Hivi Rais Samia anashikwa na "kigugumizi" gani kutoamuru Kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe ifutwe bila masharti yoyote?

Hivi Rais Samia anashikwa na "kigugumizi" gani kutoamuru Kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe ifutwe bila masharti yoyote?

Ni dhahiri sasa kwa kila anayeifuatilia Kesi ya ugaidi ya kina Mbowe, ameshabaini kuwa hiyo Kesi ni ya michongo na mashahidi wanaoletwa hapo mahakamani pia ni wa michongo!

Hivi unawatuhumu watu kwa ugaidi, halafu kila shahidi anayetoa ushahidi hapo mahakamani anaonekana kuwa amepangiwa ya kusema Ili awatie hatiani akina Mbowe?

Inafahamika wazi kuwa Ili Mahakama iwatie hatiani watuhumiwa, ni lazima upatikane ushahidi usio na shaka yoyote Ili watuhumiwa wahukumiwe kwenda jela.

Kwa mujibu wa ushahidi uliokwishatolewa hadi hivi sasa, hakuna ushahidi wowote wa kuwatia hatiani akina Mbowe, bali ni kuendelea kuwatesa kwa kuendelea kuwaweka mahabusu kina Mbowe kwa kipindi kirefu.

Hivi unawezaje kuwaita watu watuhumiwa wa ugaidi wa kulipua vituko vya mafuta, Ili Hali ushahidi uliotolewa hadi hivi sasa, hauonyeshi sehemu yoyote kuwa watuhumiwa hao walipanga njama za kulipua vituo hivyo vya mafuta?

Unawezaje kuwatuhumu watu kwa ugaidi, huku ukiieleza Mahakama, kuwa eti mtuhumiwa wa kwanza Mbowe, alifadhili ugaidi huo kwa kumtumia pesa mtuhumiwa mwingine shilingi elfu 80 tu?

Unawezaje kuwatuhumu watuhumiwa kuwa walipanga kumuua Sabaya, wakati mashahidi wenu wakidai kuwa hakuna sehemu yoyote Kati ya sms walizozi-hack, iliyomtaja Sabaya kutaka kuuawa?

This must be a joke of the year 😁

Kwa wakuu wa Serikali, akiwemo Rais Samia na IGP Sirro kuutangazia Ulimwengu kuwa wamemkamata Mbowe, wakiwa na ushahidi usio na shaka yoyote kuwa Mbowe alipanga njama na watuhumiwa wenzake kufanya ugaidi wa kulipua vituo vya mafuta na kupanga magogo Barabarani kwa lengo la kutaka nchi yetu isitawalike

Tufike mahala ambapo Mahakama zetu zisimuone Rais Samia kama mungu- mtu na zitambue kuwa yeye ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, ambaye anaweza kukosea kwa matamshi yake na matendo yake na zihukumu kwa Haki kwa kuifuta Kesi hiyo ya ugaidi ya akina Mbowe, ambayo imeliletea aibu kubwa Sana Duniani kwa watawala wetu kuweza kuwabambikia Kesi kubwa ya ugaidi
Wanaogopa uchaguzi 2025
 
Kaka hebu subiri kwanza Mzee wa watu atoke ndio uongee hayo mambo,

Watu akienda kuomba mambo yakianza kuwa mazuri mnaanza kuja na hoja zenu hapa then mambo yanabadilika

Hakuna watu wanashindana na serikali duniani kote

Ww unaandika ukiwa home na familia yako mwenzako tangu mwaka Jana Yuko jela
Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba hata wewe unaamini kwamba Mbowe alibambikiwa kesi kwasabau ya kuisumbua serikali, right?
 
Mbowe ni tishio la kisiasa tanzania,ili amani iendelee kutamalaki kwa tafsili yao ni Mbowe afungwe hata kama hana hatia.
 
Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba hata wewe unaamini kwamba Mbowe alibambikiwa kesi kwasabau ya kuisumbua serikali, right?

Tuko Africa, shida yenu mnajifanya kama mnaishi ulaya

Hata ww leo unaweza kupewa kesi ya kubaka na ukafungwa ukapotea kabisa hii ndio africa and I can't change it

Ndio maana uwa nawashangaa watu ambao wanalilia katiba mpya, hakuna rais wa Africa anataka katiba mpya unless hiyo katiba iwe upande wake

Hata ww Leo ungekuwa ni rais katiba mpya usingekubali
 
Umepotoka
 
Mimi sijakataa; ninacho kisema ni kwamba, kumbe ni kweli kwamba Mbowe kabambikiwa kesi sio?
 
Muhimili mmoja hauwezi kuingilia muhimili mwingine.

Au siku hizi mmeacha kuhubiri demokrasia?

Yaani unakurupuka na thread ya utetezi JF?mawakili wenu wameshawajulisha kuwa maji yamemfika shingoni sasa mnasaka public sympathy.
Huna akili
 
Samia yawezekana alitaka maovu ya mtangulizi wake yaanikwe.
 
Ipo haja ya wote waliobumba kesi hii ya uongo wachukuliwe hatua. Wakiwemo siro, kingai, mahita jumanne gudlack majaji na mahakimu wote waliojiingizia pesa haramu kama posho mbalimbali za kushiriki kesi ya uongo na kuitia hasara kodi yetu.
Hio gharama ya kuendesha kesi si ingenunua hata madawati.
 
Back
Top Bottom