Hivi TRA watakubali ku register kampuni ikiwa ofisi nataka ziwe nyumbani?

Hivi TRA watakubali ku register kampuni ikiwa ofisi nataka ziwe nyumbani?

Yeah,walinifanyia hivi..ndo maana nikashangaa jamaa anavyosema tofauti,ningeenda kubadili chaap.

TRA sio marafiki aisee.
Watu wengi hawaelewi kwanini wanafanya hivyo, ni hivi kwenye formula yao ya makadirio haina kipengele cha kutofautisha mtu anayefanya biashara kwenye nyumba yake au ya kupanga, inakuhesabia kama umepanga Ili kukupa hesabu sahihi kwasababu ukiruhusu hilo mwingine atakuja anadai kaachiwa nyumba na mjomba wake aitumie bure, utatumia kanuni gani?,ndo maana nimetoa mfano wa kuzawadiwa gari Japan ila likifika bongo wanalilinganisha na Bei za beforward na kwingine Ili ulipe kodi sawa na wengine.
 
Yeah,unaenda na mkataba wa pango tu.,watakata asimilia kulingana na kodi unayolipa
Okay hapo ni sawaa nashukuru sana, hili jambo ndio nilikuwa naona kama linanikwamisha maana mimi sikutaka hizo complication za ulazima wa kuwa na ofisi.

Nlichokuwa nataka ni kuweka compliance ziwe sawa ili niweze fungua account ya kampuni halafu kazi zangu nifanyie mkononi au nyumbani.

Asantee sana
 
Habarini wakuu,

Kama kuna mtu ana uelewa na hichi kitu nitaomba msaada.

Nahitaji ku register kampuni au biashara. Ila kuna mara ya mwisho nilisajili biashara nilivooenda TRA walitaka niwapatie mkataba wa pango la biashara.

Na baada ya kuwapa wakaanza kupiga mahesabu yao ya sijui withholding tax n.k

Ni mda umepita, nataka kusajili kampuni au biashara ila sasa changamoto yangu ni kwamba ofisi ya hiyi biashara au kampuni nataka iwe nyumbani kwangu kulingana na nature ya shughuli nazotaka fanya.

Sasa naulizia itakuwa ni proper kama wasema nilete mkataba basi nikapeleka huo mkataba wa upangishaji wa nyumba?

Ntaomba ushauri kwa hilo kwa sababu ndo kitu kinanikwamisha.

Asanteeni sanaa
Hakuna shida ila watakuomba mkataba wa upangaji wa nyumba ya ofisi hiyo ili wakate witholding tax !! Hata kama nyunba ni yako mkataba huu wa kupanga ni lazima.
 
hivi ni hii dalasa la saba yangu ndo sielewi au? hv kwann wanakadiria mtu kodi? sio kwamba ni miyeyusho hii? kwann isiwe FDA risiti akawa nayo kila mtu ili wapate chao. Au ni ngumu kwa necha ya wabongo?
Daah hii ni mojawapo ya mambo wengi hatuelewi, ila ndo hivo sasa itabidi tu comply kama mtu unataka kufanya biashara nchi hii..

Maana hapo ukifungua biashara mara ya mwisho ilinibidi kufanyiwa makario ya kulipa kodo kabla hata biashara haijaanza
 
Hakuna shida ila watakuomba mkataba wa upangaji wa nyumba ya ofisi hiyo ili wakate witholding tax !! Hata kama nyunba ni yako mkataba huu wa kupanga ni lazima.
Kwa case yangu mimi hii nayokaa ni nyumbaa ya kupanga na ningetaka nifanye pia kama ofisi
 
hivi ni hii dalasa la saba yangu ndo sielewi au? hv kwann wanakadiria mtu kodi? sio kwamba ni miyeyusho hii? kwann isiwe FDA risiti akawa nayo kila mtu ili wapate chao. Au ni ngumu kwa necha ya wabongo?
Kwanza ni ngumu kwa nature ya wabongo, pili sio kila mfanya biashara ana qualify kuwa na machine ya efd ndo maana lazima uende wakupigie hesabu Ili wajue upo kundi gani kuanzia mtaji, kodi ya jengo, makadirio yako ya mapato kwa siku,wiki,mwezi hadi mwaka.

Kuna watu wanalipa chini ya laki moja kwa mwaka mzima kutegemea na walivyojieleza na wanaandikiwa Tax Clearance kila mwaka kuwa hawadaiwi. Inategemea nature ya biashara yako,mzunguko n.k. Ingawa kwa ufanisi zaidi ilibidi efd imalize kelele zote hizi.
 
Hilo sio tatizo , unachotakiwa kufanya ni kuangalia nyumba kama yako eneo ulilopo ungekuwa unapanga ungelipa kiasi gani!?,hakuna Sheria inayozuia nyumba yako kuwa ofisi ila lazima wajue thamani ya kupanga nyumba kama hiyo mitaa hiyo, ikibidi jiandikie mkataba kwamba wewe mwenyewe unailipia nyumba yako labda laki 3 Kwa mwezi, umuhimu wake ni kwenye makadirio ya kodi kwa mwaka kulingana na biashara unayoifanya. Mfano mzuri ni kwa mfano upewe zawadi ya gari Japan, China au U.k uilete bongo, kwenye kikokotoo cha T.R.A hakuna formula ya gari la kuzawadiwa. Watalipigia hesabu thamani yake huko lilikotoka na utalipia sawa na mwingine aliyelinunua huko.
N.B. Jitahidi kila utakachokiandika ukishusha thamani, weka gharama za chini itakusaidia wakuweke kundi gani la kodi. Ukijichanganya waweza kukadiriwa kodi sawa na Mo Dewji kwa mwaka. T.R.A sio watu wazuri kabisa.
Pia asisahau kubeba mfuko wa kaki
 
Kwanza ni ngumu kwa nature ya wabongo, pili sio kila mfanya biashara ana qualify kuwa na machine ya efd ndo maana lazima uende wakupigie hesabu Ili wajue upo kundi gani kuanzia mtaji, kodi ya jengo, makadirio yako ya mapato kwa siku,wiki,mwezi hadi mwaka. Kuna watu wanalipa chini ya laki moja kwa mwaka mzima kutegemea na walivyojieleza na wanaandikiwa Tax Clearance kila mwaka kuwa hawadaiwi. Inategemea nature ya biashara yako,mzunguko n.k. Ingawa kwa ufanisi zaidi ilibidi efd imalize kelele zote hizi.
da nimejiona kumbe na mm nna akili licha ya la saba yangu kwamba naweza kufikiria.asante sana mkubwa kwa maelezo haya.
 
Mkuu mimi nina jingo lango ndo ofisi,ila wamegoma wameomba niandike makadirio ningekuwa nalipa kiasi gani,so wanakata hapo
Wameona hijui haki zako. Jengo lako ulipe kodi? Ni sawa na kulazimisha mwenye kampuni awe analipwa mshahara ili serikali ikate payeee, sio lazima ila ukikubaliana nao inakula kwako. Kumbuka hao nyimbu huwaza kukusanya kodi tu hata kama utakufa njaa wao hawajali. Wewe onyesha ru umiliki wa hilo jengo kama hawataki nenda kwa bosi wao.
 
Nimefanya kama hivyo nyumba ni binafsi ila nimeandika mkataba wa kupanga kilazima ili nikatwe kodi
Watanzania juweni haki zenu jamani mtaibiwa hadi damu. Nyumba yako unaanzaje kupanga na kulipa kodi? Anyway ushaingia mkenge.
 
Asante sana mkuu ... mimi kwa case yangu bado nipo nyumba ya kupanga na ndo ningetaka kutumia huo mkataba kama address pia ya biashara, i hope hiyo pia inakubalika
Kwa kuwa ni ya kupanga utawalipa kodi ya zuio TRA. Maana hapo ni kama umepanga ofisi tu. Unajua kinachotakiwa ni biashara iwe na anuani inayotambulika. Haya mengine ni ziada tu.
 
Mkuu,Hakuna ambacho hakiwezekani Duniani na wala TRA shida yao sio ofisi.Shida yao ni Kodi yao ulipe kikamilifu.Swali ni Je biashara yako inafaa kufanyika nyumbani?Kama.jibu ni Ndio basi Go ahead
 
Kwa kuwa ni ya kupanga utawalipa kodi ya zuio TRA. Maana hapo ni kama umepanga ofisi tu. Unajua kinachotakiwa ni biashara iwe na anuani inayotambulika. Haya mengine ni ziada tu.
Nimesoma posts zako kuna kitu hapa unachanganya, formula ya T.R.A ya kukukadiria wakuweke kundi gani la kodi kwa mwaka, wanaangalia mtaji wako halisi kutegemea na biashara unayotaka kufanya, unawaambia unategemea kupata faida kiasi gani Kwa siku,mwezi,mwaka halafu ndo annual income yako ambayo ni net profit baada ya kutoa matumizi yote ikiwemo kodi ya nyumba,chumba/frame unayotegemea kufanyia biashara ndo inawaambia wewe upo kundi gani la kodi. Ndo maana kwenye formula yao wamelazimisha mtu aweke kodi ya nyumba/chumba Cha biashara.

Hata kama ni nyumba yako unaandika mkataba wa kupanga wenye thamani na nyumba/chumba kama hicho maeneo hayo.(Ni Kwa faida yako), kwasababu kwa mfano faida yako baada ya kutoa vitu vyote (kasoro kodi ya nyumba)kwa mwaka ni milioni 5. Ungepigiwa hesabu za watu wanaopata faida ya milioni 5 Kwa mwaka, ila kama ungejumlishiwa kodi ya nyumba tuseme laki 1 na nusu Kwa mwezi, sawa na milioni 1 na laki 8 Kwa mwaka, ingetolewa kwenye Ile milioni 5 na kubaki milioni 3 laki 2. Kwahiyo ungepigiwa hesabu za watu wanaopata faida ya milioni 3 laki 2. Ndo maana wanalazimisha ulete mkataba wa kupanga nyumba/chumba ni kwa faida yako.

Tatizo T.R.A hawatoi ufafanuzi wa kutosha kuelewesha watu vizuri. Mtu anahisi kueleza haupangi ofisi ni nyumba yako ni dili kumbe anajipunguzia matumizi faida ionekane kubwa na kodi iongezeke pia, kwa wazoefu hata kama nyumba ni yake anaiandikia mkataba Ili iwe sehemu ya matumizi kodi ipungue. Soma kwa makini maelezo yangu utaelewa. Usipoelewa tafuta mfanyabiashara wa kati mwenye uzoefu wa kukwepa kodi akueleweshe.
 
Nje ya mada wakuu!

Ukikosea kuandika thamani ya mzigo unarekebishaje[emoji848][emoji848]yaan kama ilitakiwa iwe 720k ukaandika 72M
Unawaandikia barua na kutoa maelezo kwa kifupi namna umefanya error kwenye details za pesa.
 
Back
Top Bottom