Hivi Tanzania tuna cyber army?

Hivi Tanzania tuna cyber army?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nilikuwa naangalia Documentary moja inaitwa Zero Days. inaelezea namna Marekani na washirika wake waliweza kushambulia mitambo ya nyuklia ya Iran kwa kutuma kirusi cha kompyuta (STUXnet). kirusi hicho kilisababisha mitambo ya Iran iwe inalipuka.

wairan wakajifunza kitu na kuamua kuunda jeshi lao la mtandaoni. moja ya kazi ilizofanya ni kushambulia mitandao ya benki za Marekani na mifumo ya umeme. Pia waliishambulia Uturuki na kuzima umeme nusu ya nchi kwa saa 12.
hii ni vita mbaya sana. inaweza zima umeme, mawasiliano ya simu, mitambo na ndege za kijeshi, mifumo ya maji safi na salama, traffic control, mifumo ya benki na fedha. kifupi nchi inaweza rudi stone age ndani ya dakika. Assume tushambuliwe kwenye mifumo yetu ya simu-pesa?
je Tanzania tuna jeshi la mtandaoni?
 
mkuu nia ni kweli innawezekana ikawepo lakini ? kondoo na kuku wana weza kushindana kugonganisha vichwa ?
hawawezi mkuu. Ila kwa mtazamo wangu hii ni sehemu ambayo hata nchi masikini zinaweza kufanya vizuri maana mtaji mkubwa ni ubongo unaochemka.
 
jana korea kusini wamekiri kuwa Cyber command yao imeingiliwa na kuna siri za jeshi zimechukuliwa. wanashuku ni korea kaskazini

hawawezi mkuu. Ila kwa mtazamo wangu hii ni sehemu ambayo hata nchi masikini zinaweza kufanya vizuri maana mtaji mkubwa ni ubongo unaochemka.
mkuu, ndio maana nikasema ubongo wetu bado saana...!! hata kiwanda cha redio masafa ya AM ni tabu, tukazanie masomo ya sayansi mashuleni mkuu. sayansi watoto hawaelewi kwa sababu ya lugha, wanapofahamu lugha umri wa utundu wa kudadisi umeshapita ana madigrii ana fikiria kuoa, akiwa na familia anatembea na nadharia hakuna udadisi wala vitendo..!! umenipata mkuu ?
 
safi sana... umeielezea vzuri mkuu
 
ha ha tz tunaweza kuweza lkn tutakuwa tumeachwa tukitaka kuwaacha tujifunze kisha tuanze kufikiri zaidi yao!
 
Wanajeshi wa bongo ni hodari kwa kukimbia mbio, kupiga raia, kufanyiana ubabe na askari wa usalama barabarani, kujisifi mitandaoni utawasikia " unachezea baka baka wewe?"

Watu wana D mbili kwenye vyeti, Darasa la saba, mwenye degree sociology kaingia jeshini ili apate nyota [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hua nalitamani jeshi la North Korea wana cyber army imara kinoma
Hawa hapa chini
Bureau 121 - Wikipedia
 
mkuu, ndio maana nikasema ubongo wetu bado saana...!! hata kiwanda cha redio masafa ya AM ni tabu, tukazanie masomo ya sayansi mashuleni mkuu. sayansi watoto hawaelewi kwa sababu ya lugha, wanapofahamu lugha umri wa utundu wa kudadisi umeshapita ana madigrii ana fikiria kuoa, akiwa na familia anatembea na nadharia hakuna udadisi wala vitendo..!! umenipata mkuu ?
nimekupata vema mkuu. naona awamu hii wamejitahidi kuweka msisitizo kwenye sayansi. ila hili swala la lugha linafanya hata tendo la kujifunza liwe la polepole sana.
 
napenda sana watu waelewa, mara nyingi najiuliza kwa nini wachina ambao tunaenda kuomba msaada elimu yao wameiweka katika lugha yao ? na lugha nyingine zimekua za ziada ? what is the reason behind ? cant we reason ourself ? tell me mkuu ?
 
naona prestige ambayo iko associated na kiingereza ndiyo inafanya tuwe wagumu kuchukua hatua. hili ni tatizo kubwa, utafiti unaonyesha ni 15% tu ya wanafunzi wa sekondari ndiyo wanaelewa kiingereza kiasi cha kuitumia kama lugha ya kujifunzia.
 
Back
Top Bottom