Hivi Rais Samia amewahi kuandika Makala au Paper ya utatuzi wa changamoto za jamii?

Msomi asiye na nia njema ni tatizo, ni heri mpumbavu akupendaye.
 
Huwa hausomi zile nakala za uteuzi na utenguzi?
 
Hawa Watoto wamezaliwa Mkapa akiwa madarakani wanajifanya wajuaji sana,kumbe weupe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kwani Nyerere aliua Uchumi alio ujenga nani?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kwani baada ya kubinafsisha Wananchi wamenufaika vipi zaidi ya kutajirisha watu wachache!!?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na ujumbe wako kuanzia hapo kwenye 'vinginevyo' upo sahihi kabisa.

Hapo kwenye sentensi ya kwanza, Mungu naomba anipe uwezo wa kunyamaza, kuna vitu vinauma sana!
Magufuli alifoji Elimu kivipi wakati ata andiko lake alilopatia PhD lilitangazwa adharani?
Wekeni ushahidi wa kutosha,alifoji kivipi ili na sisi maamuma tuelewe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
..tafuta vitabu vya Edwin Mtei, na Andy Chande.

..naamini ukichanganya na uzoefu wako utapata full picture ya nini kiliangusha uchumi wetu.
Huyo Mtei si alikuwa kibaraka wa Wazungu!
Kilichoua Uchumi wetu ni uwizi na uvivu wa Watanzania, Mwalimu Nyerere alifanya kwa nafasi yake ila alizungukwa na wezi kama ambavyo ata sasa Rais kazungukwa na Wahuni!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Uwezo huo hana, to me samia, is "the president that was never meant to be"
Nchi hii ina bahati mbaya sana, Kikwete, Mwinyi(baba), Maghu,hawa walikuwa ajari mbaya kwa mustakabali wa TZ, madhara waliyoyafanya, itachukua miaka mingi 100+kulekebisha,
Sasa imagine, Mpango anakuwa Raisi wa nchi! Wizara tu ilimtoa kamasi,nilikutana nae kahama, yupo kwenye V8, na, bodyguards wake, wawili wana siraha, wanaibuka kwenye vituo vya kuuza mafuta, wanaanza kuulizia risiti kama zinatolewa! Wakasumbua sana mameneja wa vituo vya mafuta! Kwa ukubwa wa nchi hii, unawezaje kutumia hii mbinu kucheki kama risiti zinatolewa!
So pathetic!
 
Kwani baada ya kubinafsisha Wananchi wamenufaika vipi zaidi ya kutajirisha watu wachache!!?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Nakupa mfano wa kiwanda cha pombe cha TBL na benki ya CRDB, hizi zote zilikuwa chini ya serikali ya Nyerere na vilikuwa vifilisika, je kwa sasa havinufaishi wananchi?
 
Kwani Nyerere alirithi Uchumi gani toka kwa Wakoloni mpaka aka ufulisi?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Wakoloni waliacha bandari, mashamba makubwa na ranchi, viwanda, benki...vilivyokuwa vikitoa ajira na kulipa kodi kwa serikali, Nyerere alipoingia akawapora watu binafsi waliokuwa waliokuwa wakiendesha kwa ufanisi na kuwakabidhi watu wake kutoka TANU (CCM) na wakishindwa kuviendesha sababu ya elimu ndogo, rushwa na uvivu na kuviua
 
Kushinda kwenye bao na alkasusi ndiyo kufungua ubongo?
 
DP World wapo au hawapo?

Vipi ile mikataba ya Kibudu wa jalalani na Profesa uchwara wa madini? Nasikia tunainya mipesa sasa hivi.
Mikataba ilisainiwa mchana kweupe, siyo hii ya kwenu isaiiwa na waarabu kwao
 
Excellent. Kibaya zaidi katika yote haya, alitaka taasisi na mashirika yote yasimamiwe na makada wa TANU/CCM walioidhinishwa na yeye kama mwenyekiti wa chama (CC).

Hata vyama vikuu vya ushirika alivyovikuta vikiwa huru na kuwa na nguvu kubwa sana kiuchumi nchini alivivunja ili kuua nguvu na jeuri ya wenyeviti wake. Baadaye akavianzisha tena chini ya wenyeviti waliokuwa vetted na CCM! Ndio ilikuwa mwisho wa vyama makini vya ushirika na jeuri ya mkulima wa Tanzania.

Alijali sana utii (loyalty) kuliko sifa nyingine zote. Alikuwa tayari hata kuvumilia baadhi ya wezi na wala rushwa wanaomtii na kumpigia magoti kuliko weledi wanaokosoa mawazo yake. Ajabu yeye binafsi aliuchukia sana wizi na ufisadi. Lakini kukosolewa mawazo yake ilikuwa inmpandisha hasira zaidi. Hapo ndipo unafiki wa watendaji serikalini katika mnyororo wa kusimamia rasilimali za umma na uchawa (kula na wakubwa) ulipoanzia.
 
Kama ungekuwa unayajua, usingehusisha Lonrho na kiwanda cha Valmet.
 

..Mimi naamini sera za UJAMAA zilikuwa na athari kubwa kwa mashirika ya umma kuliko wizi.

..Kwa mfano, lila shirika la umma lilikuwa na tawi la Ccm, na tawi la Juwata.

..Sasa ukizingatia sera ya CHAMA KUSHIKA HATAMU ni kwamba Ccm na Juwata ktk taasisi ya umma walikuwa na uwezo wa kuingilia maamuzi ya management.

..Vilevile mashirika haya yalibebeshwa mizigo mikubwa ya huduma za kijamii kabla hata hayajaimarika.

..Haikuwa ajabu kukuta shirika la umma lina timu za mpira wa miguu, netball, bendi za muziki, mabasi ya kusafirisha wafanyakazi, etc.

..Ukiacha hayo, mashirika ya umma yalikuwa yanashindana kuwa " CHAWA " wa Ccm kwa wakati huo. Kila Mkurugenzi au Meneja Mkuu alikuwa anataka kumzidi mwenzake kwa kuchangia shughuli na mikutano ya Ccm.

..Kwa kifupi mashirika ya umma yalikuwa hayazingatii kanuni za biashara. Kukosa umakini ktk idadi ya waajiriwa ilikuwa moja ya changamoto. Na Meneja yeyote aliyejaribu kujenga hoja kwamba kampuni uendeshe kibiashara alipigwa vita kuwa analeta mambo ya ubepari, ubeberu, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…