makamba, hakuna Waziri mwingine anayesikika popote akiongelea chochote tofauti na tulivyozoea atleast.

Sisikii Waziri wa Viwanda, Elimu, Miundombinu hata WM mwenyewe ni nadra kumsikia, kwa nini ? Je, hawana morali ya kazi ? Hata Wizara ya Maji au ardhi kimya kimya tu, Wizara ya Mambo ya ndani/ njema c kimya.

Siyo dalili nzuri!
Kwanza hii dhana ya mawaziri kujizungusha ovyo nchi kavu na angani ni potofu sana.
Wizara ina watendaji na wataalamu... waachwe wafanye kazi zao.
Mawaziri wasubirie ripoti badala ya kuzunguka kutema mate huko na kule...
Delegation ingetusaidia sana kupunguza gharama na kujenga weledi
 
Bashe anafanya kazi nzuri sana kilimo kimeanza kuonekana ni ajira na kuwa na tija na thamani ya mazao imekuwa kubwa tofauti na siku za nyuma ambapo mkulima alikuwa ananufaika kwa asilimia ndogo sana na watu waliogopa kuingia kwenye kilimo.
 
Mohamed Mchengerwa he is doing a great job, Innocent Bashungwa pia anafanya vizuri, Bashe anafanya vizuri, Ummy Anafanya vizuri..
Inshort Baraza la Mawaziri liko vizuri na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano mama yetu Samia Suluhu Hassan analiangalia kwa jicho la ziada
 
Wazir anayepiga kazi ni Bashe , huyo jamaa habahatishi anachokifanya , anapambana Sana , to be honest pia Nape anajitahdi , Makamba ni Wazir wa hovyo kuwahi kutokea tangu hii nchi ipate Uhuru..mawazir wengine wote wapo neutralized , hawajui hata nini kinaendelea hii nchi , Kwa sasa wapo busy kujipimia kulingana na urefu wa kamba zao
Mbona wakulima tunahangaikia na kutafuta wakututetea ilimbolea ishuke, mpake Leo kila mtu yuko kimyaaaa.
 
ukiwa na boss ambaye yeye mwenyewe hana hiyo haiba tambua atawaambukiza uvivu, wee boss kila mara anaruka mambele huko...utafikiri hana mipango ya kuifanya nyumbani kwake, sasa wasaidizi wafanyaje inabidi wanyamaze. Mkuu akikosa maono imekula kwako, wasaidizi husubiri kuelekezwa wafanye yepi na kwa namna ipi?..sasa wamekosa wa kuwaelekeza lazima wakose dira. Nchi imekuwa kama kijiwe kila mtu anajiamulia lakufanya, boss mwenyewe hajui la kwenda nalo
 
Kwanza hii dhana ya mawaziri kujizungusha ovyo nchi kavu na angani ni potofu sana.
Wizara ina watendaji na wataalamu... waachwe wafanye kazi zao.
Mawaziri wasubirie ripoti badala ya kuzunguka kutema mate huko na kule...
Delegation ingetusaidia sana kupunguza gharama na kujenga weledi

Matumizi ya thamani za JWTZ ya angaliwe upya na kwa umakini.
 
Back
Top Bottom