Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Haihitaji mazungumzo sana.japo nimeiacha Kwa Sasa napanga kubadili.lakini kwanini kama unajua mtu ana shida usiwe sehemu ya msaada kwake badala uwe kikwazo kwake?
Unajua huyu mtu ana weza kupata tabu kufanya hiki ila mie naweza sogea Kari u saidia kuliko kukaa mbali na kushoot "hawezi huyo"
Then unaendelea na yako.inaleta matokeo gani?

Na sio Kila biashara inamudu kumlipa mtu.wengine ndo tunaanza from scratch
Kama unafanya Biashara inayohitaji mazunguzo Sana tafuta msaidizi wa kuwa nae katika eneo lako la Kazi .
 
Sawa pole utapata msaada
 
Tunawavimilia but wanaumiza
Ndio walimwengu, ni mwendo wa kuvumiliana tu na kuishi kwa kujizingatia wewe kwanza then ndio uanze kuchagua watu wa kuwa nao karibu kwa maana wale ambao wanakuzingatia na wewe unawazingatia wasio kuzingatia unapiga chini.
 
Ndio walimwengu, ni mwendo wa kuvumiliana tu na kuishi kwa kujizingatia wewe kwanza then ndio uanze kuchagua watu wa kuwa nao karibu kwa maana wale ambao wanakuzingatia na wewe unawazingatia wasio kuzingatia unapiga chini.
Asante.nimeelewa
 
Kama unasikia kiasi naona sio sawa watu kudakia kwa watu wanaokusemesha ila kama husikii kabisa, mtu akikusemesha mara 2 hadi 3 mtu anaekufahamu anaweza kuitikia kwa niaba yako kwa kusema una tatizo la kutokusikia vizuri

Nilikua nasambaza gesi majumbani nikakutana na visa viwili vya aina hii, sasa kwakuwa mimi ni mtu wa kusalimia kila mtu nikishaingia getini alafu mwenye matani mengi nilijifunza kwamba mtu ambae hasikii vizuri ukimsemesha mara 2 asipoitikia unaona ni dharau kumbe sivyo ndio maana nikasema mtu anaejua tatizo lako akiwepo karibu lazima atamjibu yule anaekusemesha ili kuondoa sintofaham.
 
Uzi ufungwe Kwa hii comment
 
Je akifanya hivo nikiwa na maongezi tumefika mbali. Mimi na muulizaji utatafsirije?

Anawakuta tu akitokea tu anaanza.huyu tusemeje?
 
Kabisa mkuu. Kama umetokea familia duni ukiwa na changamoto hiyo mateso
 
Samehe tu mkuu na usiwazingatie kama hao wakukupa stress zaidi ignore
 
Hata mimi Nina tatizo la kusikia na nimepitia mengi
Mimi pia. Hata simu sipokei labda SMS ukipiga simu naiangalia weeee mpaka inakata.
Lakini ukituma SMS ndani ya sekunde nimeshaijibu.
Kuna kazi zingine nakosa sababu ya tatizo hili la usikivu.
Kuna interview kibao nimefanya ila wakijua tu changamoto yangu basi ndio imetoka hiyo hata kama nimejibu vizuri maswali yangu
 
Je umetumia tiba za Asili sijajua ukubwa wa tatizo lako Ila huwa zipo tiba
 
Nilidhani ni mimi tu...Dah inakele mwanzoni nilikuwa ngumi saiv nawaachia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…