Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Kwenye awamu ya JPM waliuwawa na kufungwa sana. Vibaka na majambazi walipotezwa mno. Wengi walikimbilia SA ambako nako wengi wameuwawa.
Alisaidia sana, Japo kwa sababu shetani hajafa wakipata mwanya atashawishi wengine watusymbue. Ilq tunaomba amani ya kitaifa na ya mmoja mmoja. Ni uhai kwanza.
 
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru mamaaa Samia🙏
Maana toka aingie madarakani majambazi waliokuwa mtaani wamerudishwa serikalini

Uzuri ameyaambia yale kwa urefu wa kamba,, japo Kuna mengine hayana kamba
 
Tunafanya kazi yetu vzr
 
Majambazi wengi wamemalizwa na polisi, kwani ukuaji wa technology umerahisisha sana kuwakamata majambazi, yaani hata akimbilie wapi kwa jinsi Cyber unit ya police wetu iko advance sana, sasa majambazi wao bila simu hawawezi fanya kazi, so walinaswa kama kuku na kupotezwa..

Pili, sbb ya technology miamala ya fedha mingi ni mitandaoni, watu hawana cash kabisa siku hizi, yaani huwezi mkuta mtu ana mil 2 au 3 cash anabeba, fedha zote ziko mitandaoni, sasa majambazi ataibia nini? Yaani huwezi kuta mtu ndani ya nyumba au kwenye gari kabeba mil 5, yaani sio rahisi na haipo, maana hakuna sbb ya kubeba mzigo wakati fedha ukitaka kiasi chochote unatoa kwa simu yaani easy access to money online na katika mitandao ya simu imeondoa cash payment au kubabe fedha nyingi kuvutia uwizi..!!

Ila kubwa zaidi ni Polisi wetu wamefanya kazi kubwa sana sanaaa, pongezi ziende kwao.!!
 
Hongera sana kwa Jeshi la Polisi.
 
Ukiona ualifu umeongezeka kuanzia mtaani jua hali ya uchumi ni mbaya na ukiona umepungua jua ni kinyume chake, hakuna cha polisi kuwa imara au nini, kibaka mmoja aliwahi kusema wakiwa na hali mbaya mfukoni sehemu nzuri na rahisi ya kuiba ni polisi na mahakamani.
 
Majambazi yote yapo si si emu! Wakati huu yanakula kwanza hela za uchaguzi. Yakitoka huko, shughuli inaanza tena.
 
IGP wa sasa yeye anasifika mno kwa kushughulikia majambaka!! Ni mwendo wa chuma tu!

Naona majambaka wengi wakaona wahamie kwenye “ile pesa tuma kwenye namba hii”.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…