Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Mwaka flani yaliteka basi na kuwapora Kila kitu Hadi nguo Kisha yakawaambia waanze kuimba wimbo wa "Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe."
Huku wakiwa uchi mhanga mmoja wa tukio Hilo alikuwa wa kijijini kwetu. Waliimba badae yakatokomea na nguo maporini gari iliyokuja na kuwakuta wako uchi ilibidi itoe taarifa police wakaja na mashuka Yale ya minadani mwaka2002 kama sikosei
 
We jamaa umenikumbusha mwanzoni mwa miaka ya 2000 huko mkoani walikuja majamaa wale mbavu nene imepanda hewani watatu na kila mmoja na sub machine gun yake full kujiamini , walikuja kwa boss wa boti za uvuvi yule mpemba alikua anakaa na pesa ndani kama milioni 150 hivi ,basi wawili wakaingia ndani , alafu moja likabaki nje

Mpemba akaminywa na mkewe kilio kikamtoka majirani wa kwanza kufika kutoa msaada wakakuta jamaa halina hata time tena limewasha sigara chuma mkononi ,
Basi wale wa kwanza wakaanza kurudi mbio kwa mayowe makubwa sanaaaa " jamani ni majambazi sio wezi kimbieeeni basi unajua kilichotokea? WA MWISHO ALIKUA WA KWANZA🤣🤣🤣🤣
 
Kabla ya awamu iliyokatishia njiani na hii ya sasa ilikuwa haipiti wiki unasikia watu wamevamiwa, majambazi yameuwawa ila siku hzi hizo habari hazipo kwa kasi ile.

Cha ajabu sikuhizi vimeibuka vituo vingi (benk ndogo) mitaani vinavyofanya kazi kwa miamala ya simu na Benki. Zamani ikifika saa 12 vituo hivi kama sio kufungwa basi hawawezi kufanya miamala zaidi ya 100K. Sasa hivi hata 1M unaweza kutoa usiku na hakuna matata.

Sababu ya huu ushwari ni nini?

1: Majambazi yalitokomezwa kabisa?
2: Jeshi la Polisi liko imara?
3: Majambazi wametafuta shughuli za kufanya au wameadvance zaidi?
4: Upo ila taarifa ndio wengi hatuzipati?
5: Mama anaendelea kuupiga wa kutosha?

Ni hayo tu.
Ni tukio gani ambalo hautalisahau.
NambA 1, 2 na 5 ni hao hao, wameelewana kufanya yao kwa jinsi tofauti!
 
Kipindi kile, ukikutwa na Bunduki ni bye bye 👋.

Ukishapewa kisago ukataja wenzako, wanakuchukua unaingizwa porini kisha unakula ya kichwa stori imeisha.

Huu mfumo ulianzia kenya, watu wLikua wanapigwa risasi waziwazi maeneo kama kkoo mbele ya kadamnasi.


View: https://youtu.be/pOjYnSAAcnQ?si=Px9Fz94638UZd7Xk

Bonge moja la Documentary niliifuatiliaga kitambo kidogo ilikua mwaka 2021 UKITAKA UIELEWE USIRUKE RUKE ANZA NAYO MWANZO NI KAMA MOVIE VILE
 
Huu mwaka ulioweka ni sahihi?


Maana hii tabia inasemwa ni ya Rais aliyetangulia mbele ya Haki (2015-2020).
Uchumi umeimarika , maadili na michongo imekuwa mingi,
Jeshi la polisi liko imara sana, mpaka wao Sasa ndio wamekuwa watekaji na wauwaji wa raia.

Ukuwaji wa technology imesaidia sana ujambazi kupungua.

Nakumbuka tukio la kkkt kimara, zilikuja defenders 3, zikiwa na njemba kama 6 ivi, wakawafungia waumini ndani ya kanisa hakuna kutoka MTU, wakaingia jengo la muasibu , wakatoa pipe wakapewa sadaka za makusanyo ya juma2 hio, ZaidI ya mil35 .
Walitokomea kusikojuliiana huku defender MOJA ikibaki kuhakikisha wale walio tangulia hawafuatiliwi, nao baadae wakatokomea kwa mwendo wa ngiri. 2012
 
Kabla ya awamu iliyokatishia njiani na hii ya sasa ilikuwa haipiti wiki unasikia watu wamevamiwa, majambazi yameuwawa ila siku hzi hizo habari hazipo kwa kasi ile.

Cha ajabu sikuhizi vimeibuka vituo vingi (benk ndogo) mitaani vinavyofanya kazi kwa miamala ya simu na Benki. Zamani ikifika saa 12 vituo hivi kama sio kufungwa basi hawawezi kufanya miamala zaidi ya 100K. Sasa hivi hata 1M unaweza kutoa usiku na hakuna matata.

Sababu ya huu ushwari ni nini?

1: Majambazi yalitokomezwa kabisa?
2: Jeshi la Polisi liko imara?
3: Majambazi wametafuta shughuli za kufanya au wameadvance zaidi?
4: Upo ila taarifa ndio wengi hatuzipati?
5: Mama anaendelea kuupiga wa kutosha?

Ni hayo tu.
Ni tukio gani ambalo hautalisahau.
Ujambazi wa silaha hakuna nyakati hizi either umepungua ila misala imehamia mitandaoni kwa sasa. Ndo watu wanakovamiwa.
 
Yamebaki makaburi na picha za kumbukumbuku.. Hiyo awamu iliyopita haikuwa na msalie mtume.. Walifuatwa waliko wakamalizwa huko huko kimya kimya
Hawa waliobaki kwa haya tunayopitia hata sisi wanatuonea huruma
Sure ,awamu ya jiwe ilifanikiwa sana kulala nao "MBERE" ,hata Panya Road nao walitangulizwa mawinguni...Ukicheka na Nyani utavuna mabua ,walikuwa wakikamata jambazi wanachukua chain yao yote wanaenda kula VYUMA.
 
Back
Top Bottom