Hivi tutawapoteza watu wetu wa karibu mpaka lini kisa Pesa.!?

Kuna jamaa nilimkopesha pesa ila kwenye kulipa akawa analeta danadana, nilimuandikia meseji nzito mpaka akaona aibu ingawa kwenye kunilipa alinilipa nusunusu

Kiukweli jamaa sina maelewano mazuri nayeye mpaka hivi leo ingawa salam tunapeana

Mkuu hiyo msg kama bado unayo na mie nitumie kuna msengerema ananizungusha sana
 
Kuna ex wangu wangu

Eti ameninunia Lisa sijamchangia mchango wa harusi take

Chakushangaza yy hakufanya send off,ila alitaka nimchangie kwenye harusi ambayo mm haiijihusu

Jua bado nakupenda Maria but hukunifanyia fair
 
Funguka zaidi Carleen ili tuchangie kwa kina. Unaongelea Ndugu, jamaa rafiki au BF!?
 
Ww kama mm tena ni mlokole mwenye cheo chake kanisani alikua mtumishi sikuamini nmelamba block kila kona
Utapeli na udhulumaji hauna dini wala kabila aisee,huyu ni wakumwendea tu kwa mchungaji wake labda litaona aibu likiitwa na wazee wa kanisa lake ikishindikana unamshtakia tu Mungu.
 
Pole sana Carleen....

Uzi wako umenifanya nimkumbuke rafiki yangu mmoja..kipindi fulani cha maisha yetu tuliwahi kuishi pamoja na kuwa karibu sana..Tulikuwa ni kama ndugu wa tumbo moja ingawa tulikutana ukubwani katika harakati za maisha..nikiugua ananitibia, akiugua namtibia pia, hayo ndio yalikuwa maisha yetu ya upendo ..Kwa zaidi ya miaka 2 tuliyoishi pamoja, HAKUWAHI KUNIFANYIA KITU KIBAYA/ROHO MBAYA na wala sikuwahi kumfanyia ubaya...Hatukuwahi hata kugombana ile seriously ukiacha some quarrels which are normal in life....

Kipindi fulani alipata shida moja kubwa sana ambayo ilikuwa inaweka hatarini future yake..Hakuwa na tegemeo jingine zaidi ya mimi ndugu yake..Hata wazazi wake wasingekubali kumsaidia ndio maana hakutaka kuwashirikisha..Namimi isingekuwa rahisi kumkimbia ndugu yangu niliyeishi nae vizuri sana kisa changamoto aliyoipata..nikapiga moyo konde, nikasema wewe ni ndugu yangu tunasolve hii inshu..Inshu yenyewe ilihusisha pesa, alikuwa na inshu moja kubwa sana na ya muhimu ambayo alitakiwa kuisolve kwa pesa...Akanifata akanambia, FOHADI naomba unikopeshe kiasi XXXXXXX haitapita miezi miwili nitakupa....Sikuwa na hofu, wala sikuwaza kama nitaipoteza ile pesa kwa jinsi tulivyokuwa...Nilizama mfukoni nikamkopesha ndugu yangu nikiamini kuwa nailinda future yake...Nikweli, alisolve inshu yake na mambo yake yakawa byeee kabisa...nilikuwa na furaha kumuona ndugu yangu amekuwa na amani...Baada ya muda akapata kazi Musoma, ikabidi aniage akaondoka huku akiniahidi kuwa ndani ya miezi 2 pesa yangu itakuwa imerudi...

Kilichofata baada ya hapo ni maumivu kwangu..Niliumia sana kupoteza kiasi kikubwa tena kwa mtu ambae sikumtarajia na mbaya zaidi mtu aliyekuwa na uwezo wa kunilipa ile hela...Simu zangu zilikuwa hazipokelewi, msg hazijibiwi na sikuambulia kitu..Ni miaka mingi imepita, hadi leo sijaambulia kitu chochote, Nimesamehe, nishasahau...Ila urafiki mimi nayeye tena ni FUTURE IMPOSSIBLE TENSE...

Pole sana carleen..I know the feeling.
 
Watu kwao Uaminifu ni jambo gumu sana.

Hatuna kabisa utamaduni wa kuheshimu makubaliano au mikataba.

Sometimes, tunalalamika hatuna mitaji lakini ukiangalia tatizo kubwa linaanza kukosa uaminifu.
 
Pesa ni shetani aliye tengenezwa na binadamu..
 
Ukitaka kuweka amani na kila mtu basi usiweke matarajio makubwa sana kwa watu.
Ukikopeaha kopesha kiroho moja kwamba fanya kama umetoa tu sadaka asiporudisha basi. Vinginevyo utavunjika moyo bure uje ugombane na kila mtu na ni ww ndiye utaonekana mkorofi.
Hii kanuni huwa inanisaidia sana. Nikitoa basi natoa tu. Isiporudi poa tu.
 
Ulikosea sana ndugu yangu na haukufanya vizuri hii kitu imenitokea kwa watu wangu wa karibu wamenifanyia hivi tu hapa majuzi na mm nimetokea sana kuwachukia cha msingi kama ni kusaidia Saidia au kama huwezi bora umwambie mtu mapema kuliko kumwahidi inakuwa siyo vizuri kumbuka malipo ni hapahapa leo wewe unacho yeye hana kesho huna yeye anacho!
 
πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯ngoja nilie kwanza nina mikasa mingi mno nimepoteza pesa nying mno

Namba moja siku moja kuna demu nilikutana nae chuo tukazoeana fresh basi kufika mwaka wa pili kwenda wa tatu yeye alicarry mi nikapita nikamliza yeye akawa bado yuko mwaka wa tatu sasa aliyumba kiuchumi sana baada ya kukaa home kwao mwaka bila ya kusoma wala bum ikumbukwe hapa sijakuwa na mahusiano nae wala na alikuwa mpole tulizoeana kwa vile tulikuwa group moja mwaka wa kwanza na wapili siku moja akaniomba laptop yangu ambayo nilikuwa nataka kuiuza ili niendelea na harakati za kutafuta maisha yeye kwa vile bad yupo chuo mi nishamaliza nikamwazima sasa kumbe walikuwa wanakaribia kufunga chuo tukakubaliana nikapta mteja nakuja chukua laptop yangu yule demu akakaa nayo miezi miwili na likizo alienda nayo sijui kauza au kapoteza


Nimepata mteja kanikana sijampa laptop na nisiendele kumsumbua atanisingizia nimembakaπŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯πŸ˜₯kutokana na kunizushia nimeenda kwa mganga imeniuma sana laptop kama ya laki 4
 
Nyingine rafiki yangu siku moja alinipigia simu oy niko mahali hapa nachukua mzigo wa vitu nimepungukiwa na laki 2 maana yeye ni mfanya biashara nitumie fasta jioni napitia bank nakupa maana bank nipp mbali na bank na mzigo ni fasta na hapa nje ya duka kuna mpesa nikasema ngoha niharakishe nimatumia na ya kutolea

Kumbuka ni baadae means siku iyo iyo atanilipa basi sikuwa na wasi alivyorudi sikumsumbua huwezi amini kanizungusha na mzigo kauza kapata faida mara 2 sijaambulia hata mia miaka 2 sasa ananitumia ma meseji marefu ya kuomba msamaha ilihali anajua ishu ni peda hataki kutoa
 
Shukrani sana kwa somo zuri braity..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…