Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
Sawa.maybe hatuzijui.
Huwezi jua tutasaidika.
Nakusubiri
 
Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
Naomba ulizingatie hilo expert wangu,hawa wanahitaji msaada sana

Yan nasoma komenti hapa nasikitika,mtu unaweza kujiona unachangamoto fulani kumbe wenzio ni kubwa zaidi

Poleni sana ndugu zangu,maana binafsi nilipata tu changamoto ya sikio la kushoto kutosikia vizur kutokana na kutumia zile stiki kutoa uchafu,kumbe nikawa nasokomeza uchafu ndani,kutokana na maji basi ukaganda na kusikia ikawa shida

Mtu akiwa anaongea upande wa sikio la kushoto ambapo nilipata changamoto ilikuwa mpaka nigeuke sikio la kulia,simu nayo nilizoe kushoto ikabidi nitumie upande wa kulia

Kuzungumza ikawa shida katika kubalance sauti,sometime naongea sauti kubwa,lkn nilienda hosp wakaniflash na maji ya moto kwa kutumia bomba la sindano,ofkozi hakuwa doktori special wa sikio ila allijiongeza tu

Kweli ukatoka uchafu mwingi,baada ya hapo nikiwa na usikivu mzuri wa awali,sasa hv hunikuti natumia vijiti vya pamba ng'o

Sasa mm hiyo ni changamoto ya mda tu,nyie wenzangu ndio mtihani sana
 
Salaam,

Imenibidi niulize Kwa maana Hali Halisi niionavyo na nikiwa kama mhanga mmojawapo inanifkirisha sana. Nasema hivi sababu Kuna baadhi ya watu jinsi wanavyotendea wenye matatizo ya usikivu ni kama kuwafanya vituko. Hugeuza tatizo lao kuwa utambulisho badala ya kumsaidia.unakuta uko eneo lenye mkusanyiko anakufata mtu "choo Kiko wapi"?.. wakati unatarajia kumjibu anakuja au anadakia mtu "haskii vizuri"

Kwa Namna hii inakuwa anamnuong'onyeza yule mwenye tatizo badala ya kumsaidia. Hawa watu wako beneti mda wote attention kuhakikisha hakuna anaekuongeasha.hata salamu. Na hawa ndo wale wakishajua husikii vema basi hata salamu hakupi,anakupita kama sanamu hata ukimsalimia "habari yako" hakujibu. Mwingine unakuta ni Mzee kabisa,unatarajia atakuwa tofauti na labda sababu ya ukomavu kiakili lakini nae eti unamsalimia hajibu.nabaki naduwaa!.

Kuna wakati najiuliza matatizo ya sikio ndio makubwa kuliko yote,mbona mtu haoni vizuri anavaa miwani hafanyiwi hivi? Kuna watu bila miwani hawawezi hata kutembea barabarani,kusoma hawawezi kabisa,why hawapitii masaibu kama wenye usikivu hafifu?

Basi angalau iwe Kwa watu Baki,tunayapitia pia na Kwa tunaowaona wapendwa na ndugu zetu.maumivu yake sio madogo. Achana na ndugu na wapendwa Kuna nyumba ya ibada.nliwahi fanyiwa jambo nkajikuta nachukia kuingia nyumba ya ibada. Kwenye maofisi hasa ya umma Hadi tunaogopa.maana kama wenye masikio Yao tu wanakiona Cha moto vipi wewe mwenye masikio mazito🤣

Lakini pamoja na kukutana nawatu wenye kutibua hisia na maumivu,bado Kuna watu wema hata mie nakutana nao,ni watu waelewa,wako friendly hawajali kabisa ukiwa open unafurahia wanakusahaulisha hata shida zako..Mwenyezi Mungu awatunze sana!

Nb:Abigail ni muhanga wa Hilo tatizo na nilijua nko mwenyewe ama tuko wachache lakini nilivyojiunga kwenye jamii za wenye Hilo tatizo ndipo nkajua tupo wengi sana,asilimia kubwa ni vijana.japo vyanzo vya shida vinafanana na wengine havifanani,katika kushea changamoto wanazopitia nikaobserve mengi mojawapo ni Hilo.
Pole sana mkuu. Kwangu mimi nadhani ni tatizo dogo ila watu sijui ni kwa nini wanafanya hivyo. Umewahi kujaribu kutumia hearing aid?
 
Dawa za asili zipo usiwe mbishi Kwa kila kitu Mimi mzee wangu alikuwa hasikii .

Ila kuna Dawa alitumia akapona .

Nipo Bukoba Ila nikifika DSM Kwa mzee nitamuuliza hiyo Dawa.

Dawa zipo na zinatibu
mkuu tatizo la usikivu wa mzee wako ulikuwa kiwango gani..maana matatizo ya usikivu yana tofutiana kiwango kuna ambao hawasikii kabisa,kuna wanaosikia kwa mbaali sana na kuna wale wanasikia sauti tu iwe mtu anaongea au awe anaongea kwenye spika au redio atasikia vizuri tu lakini hatoelewa maneno gani yametamkwa yaani kwake anasikia kama zogo tu hapati tafsiri ya maneno yanaongelewa zaidi ya sauti tupu..ukitaja hio dawa ya asili utakuwa umesaidia wengi kwani tuna ndugu wana hii shida
 
Mzee wangu alikuwa anasikia Kwa mbali ili msikilizane inabidi utumie sauti kubwa Sana na umsogelee masikioni .
 
Naomba ulizingatie hilo expert wangu,hawa wanahitaji msaada sana

Yan nasoma komenti hapa nasikitika,mtu unaweza kujiona unachangamoto fulani kumbe wenzio ni kubwa zaidi

Poleni sana ndugu zangu,maana binafsi nilipata tu changamoto ya sikio la kushoto kutosikia vizur kutokana na kutumia zile stiki kutoa uchafu,kumbe nikawa nasokomeza uchafu ndani,kutokana na maji basi ukaganda na kusikia ikawa shida

Mtu akiwa anaongea upande wa sikio la kushoto ambapo nilipata changamoto ilikuwa mpaka nigeuke sikio la kulia,simu nayo nilizoe kushoto ikabidi nitumie upande wa kulia

Kuzungumza ikawa shida katika kubalance sauti,sometime naongea sauti kubwa,lkn nilienda hosp wakaniflash na maji ya moto kwa kutumia bomba la sindano,ofkozi hakuwa doktori special wa sikio ila allijiongeza tu

Kweli ukatoka uchafu mwingi,baada ya hapo nikiwa na usikivu mzuri wa awali,sasa hv hunikuti natumia vijiti vya pamba ng'o

Sasa mm hiyo ni changamoto ya mda tu,nyie wenzangu ndio mtihani sana
Hakika nami nilipitia hali hii kwa masaa kadhaa ila nilihisi upweke mkubwa , nikawaza siku yangu kazini itaenda vipi ila baadae hali ikakaa sawa, japo mpka sasa hali uachafu kwenye masikio inanipa tabu kwani huwa hautoki hvyo kuna kipindi sikio linawasha sana ila mpka ule uchafu utoke inakua kipindi kigumu na ukitoka unakua umekauka kabisa
Poleni ndugu zangu wenye shida hii
 
Pole sana,sasa ikiwa bado unakusumbua fanya mpango siku moja uwatembelee wataalamu wa sikio,ili kama kuna mabaki baki wayaondoe kabisa

Huwezi jua kiasi kidogo kinachobaki huenda kinachangia tatizo kujirudia mara kwa mara
 
Naaam nimeelekezwa hospital ya Ekenywa Magomeni ndo nataka kwenda maana hali hii ya kuwasha kwa sikio ikinipata nakua kama chizi
 
Ni kweli ila jamii inalikuza

Nimewahi ila nkawa naambulia maumivu
Je, zilikusaidia? Yaani ulisikia vizuri ila ukakatishw tamaa na maumivu? Ulinunua brand nzuri au ulinunua za bei rahisi zisizo na viwango? Huwa wanasema ni kawaida kuwa uncomfortable kwa siku za mwanzoni na baada ya muda utazizoea.
 
Mzee wangu alikuwa anasikia Kwa mbali ili msikilizane inabidi utumie sauti kubwa Sana na umsogelee masikioni .
poa, na vp wale wanaosikia sauti vizuri tu lakini hawaelewi ni maneno gani muongeaji ameyatamka je,hawana dawa au ndio tuamini wenye shida ya wanasikia sauti tupu bila tafsiri ya maneno yatamkwayo kuwa tatizo hilo haliponi na halina dawa.?
 
Je, zilikusaidia? Yaani ulisikia vizuri ila ukakatishw tamaa na maumivu? Ulinunua brand nzuri au ulinunua za bei rahisi zisizo na viwango? Huwa wanasema ni kawaida kuwa uncomfortable kwa siku za mwanzoni na baada ya muda utazizoea.
Nlipata za kiwango Cha kawaida,baadae nkapata za bei ya juu.but ndio hivo zinasaidia ila ukivua Sasa usiku maumivu Hadi kwenye ubongo
 
Je, zilikusaidia? Yaani ulisikia vizuri ila ukakatishw tamaa na maumivu? Ulinunua brand nzuri au ulinunua za bei rahisi zisizo na viwango? Huwa wanasema ni kawaida kuwa uncomfortable kwa siku za mwanzoni na baada ya muda utazizoea.
Mkuu hiki kifaa kazi yake ni kukusanya mawimbi ya sauti na kuyaelekeza ndani ya sikio, sasa kwa mtu ambaye anashindwa kuelewa kinachozungumzwa hata kwa sauti kubwa kitamsaidia vipi?.
 
poa, na vp wale wanaosikia sauti vizuri tu lakini hawaelewi ni maneno gani muongeaji ameyatamka je,hawana dawa au ndio tuamini wenye shida ya wanasikia sauti tupu bila tafsiri ya maneno yatamkwayo kuwa tatizo hilo haliponi na halina dawa.?
Mkuu matatizo mengi yana Dawa iwe za asili au kisasa

Mimi nilikuwa naumwa sana kichwa wanaita kipanda uso Ila kuna Dawa nilitumia na nikapona kabisa ilikuwa ya asili.

Kuhusu swali lako ninachojua Dawa zipo mkuu.

Za asili zipo .

Mimi mzee wangu ana 68 yrs tatizo lilmpata akiwa na 63 yrs Ila alipona na sasa imepita miaka mitano yupo vizuri tu.

Kama nilovyosema nikifika DSM kupitia huu Uzi nitapiga Picha Dawa hiyo ya Asili na kutoa mchanganyiko wake ili watu wajaribu kutumia.
 
Back
Top Bottom