uchagani spirit ya utafutaji huwa inazoezwa tangu mtu akiwa mtoto mdogo, mfano asilimia kubwa ya watoto wana sungura zao , kuku zao wanazipambania mpka zianze kuzaa matunda , mauzo ya pesa wanazopata wananunulia baadhi ya mahitaji ya shule na zinazobaki zinaendeleza mitaji yao mpka ikuwe , mfano mimi nikiwa msingi niliuza sungura zangu nikanunua baiskei kwa ajili ya kwenda kusagia unga majirani , nilikua natoza mia tano kwa kila kichwa , pesa nilizopata nilizitunza kwenye kibubu , nilipovunja nyingne niliendeleza mradi wa sungura , nanyingne niliongeza nguruwe jike mmoja , nikawa nazipambania na baiskeli yangu nikitoka shule , nasaga mahindi kwa mia 500 nakuchota maji madumu kumi 2000 natunza pesa , kwani nilikua nakula nyumbani , nguo na vingne wazazi wananunua[emoji4] mwisho wa siku nikajikuta na pesa ambazo kwa udogo wangu sikueza kuzicontrol , nikamshirikisha maza , akanishauri tupanue mradi wa ngurue na tununue kuku wa mayai kilacha , vifaranga mia tutunze , namaliza form 4 na pesa nyingi tu , nasubiri matokea kwenda form 5 nikafungua mpesa , tigo pesa na sehemu ya kupika kiti moto , nikapiga biashara mpka matokeo yalivyotoka nikachaguliwa form five pcb same boys nikamwacha mdgo wangu wakike anaefuata aendeleze biashara , ilikua mno , nikiwa likizo nafuatialia ilinisaidia mambo mengi mno kishule , mpka naenda chuo biashara hyo inanibeba , namaliza chuo nipo mazoezi kwa mda wa miaka miwil biashara inakua , nikapata wazo nifungue maabara na phamancy kupitia hyo biashara na sasa nipo apo . hii nikuonyesha misingi huwa inajengwa toka mtoto akiwa mdgo anatakiwa ajue pesa , kuitafuta na jinsi yakuiendeleza , pesa izae pesa na pesa izae pesa na nakuendelea.