Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Wewe Ndio Mtanzania pekee unae miss milio ya bunduki...
Majambazi wengi wako kwenye ripoti ya mkaguzi mkuu .
Kuuliza sio ujinga. Kunaweza kukawa na ujambazi unaendelea kumbe taarifa ndio zipo.

Hao wa kwenye rippti walikuwa wengi zaidi enzi za yale majambazi ya risasi kuliko hata siku hizi. Wenda na wao wameadvance au wanakula za halali.
 
Yamebaki makaburi na picha za kumbukumbuku.. Hiyo awamu iliyopita haikuwa na msalie mtume.. Walifuatwa waliko wakamalizwa huko huko kimya kimya
Hawa waliobaki kwa haya tunayopitia hata sisi wanatuonea huruma
Hii ilikua ni kazi iliyotukuka kutoka kwa Mafwele.(apewe maua yake).

Alisifiwa kukimbia, naona kapitiliza home
 
Siku hizi wengi hawatembei na pesa miamala inafanyika kielectroniki au kwa njia ya benki

pongezi kwa polisi, maana walikua wanawapoteza pasipo kuwafikisha mahakamani, itakuwa wamepungua na wengine kufanya mambo mengine
 
Ujambazi umepungua kwa sababu kuu moja watu sasa hivi hawatembei na cash.mitandao ya simu imesaidia sana mawakala wa mabenki wametapakaa kila mahali zamani wakiteka basi Wana uhakika wa makusanyo ya kutosha sababu watu walitembea na cash.sasa hivi unateka basi watu hawana pesa mtu unakuta Ana elfu kumi tu ya kula
 
Mambo yanabqdilika kwa kasi. Hata ukiacha sekta hii ya uharifu hata sekta nyingin4 halali zinabadilika au badil8shwa kwa kasi sana mtu aspojiongeza anaweza kudhali kalogwa kumbe amegoma kubadilika.
 
Acha tupumzike kidogo mkuu hapo nyuma tumepitia hekaheka nyingi sana,

Majambazi yalikuwa yanajiamini hatari, unashangaa eti Bank imevamiwa unajiuliza mara mbili mbili yaani inawezekanaje Bank kuvamiwa!!

Sasa kama Bank wamevamia sisi tulioko huku Mziha tunafanya biashara ya Ngo'ombe wakituotea itakuaje!!

Baadhi yetu tuliandika wosia kwa kazi zetu
 
Sahihi
 
Nchi za kiafrica na tawala zake ,hata majambazi na wachawi kuna muda wanatuonea huruma.just jokes. Kwa kweli Jeshi la polisi linahitaji pongezi mnoo kwa hili la kuutuliza ujambazi kiasi tunasafiri masaa 24 nchi nzima
 
Hapo kwa mwendo wa ngiri umesahau mkia juu😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…