Asante sana
Carleen na nimejifunza sana..na hapa naungana na
mamylove ila natofautiana nae sehemu ndogo sana..Watu pekee ambao sitaacha kuwakopesha kamwe ni ndugu zangu...hata wasiponilipa sitaumia maana it has always been my desire kufanikiwa na kuwasaidia ndugu zangu kimaisha...I have my young bro yuko chuga..Desemba mwaka jana alibanana nikamkopesha ila hadi leo hajanilipa na siumii na wala huwa sipigi mahesabu kama kuna hela ipo kwake coz that is my responsibility as a big bro to my juniors....
Kuhusu Marafiki ni HAPANA..kuna rafiki angu mwingine nilisoma nae advance, tulivoenda chuo akaja nmkopeshe ada na kweli asingefanyiwa registration...nakumbuka ilikuwa 100k na akasema atanilipa na riba, mimi nikakataa riba ila nikamwambia akipata tu hiyo hela anilipe..na aliahidi within one month maana atapata toka hom...
Sikuona ile hela, badae anakuja ananipa namba ya mama ake niwe namdai..kwani mimi nilimkopesha mama yake?....sawa nikawa naongea na yule mama ananipa ahadi kila siku...Baadae rafk yangu akaja kunambia kuwa eti katika kumdai yule mama yake nilimtukana kwenye msg na ndio maana hataki kunilipa....Nilijisikia vibaya sana, nikamwambia nimemtukana kwa msg, basi nipo tayari twendeni polisi akashitaki..kati ya kitu siwezi kufanya ni kumtukana mama mtu mzima tena mzazi wa rafiki yangu maana hata mm sitapenda kutukaniwa mama yangu...Mwisho wa siku nilipoteza hela na urafiki....
Baada ya mwaka mmoja yule rafiki yangu akaanza kunitafuta tena..kipindi hicho tumemaliza chuo..Mambo yake yakibanan ananicheki nimsaidie hata nauli au hela ya vocha..mwanzoni nikawa na mpa ila mara ya mwisho nilimtumia ilikuwa 2000 tu ya vocha na hapo hapo nikamuuliza, hivi mshikaji, pamoja na kunidhulumu laki moja yangu na kunisingizia nimemtukana mama yako, unapata wapi ujasiri wa kunitafuta na kuniomba tena hela?.....Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kaniomba msaada yule jamaa...
NB: 'unakuta unaemwamini ndiye anakuwekea sumu, hawana alama binadamu wanaokuja kukuhukumu' - DARASA