Kwani mkuu GB 1 wewe huwa unainunua kwa shilingi elfu 11500 au hujui tafiti zimefanyiwa ulaya
Kwahiyo mkuu umeamini kabisa 1GB kwa Tanzania ni wastani wa Tsh. 11,500/-?
Jama jama wastani gb 1 ni 11000/= ivi kuna tz nyingine au ni hii moja
Hamuwezi elewa kilichowekwa hapo mpaka uwe umesoma shule za kweli, sio shule za kata, au uwe ulisoma hesabu vema.
Kilichowekwa hapo ni halisi kabisa.
Sababu,
1. Huo ni wastani (sasa namna yakutafuta wastani kajitafutie mwenyewe.
2. Hizi unazozozipata 1GB kwa 2500, mara mb 500 tsh 700/- ni OFA
Narudia ni tena OFA ndio maana hazidumu, kila siku vifurushi vipya, wiki moja kinakuja kipya.
Ebu tuambieni mnanunuaje internet data zenu kama sio kwenye OFA MAALUMU na YA KWAKO TU. Mara YATOSHA, ikifika mwezi mpya kinapotea. Na ndio maana hizi Ofa zinatifauti kutoka mtu mmoja kwenda mwingine lakini wote wateja wa kampuni moja.
3. Nawapa zoezi nenda moja kwa moja kanunue internet bila kuingia kwenye vifurushi maalumu vya ofa uone bei halisi.
Utakuta 300mb kwa tsh 2000/= masaa 24.
Unabisha?angalia chini hapa
Sasa angalia hapa 70mb tsh 500, 250 mb tsh 1000, kwa saa 24.
Isikuchanganye hiyo tsh 2000 1GB ndani ya hizo mb 700 ni za Facebook na Whatsapp. 300+ zilizobaki ndio zipo huru tena limited within time.
Utafiti hupingwa kwa utafiti. Ni akili ndogo tu ndio huwa zinabishia Mambo makubwa