Hivi uharamu wa Gongo, Bangi na kitimoto ni nini?

Hivi uharamu wa Gongo, Bangi na kitimoto ni nini?

Tangu nakua mpaka sasa nishazeeka nasikia kuwa Gongo, Bangi na Kitimoto ni haramu. Hivi uharamu wake upo kwenye nini hasa?

GONGO
Uharamu wa Gongo upo kwenye vikorombwezo vinavyotumika kuitengenezea? Kwenye vyombo vinavyotumika kutengenezea ama kunywea? Upo kwenye sehemu inaponywewa au kwa wauzaji wake? Au Uharamu wake upo kwa wanywaji wenyewe?

BANGI
Uharamu wa Bangi ni kwa jinsi inavyolimwa, inavyovunwa, inavyovutwa, maeneo itokako, wavutaji wake au jina lenyewe ndiyo haramu?

KITIMOTO
Huyu mnyama uharamu wake ni kutokana na ngozi yake ilivyoshikana na nyama yake, rangi yake, sauti yake, pua yake, kujaa kwake mafuta, ama tabia yake ya kupenda kujigalagaza kwenye matope?

Hebu tujadiliane jamani!!
Napata nitarudi baadae 🚶
 
Tuanza na Mkuu wa Meza [emoji241] KitiMoto

Huyu ana mnyoo ambao umethibitika kitabu kwamba haufi hata ukiwekwa kwenye nyuzijoto 130 na zaidi yaan hata akiwekwa kwenye lile joto la kuyeyushia chuma hafi na huyo mnyoo chakula chake kikubwa ni protein na hupendelea zaidi protein ya kwenye ubongo wa mwanadamu, hivyo basi akiingia mwilini hukimbilia kwenye ubongo kisha anaanza kuishi uko

Anaitwa Taenia solium husababisha Cysticercosis pamoja na Taeniasis

Bangi hii bwana ni uraibu na ina uraibu mkubwa nakumbuka Bro's wangu wawili km sio watatu imewachukua hii kitu

Wa kwanza alikua akivuta bangi ndio anapata stimu za kulima so akienda shamba chakula chake kikubwa kilikua ni Bangi na alikua analima mchana wa jua Kali saaana yaan akishapiga bangi zake kete kadhaa akishanyonga akavuta mipuli yake kadhaa anaingia shamba analima na alikua analima sio kawaida, but siku ya siku ilimchukua maana alianguka shambani ile kumuwaisha hospital wakagundua kaishiwa maji ikabidi wamwekee dripu za maji wakaangaika madaktari weee kumkomboa ila hakumaliza wiki akavuta pumzi ya mwisho

Wa pili yeye pia alikua anavuta bangi ila hali chakula chochote kwa hio the same alivuta siku sababu ya kupungukiwa maji na alikua ameanza kua mental retarder, naye akavuta pumzi ya mwisho bangi ikamchukua

Wa mwisho yeye alikua ndio anaanza kuingia kwenye uraibu wa kuvuta bangi sasa bahati mbaya siku hio amevuta akapanda kwenye bodaboda wanaenda club na wenzake si akajisahau kwamba yupo kwenye bodaboda akajirusha akaangukia kichwa huo ndio ukawa mwisho wake maana alipasuka fuvu la kichwa na damu zilivilia kwenye ubongo baada ya siku 3 tukamzika

Gongo sio nzuri hii pia imenipotezea brother wangu mwingine, yeye huyu alikua akishapiga urabu wake anawavizia wake za watu anaokunywa nao gongo kisha anawamega, basi akategewa mtego kuna mke wa mtu alikua anammendea mmewe akawa amegundua mchezo wa jamaa kwamba Jamaa anamla mkewe sasa siku ya siku Jamaa akajichanganya akaenda kwa huyo mwanamke wakafanye yao Jamaa alipokutwa red-handed akakatwa bega kwa panga, bro hakumaliza wiki nae alipoteza maisha

Sasa umeona ubaya wa hivyo vitu kwenye jamii na mifano hai tunayo

NB:

Kuna watu bangi haiwadhuru ila inawachukua taratibu wanakufa kidogo kidogo yaan inawatafuna kidogo kidogo

Kuna watu Kitimoto hawadhuru ila inawachukua wanakufa kidogo kidogo mpaka aje kushtuka mwili mzima umejaa minyoo tupu hapo ndipo mtu anarukwa na akili

Kuna watu gongo haiwadhuru ila inawachukua taratibu wanakufa kidogo kidogo yaan sura ya kizee ila ni mtoto tu wa miaka 20

Sipendi bangi
Sipendi gongo
Sipendi kitimoto

Nayajua madhara yake ni makubwa kuliko wengine wanavyoyachukulia

Nitarudi...
Nyie jamaa huwa mnajitekenya ma kisha mnacheka wenyewe.....
Nna babu yangu amefariki mwaka 2019 akiwa na miaka 115 (iringa image)
Na alikuwa mlaji mzuri sana wa hii kitu...
Katika kupiga piga story nae anadae toka ujana wake karibia kila wiki lazima apate hii kitu ikizidi sana labda wiki 3 na kule upatikanaji wa hii kitu ni rahisi sana....
kama umeandikiwa miaka michache ya kuishi hata ufanyeje muda ukifika unadanja tu....
Sasa hapo ni kwamba mnataka kuaminisha kuwa asingekula kitimoto angeishi miaka zaidi ya hiyo?
 
Nani kasema kitimoto ni Haram? Hao wanaosema Haram huku mtandaoni mbona tunakula nao hapa!
 
Nyie jamaa huwa mnajitekenya ma kisha mnacheka wenyewe.....
Nna babu yangu amefariki mwaka 2019 akiwa na miaka 115 (iringa image)
Na alikuwa mlaji mzuri sana wa hii kitu...
Katika kupiga piga story nae anadae toka ujana wake karibia kila wiki lazima apate hii kitu ikizidi sana labda wiki 3 na kule upatikanaji wa hii kitu ni rahisi sana....
kama umeandikiwa miaka michache ya kuishi hata ufanyeje muda ukifika unadanja tu....
Sasa hapo ni kwamba mnataka kuaminisha kuwa asingekula kitimoto angeishi miaka zaidi ya hiyo?
Bado haujanisoma nimesema kuna watu haiwadhuru kwa sababu wanajua kui-dilute na wanajua kuishi nayo pasina kuwaletea madhara ila inawatafuna ndani kwa ndani, ushaelewa sijui?

Ila naona wewe kunielewa itakua ni ngumu sababu ushajilisha unachokiamini kuna maswali haukuwahi kumuuliza babu yako that's why ungemuuliza usingepinga nilichokueleza

Bangi mbaya
Gongo mbaya
Kitimoto mbaya

Tumia kwa kujihatarisha wewe binafsi hakuna anaekukataza ili hata km yakikukuta huna wa kumlaumu ni wewe na nafsi yako na usiseme hukuambiwa
 
Ngurue kwa wakristo anakatazwa tusile kwa sababu haja meet criteria za kuwa na kwato na kucheua, mcheuo ni kiungo muhimu sana[emoji28]. Kuna wengine kama ngamia na sungura hawna izo sifa! Mungu alimwambia Musa atuambie tule wanyama wenye kwato na wanaocheua kasome Mambo ya walawi 11:27 japokua sisi tunakula sijajua kwa upande wa hawa ndugu zetu wa vibandiko au wanapenda mcheuo sana[emoji23].

Kuhusu bangi, gongo, sigara, ugoro na vyote vyenye madhara kwa maisha na afya ya binadamu: sababu ni dhambi. Kwenye theologia ya kikatoloki kuna dhambi inaitwa "sin of desperatio" dhambi ya kukataa huruma ya Mungu aliekupa uhai, kwa kutumia hivo unahatarisha uhai wako ambayo ndio huruma ya mungu.
Kumbe ngamia hana kwato hacheui
Mbona waislam wanakula??
 
Tangu nakua mpaka sasa nishazeeka nasikia kuwa Gongo, Bangi na Kitimoto ni haramu. Hivi uharamu wake upo kwenye nini hasa?

GONGO
Uharamu wa Gongo upo kwenye vikorombwezo vinavyotumika kuitengenezea? Kwenye vyombo vinavyotumika kutengenezea ama kunywea? Upo kwenye sehemu inaponywewa au kwa wauzaji wake? Au Uharamu wake upo kwa wanywaji wenyewe?

BANGI
Uharamu wa Bangi ni kwa jinsi inavyolimwa, inavyovunwa, inavyovutwa, maeneo itokako, wavutaji wake au jina lenyewe ndiyo haramu?

KITIMOTO
Huyu mnyama uharamu wake ni kutokana na ngozi yake ilivyoshikana na nyama yake, rangi yake, sauti yake, pua yake, kujaa kwake mafuta, ama tabia yake ya kupenda kujigalagaza kwenye matope?

Hebu tujadiliane jamani!!
Bangi sio haramu aiseh
 
Back
Top Bottom