Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Hivi tatizo la kutosikia vizuri ni tatizo kubwa zaidi duniani?

Mimi huwa naona njia nzuri na bora ya kushinda hali Kama yako.

Kuwa na circles ya watu wanaojua shida yako and hang out with them.

Maana huku Africa Tanzania hatukuandaliwa Kama watu ambao tunaweza Kuvaa viatu vya mtu.


Nimewahi kuona mama mtu mzima na nilikuwa namuheshimu Sana Ila alikuwa akimuita Dada ninayekaa nae mtaani Kiziwi alikuwa hasikii vizuri so that was bullshit Ever.
Tutafanyaje mkuu...Kuna mda inabidi kuzingatia idadi ya watu wa karibu na kupungiza mazoea. Nao.
Mi natamani kuhama mtaa nnaoishi ila ndo hivo
 
Mimi nilihudhuria clinic Muhimbili ENT miezi 3 nikitumia dawa huku wakiendelea kuniangalia,na aliyekuwa daktari wangu ni specialist wa ENT,baada ya miezi 3 wakasema solution ni mbili,ufanyiwe operation ambayo ni very risk,unaweza kupona au ukabaki na kilema,au utumie hearing aids,akasema sikushauri ufanye operation,kwahiyo nikaandikiwa hearing aids na nikaanza kuzitumia,zinasaidia kwa kiwango flani lakini sio kama zinakurudishia usikivu wa sikio la kawaida...
Pole sana mkuu, kuna rafiki yangu mmoja wa kimahusiano alikuwa na changamoto kama hiyo miaka 7 imepita, nikatafuta hospitali yenye huduma hiyo kwa mtandao, nikapata hapo Arusha, lakini huyo dokta hajaajiriwa ila kutokana na utaalamu wake alikuwa anatumiwa na hospitali nyingi, kwa hiyo kumpata kwake mpaka mpeane 'appointment' kupitia hospitali husika.

Nilivyomtuma mgonjwa kuonana naye siku husika; alimulikwa tu na zile tochi zao; mpaka leo tatizo la kuumwa au kutokusikia kwake limeisha.

Haya matatizo ambayo ni 'technical' ni vizuri kujaribu kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwa sababu ujuzi huwa wanatofautiana.​
 
Yess naijua.
Basi ndio chanzo Cha Hilo tatizo Kwa asilimia kubwa.wengi wanadungwa ama wanawekewa kwenye drip kuwaokoa malaria ikigoma kupona.sasa side effects zake mojawapo ni masikio.
Watu wengi Sanaa walikufa ka malaria ila wengine ikwaokoa..ukioverdose ndo matokeo huwa hivo
Hata Sasa yapo madawa yanatobu na kuharibu masikio,ama Figo nk
 
Kukosa kutosikia ni ulemavu na tatizo kubwa Sana .


Hili tatizo ni kumuomba Mungu usilipate maana ukiwa unatoka broke family na haupo vizuri litakukosesha fursa nyingi na Kuonekana haufai.

Nilichogundua mawasoliano yabeba sehemu kubwa ya mafanikio ya MTU .
Kuna interview moja niliingia, nilipojitambulisha tu kuwa ninashida kiasi ya usikivu, hivyo kwa maswaali ambayo itakuwa sijayasikia wanaweza kuniandikia kwenye karatasi. panelist wakastop kuniuliza maswali badala yake wakaniomba mimi ndio niwaulize wao maswali dah..
 
Basi ndio chanzo Cha Hilo tatizo Kwa asilimia kubwa.wengi wanadungwa ama wanawekewa kwenye drip kuwaokoa malaria ikigoma kupona.sasa side effects zake mojawapo ni masikio.
Watu wengi Sanaa walikufa ka malaria ila wengine ikwaokoa..ukioverdose ndo matokeo huwa hivo
Hata Sasa yapo madawa yanatobu na kuharibu masikio,ama Figo nk
Aiseee ni hatariiii.
 
Mimi pia nimewahi kupewa hiko kifaa. Mjini kimekuwa ni kama biashara ya kulazimisha kila mwenye tatizo la kusikia kukitumia.
Mimi nachoshukuru nilionana na daktari Mhindi pale Upanga akaichana ukweli;
"Kijana hiki kifaa hata nikikupa hakitokisaidia kabisa maana masikio yako yana matatizo zaidi upande wa mishipa, kwahiyo mshukuru Mungu hata macho yako yanaona unajua kusoma na kuandika."
Mwisho wa kunukuu
 
I cried because I had no Shoes, Until I saw Someone with no Feet...;
"if we all threw our problems in a pile and saw everyone else's, we'd grab ours back".

Just image unamuhadithia hii story yako (sad as it may) Mtu ambaye hasikii kabisa Kiziwi, na Bubu; tena bora huyo mwingine ni kipofu pia hivyo inabidi umandikie kwa kutumia Braille

Nachotaka kusema ni kwamba, ukiwa na mtizamo kama huo hapo juu kwenye sentensi mbili za mwanzo utaishi a fulfilled life...
 
Back
Top Bottom