Hivi Tanzania inamilikiwa na nani. CCM, Dola, au kila Mtanzania?

Hivi Tanzania inamilikiwa na nani. CCM, Dola, au kila Mtanzania?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kuna wakati nawaza sana kuwa nimo kwenye nchi ambayo sijui kama mimi ni mmiliki wake ama nani ndiye anayeimiliki. Nadharia ziko nyingi lakini sijaona hata moja inayonifanya nijue nani hasa ni mmiliki wa hii nchi ninayoishi. Kila siku nikiwaza umiliki wangu kwa Tanzania nautilia shaka sana?

Ukiangalia kwa undani maana ya umiliki inahusisha pia uwezo wa kufanya jambo lolote kwa unachokimiliki. Ukisema huyu ni mke wangu lakini ikifika usiku anakwenda kulala na jamaa nyumba ya jirani, hapo lazima kutakuwa na walakini.

Ni jambo gani labda linaloonesha sisi watu wa kawaida kwamba tunaimiliki Tanzania? Kuna jambo gani linalotupa imani kwamba kweli sisi ndiyo wamiliki wa nchi yetu?

Wewe binafsi unajiona kwamba ni mmiliki halisi wa Tanzania?
 
[emoji2962]
JamiiForums-935695326.gif
 
Nchi hii inamilikiwa na kikundi kidogo cha watu ambacho kimejishikisha kwenye vyombo vya dola.Ww ona watu kama akina Wasira teuzi wanarenewed wakati nchi ina watu kibao wenye nguvu ambao ni potential kabisa.Hao akina Wasira wamekuwa serikalini tangu enzi za mwalimu na ulikuwa muda wa kupumzika na kulea wajukuu
 
Sijasoma mada, ila majibu yangu kwa kufuata heading,

Kwa mujibu wa google, Tanzania inamilikiwa na mtu mtu mmoja anaitwa Mohamed Dewji.

Ahsante

REF: GOOGLE:
Who is the owner of Tanzania?

NB: Vitu vingine tusichukulie serious sana.
 
Back
Top Bottom