Aisee umenikumbusha ule mtiti wa wale washenzi , ilikuwa ni balaa 2004 kama sikosei hiyo mzee , actually Mimi nilikuwa mhanga wa hao wapuuzi , nilikuwa nakaa na wazazi wangu mtaa wa Kiloleli - Mwanza , Tulivamiwa usiku mmoja wale wapuuzi walikuwa wanavunja milango kwa mawe flani yanaitwa Fatuma .
Na walikuwa wanafunga mtaa ,njemba thelathini , na wana magobole na silaha nyingine kali ,panya road wakasome .
Aisee nakumbuka siku hiyo ile nyumba niliyokuwa nakaa walipiga sana na kujeruhi watu na wengine wanawake walibakwa kabisa .
Yale majamaa sitasahau kabisa ,na sehemu au pango walilokuwa wanajificha ni hapo juu ya kilima cha wakatoliki karibia na Pàrokia ya Kiloleli na shule ya Montessori .
Yalikuwa yanajificha hapo halafu usiku yanaingia mtaani kukinukisha ,halafu wengi walikuwa wakurya ,
Siku wanaenda kufurushwa mle aisee zilipigwa risasi zaidi ya masaa sita na polisi ila walifanikiwa kuyaua mwishoni ,ila naamini kuna mengine yalitoroka .
2004 -2005 ilikuwa miaka hatari sana Mwanza kwa ujambazi wa kutumia silaha