Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Nilikuwa naangalia Documentary moja inaitwa Zero Days. inaelezea namna Marekani na washirika wake waliweza kushambulia mitambo ya nyuklia ya Iran kwa kutuma kirusi cha kompyuta (STUXnet). kirusi hicho kilisababisha mitambo ya Iran iwe inalipuka.
wairan wakajifunza kitu na kuamua kuunda jeshi lao la mtandaoni. moja ya kazi ilizofanya ni kushambulia mitandao ya benki za Marekani na mifumo ya umeme. Pia waliishambulia Uturuki na kuzima umeme nusu ya nchi kwa saa 12.
hii ni vita mbaya sana. inaweza zima umeme, mawasiliano ya simu, mitambo na ndege za kijeshi, mifumo ya maji safi na salama, traffic control, mifumo ya benki na fedha. kifupi nchi inaweza rudi stone age ndani ya dakika. Assume tushambuliwe kwenye mifumo yetu ya simu-pesa?
je Tanzania tuna jeshi la mtandaoni?