Hivi Tanzania inamilikiwa na nani. CCM, Dola, au kila Mtanzania?

Hivi Tanzania inamilikiwa na nani. CCM, Dola, au kila Mtanzania?

Kuna wakati nawaza sana kuwa nimo kwenye nchi ambayo sijui kama mimi ni mmiliki wake ama nani ndiye anayeimiliki. Nadharia ziko nyingi lakini sijaona hata moja inayonifanya nijue nani hasa ni mmiliki wa hii nchi ninayoishi. Kila siku nikiwaza umiliki wangu kwa Tanzania nautilia shaka sana?

Ukiangalia kwa undani maana ya umiliki inahusisha pia uwezo wa kufanya jambo lolote kwa unachokimiliki. Ukisema huyu ni mke wangu lakini ikifika usiku anakwenda kulala na jamaa nyumba ya jirani, hapo lazima kutakuwa na walakini.

Ni jambo gani labda linaloonesha sisi watu wa kawaida kwamba tunaimiliki Tanzania? Kuna jambo gani linalotupa imani kwamba kweli sisi ndiyo wamiliki wa nchi yetu?

Wewe binafsi unajiona kwamba ni mmiliki halisi wa Tanzania?
Familia za maraisi wastaafu,ikiongozwa na Kikwete hao ndio wanaomiriki bongo kwa sasa,state ipo captured na hii familia,hakuna mradi,shughuri ya serikali itafsnyika kama inaenda kinyume na hii familia na wapmbe,marafiki zao
 
Back
Top Bottom