Uchaguzi 2020 Hivi Tundu Lissu akishindwa mtafanya nini?

Lissu ameshindwa kiuhalali ndo mana kasepa mapema , Lissu kwenye sanduku kapigwa kabisa hakuna haja ya kusingizia kaibiwa kura , kuna wabunge wa upinzani wamefanyiwa figisu , japo nasikia mbowe naye kapigwa kiuhalali , ila Kwa Lissu ni total defeat....
Labda kama tunatengeneza kichaka cha kujifichia hapo sawaaa
 
Kuna watu waliongea kama majasiri kumbe ni wale wale tu keyboard warriors
 
halafu akawahimiza watu waingie barabarani alipoona wamempuuza akakimbilia ubalozini eti kuna mtu anamtishia nani ?kwalipi mpaka wamtishe yeye ni nani hala lolote mwishowake kaamua kuwakimbia na mngeingia barabarani mngepigwa mvunjwe miguu halafu mwenzenu anaondoka anawaacha na majeruhi
 
Lissu alidhani ile hali ya kuzungumza na Balozi wa USA wakati ule akadhani wanamkubali. Hawa ni wana diplomasia na wanajua na kufahamu namna ya kudeal na watu kama akina Lissu. Kuongea naye wakati ule akadhani wako tayari kumkaribisha; alipokimbilia huko, ubalozi wa US wakamtolea nje, akaanza kuhaha ndipo akaishia huko alikoishia na hatimaye kuikimbia nchi. Halafu hili suala la kutishwa! Hivi katishiwa Maisha na nani? Kwa nini asilipoti Polisi au kwenye vyombo vingine vya usalama?Ingawa yeye, Lissu, anase,a haviamini! Hawa watu ni WAOGA SANA, wanapigiwa simu au kutumiwa ujumbe na "matapeli na waigizaji wenzao" wanaanza kukimbia nchi! Hii ni ajbau na kweli!
 
Wewe Mkaruka Mzee yawezekana kichwa chako ni kama mfuko wa kubebea meno tu. Sidhani kama akili yako inabidi ya mende.

Yaani nimemchukukia Lissu kirahisi namna hiyo. Yaani uhuni wa NEC na TISS na Polisi hujauona wakati wakizuia mawakala wa UPINZANI?
Haya waliitisha maandamano; Je hujui kuwa viongozi wao walikamatwa usiku wa kuamkia maandamano?

Ulitaka wafanya nini wao baada ya kuwa rumande?

Ni kweli hakukuwa na uchaguzi na Watanzania wameridhika kuongozwa KIIMLA na DIKTETA wa CHATO. Sasa Lissu awasaidieje kama hamuwezi kukusaidia.

Ujinga huu uko Tanzania tu, hapo Malawi asingetgubutu
 
Hayo ni mawazo yangu. Unaonaje hiyo sentensi yako ya kwanza hapo juu = NIKURUDISHIE WEWE "yaani kichwa chako ni kama mfuko wa kubebea meno tu ……". Wacha maneno ya kulinganisha nchi na nchi, huo ni utoto kwenye suala la policy analysis. Utoto tena wa chini sana! Zungumzia TZ yetu na ujenge hoja! Haya usemayo ni rhetorics za Lissu ambazo sasa unazileta wewe. Lete ushahidi, vinginevyo, wakifanya fujo watakutana na nguvu za dola, no more no less. Lissu knows this ndiyo maana KASEPA!
 
Usimjibu mpumbavu sawa na upambavu wake usije kuwa sawa naye.. (Mithali 26:4)
 
Hongera sana kumbe uliwahi kuyafikiria haya mapema na kutoa ushauri. Upinzani sasa hivi wako kukimbilia nje tu; Lissu keshahamia Ubelgiji a,bako alikuwa na apartment na alivyokuja kwenya uchaguzi bado lease ya apartment ilikuwa active, kwa maana ya kuwa alikuwa anajua atarudi; Lema naye yuko Kenya lakini anataka kwenda huko nchi za ng'ambo, Zito naye ameanza kutafuta sababu za kuhamia ujerumani.

Kitu cha muhimu ninatangaza hapa kuwa mimi nitatumia mbinu zote ninazoweza kuhakikisha serikali ya Biden haingilii kabisa siasa za ndani ya Tanzania. Nilishakutana na timu yake mara kadhaa kwenye shughuli zao uchaguzi na nitajitahidi kuwatumia kuhakikisha kuwa wanaiacha Tanzania bila madhara ya wanasiasa uchwara hawa; yaani wao wakishinda wanakubali matokea, ila wakishindwa wanalalamika. Sasa hivi timu ya Biden inajua tatizo hilo vizuri sasa na najua watanielewa. Stay tuned.
 
Mtaanza lini kukinukisha? Ahahahahahah!
Hahhaah. Yaani kabisa ulikaa kutegemea wabongo wakinukishe kisa Halima Mdee kakosa ubunge?

Wabongo mikwala mingiii.
Wewe ukitaka tukinukishe maisha yawe magumu. Bado maisha sio magumu. Ugali upo bado. Life likiwa gumu unga hakuna njaa siku tatu hata wewe sweet kidume unayetumia jina la kike utaingiza makalio bara barani tu. Kama moroko
 
Majibu nafikiri umeyapata sasa...watu wamekuwa wakulalamika tuu kila siku, uchaguzi ulishaisha sasa hivi mjipange kwa uchaguzi ujao
 
Ila humu JF mshakinukisha sio? Ahahahahahahah! Nasikia Lissu akihojiwa VOA amewaponda sana kwa kumsifia na kumpamba sana kwenye mikutano yake na mtandaoni lakini alipowaambia muandamane akaishia yeye kukimbilia Ubeleji amesindikizwa na mabalozi wa nchi zingine badala ya ninyi! Ahahahahahh!

Halafu, ndio, mimi ni sweettablet na ni MWANAUME tena MWANAUME BAROBARO, Ila sifanyi mambo ya Lissu na Amsterdam! Ahahahahahahah!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…