Hivi TRA watakubali ku register kampuni ikiwa ofisi nataka ziwe nyumbani?

Zawadi huwa hailipiwi kodi nenda popote duniani. Ni hawa wakuda wa TRA ndio wanaforce watu kulipia kodi mali ya zawadi.

Inatakiwa ukipewa zawadi ya gari au gari ambayo umenunua kwa matumizi binafsi na sio kuuza zisiwe taxed kama hivi tunavyolipishwa. Gari ya kununua ina kodi yake ambayo ni ndogo sana. Haifiki hata 10% ya bei ya gari. Wanaotakiwa lipa kodi ni wale wamiliki wa yards za magari.
 
Ulichosema ni kweli kabisa.
 
Umeeleza vizuri sana, na hii ni moja ya trick ya ukwepaji kodi kisheria.

Na kwenye huo mkataba hakikisha umeweka kodi kubwa kubwa.
 
Watanzania juweni haki zenu jamani mtaibiwa hadi damu. Nyumba yako unaanzaje kupanga na kulipa kodi? Anyway ushaingia mkenge.
Bro wewe ni mlipa kodi? Haki kwenye sheria za kodi? Mgogoro wa juzi kati hapo kariakoo hadi wafanyabiashara wakafunga maduka unadhani hawajui haki zao? Ungekua unafahamu jinsi sheria za kodi zinavyo ji contradict usingekuja hapa kusema hivyo!
Mlolongo wa kuifanya nyumba yako itambulike kama ofisi bila kulipa kodi ya pango ni mrefu sana ndo maana kwa mahesabu rahisi tunakubali tu kuandika mkataba.
Mfano threshold ya kusajiliwa Vat ni mzunguko wa milioni 100 kwa mwaka , lakini siku mapato yakipungua milion 100 kwa mwaka hao hao Tra hawana uwezo wa kukutoa Vat.
 
Hawakubali kwa wasiojielewa. Biashara ni yako na nyumba ni yako wewe ndio mwenye maamuzi ulipe kodi au ujipatie nyumba bure. TRA hawana mamlaka ya kukulazimisha ulipe kodi kwenye nyumba yako.
Wewe unayejielewa unafanya biashara ipi ?
Maelezo mazuri ila naomba nitofautiane kidogo nawe kwenye hiyo kodi ya pango! ni kweli inakufanya uonekane na matumizi ya ziada ukiwa kama mpangaji lakini huko mbele utabanwa na witholding tax ukiwa kama mpangishaji.
Its a chain reaction
 
Mkuu ridia kunisoma vizuri, hakuna mkwepa kodi mzoefu atasema hiki chumba/nyumba/ jumba ninapofanyia biashara ni la kwangu. Anajua inamuharibia hesabu. Wadau hapo juu wanaongea vitu hawavijui na nahisi sio wafanyabiashara.
N.B. 99.9% ya watanzania nikiwemo mimi na wewe ni wakwepa kodi(tunalipa ya kuzugia).
 
Mkuu nina taarifa za huko duniani kuhusu zawadi. Naongelea kwa hapa Tanzania hakuna kitu kama hicho. Ukizawadiwa gari ukaja nalo bongo kodi iko palepale. Mojawapo ni kuwa wabongo janjajanja nyingi. Ilikuwepo ikaondolewa Kwa wanaotoka masomoni. Wabongo walianza kila akija likizo baada ya muda fulani anadai kazawadiwa gari anapunguziwa kodi, wakaona isiwe tabu.
 
Sheria yao,hata kama jengo ni lako.
Lazima uandike mkataba unalipa kiasi gani kwa mwezi.ili nao wapange hayo maokoto yao ya withholding
Sio Lazma mkuu Kama jengo ni lako unawasilisha hati ya Nyumba au rizi ya eneo husika
 
Nje ya mada wakuu!

Ukikosea kuandika thamani ya mzigo unarekebishaje[emoji848][emoji848]yaan kama ilitakiwa iwe 720k ukaandika 72M
Unaandika barua TRA unaambatanisha na risiti ya manunuzi ya mzigo wenyewe. Na kawa wewe ndio umeuza mzigo ukakosea basi toa risiti nyingine sahihi mda huohuo, zihifandi zote mda wa return utaambatanisha katika ADJUSTMENT FILING kuondoa hiyo kasoro.
 
Yes inawezekana
 
Unaandika barua TRA unaambatanisha na risiti ya manunuzi ya mzigo wenyewe. Na kawa wewe ndio umeuza mzigo ukakosea basi toa risiti nyingine sahihi mda huohuo, zihifandi zote mda wa return utaambatanisha katika ADJUSTMENT FILING kuondoa hiyo kasoro.
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hata risiti ya luku anaweza ambatanisha mimi nimefanya ivyo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…