Nimesoma posts zako kuna kitu hapa unachanganya, formula ya T.R.A ya kukukadiria wakuweke kundi gani la kodi kwa mwaka, wanaangalia mtaji wako halisi kutegemea na biashara unayotaka kufanya, unawaambia unategemea kupata faida kiasi gani Kwa siku,mwezi,mwaka halafu ndo annual income yako ambayo ni net profit baada ya kutoa matumizi yote ikiwemo kodi ya nyumba,chumba/frame unayotegemea kufanyia biashara ndo inawaambia wewe upo kundi gani la kodi. Ndo maana kwenye formula yao wamelazimisha mtu aweke kodi ya nyumba/chumba Cha biashara.
Hata kama ni nyumba yako unaandika mkataba wa kupanga wenye thamani na nyumba/chumba kama hicho maeneo hayo.(Ni Kwa faida yako), kwasababu kwa mfano faida yako baada ya kutoa vitu vyote (kasoro kodi ya nyumba)kwa mwaka ni milioni 5. Ungepigiwa hesabu za watu wanaopata faida ya milioni 5 Kwa mwaka, ila kama ungejumlishiwa kodi ya nyumba tuseme laki 1 na nusu Kwa mwezi, sawa na milioni 1 na laki 8 Kwa mwaka, ingetolewa kwenye Ile milioni 5 na kubaki milioni 3 laki 2. Kwahiyo ungepigiwa hesabu za watu wanaopata faida ya milioni 3 laki 2. Ndo maana wanalazimisha ulete mkataba wa kupanga nyumba/chumba ni kwa faida yako.
Tatizo T.R.A hawatoi ufafanuzi wa kutosha kuelewesha watu vizuri. Mtu anahisi kueleza haupangi ofisi ni nyumba yako ni dili kumbe anajipunguzia matumizi faida ionekane kubwa na kodi iongezeke pia, kwa wazoefu hata kama nyumba ni yake anaiandikia mkataba Ili iwe sehemu ya matumizi kodi ipungue. Soma kwa makini maelezo yangu utaelewa. Usipoelewa tafuta mfanyabiashara wa kati mwenye uzoefu wa kukwepa kodi akueleweshe.