Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Yes it happens; you love all your kids, but you like one the most

1. Single parenting; kuna wale wazazi ambao walijikuta wanalea mtoto peke yao kwa sababu moja au nyingine; automatically mapenzi yao yanakuwa makubwa sana na huyo mtoto kuliko watoto wengine atakaowalea na mwenzie. Mtoto anaumwa, anaumia, kila function upo wewe tu; maisha yenu revolve around each other; automatically upendo utaegemea sana kwao. Ingawa kuna wengine ile chuki juu ya mzazi mwenzie aliyemuacha labda, na uchungu wa kumlea mtoto peke yake; anahamishia uchungu wote kwa mtoto, aisee mtoto atateseka hadi ajiulize kama huyu ni mzazi wangu kweli.

2. Mazingira ya kutungwa mimba, kuilea hadi kujifungua na malezi kwa ujumla. Mzazi/Couple ambayo imehangaika sana kutafuta mtoto afu ikaja kufanikiwa kumpata mtoto baada ya struggles nyingi; upendo kwa huyo mtoto wa kwanza utakuwa ni mkubwa zaidi.

-Kuna wale unakuta wakati mama ana mimba labda ikawa inamsumbua sana, kakaa bed rest, sijui kajifungua ikabidi wabaki months hospitalini na mtoto; hako katoto kanatokea kupendwa zaidi ya wenzie

-Mtoto mgonjwa au anayehitaji special need, anachukua nafasi na muda wa wenzie zaidi. Ndiyo maana kuna baadhi ya wazazi/familia, wanaamuaga kutoongeza watoto wengine ili wampe attention yote yule mwenye special need.

3. Kuna watoto ambao wanapendeka kirahisi zaidi. Mtoto mwingine akishakusalimia amemaliza, huyo anaenda kucheza; wakati mtoto mwingine akishakuona tu kashakukimbilia, mara kakuletea hiki na kile, mara kakufanyia hivi, mara kaja kukaa mkapiga story; yaani anakuonyesha upendo hadi basi. Mtoto wa hivi automatically atakuwa anapendwa zaidi na wenzie. Kuna ka-niece kangu kenyewe hakana habari na mtu yoyite zaidi ya kaka yake; hata akilia haiti mama au baba, anaita tu kaka

4. Mtoto anaye-share/serve interest za mzazi;mzazi anajikuta anampenda mtoto huyo zaidi. Mfano kuna watoto wazito na watoto wepesi wa kazi; kukiwa na kikazi tu huyo ashanyanyuka kusaidia. Mzazi anajikuta yupo karibu na huyo mwepesi zaidi. Labda mzazi anapenda kitu fulani na mtoto anakipenda pia, automatically hawa wawili wanaconnect zadi

5. Last borns wengi wanapendwa zaidi.

6. Mtoto ambaye ni wa jinsia ya pekee kwenye familia yao; mara nyingi anakuwa kipenzi cha wazazi hata na wenzie. Mfano ukute familia ambayo mtoto wa kike ni mmoja tu; huyo anakuwa kipenzi zaidi na roho ya baba yake; wa kiume wa pekee ni pumzi ya mama yake.

7. Watoto wanaopewa majina ya kurithi ya bibi/babu/kipenzi cha mzazi. Ule upendo alionao mzazi kwa yule mwenye jina, huwa unahamishiwa kwa mtoto aliyerithi jina hilo.

N:B Ingawa kupendelea mtoto ni kama kitu kisichozuilika; inabidi wazazi tuwe makini sana. Huwa inaleta chuki na madaraja kwa watoto as wale wengine wanaona kama wenyewe hawapendwi; au wengine wanajikuta wana inferiority complex; anajihisi si bora kuliko yule anayependwa zaidi. Ingawa wazazi huwa tunajitetea sana like "sio kweli, tunawapenda wote sawa".

Changamoto niliyoi-notice haswa kwa baadhi ya wamama; ni pale ambapo favorite child wa baba anakuwa si mtoto wa mama wa kumzaa (mtoto wa nje wa mume). Huo moto utakaochochewa kati ya watoto wa nje na wa ndani mmh. Au huyo mtoto akiwa ndiyo mtoto pekee wa baba; hali ndiyo inakuwa tete zaidi . Mungu anatuona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kudeka tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna upendeleo wa kuwa first born au last born. Kuna upendeleo wa kufanana na Baba/Mama. Kuna upendeleo wa kitabia kuwa msikivu, msafi, kufanya vizuri shuleni, kusaidia kazi mbali mbali za nyumbani, kuwa na heshima na adabu si nyumbani tu bali hata kwa majirani na shuleni pia. Hivyo mtoto kama huyu anakuwa hana usumbufu wowote kwa Wazazi wake pale mtaani au shuleni ukilinganisha labda na ndugu zake au watoto wa majirani. Hivyo unakuta Wazazi wanampenda sana huyu japo wanaweza kuwa hawaonyeshi wazi wazi.

 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Hili toto dogo lilikuwa nyweeeee nyweeeeee na sasa wamekuwa kidogo. So ikitokea leo hii amelia hata I won't bother much nishazoea naona ni deko tu. Hili ni litubdu, likorofi na ngumi nje ila mwepesi kushtaki.

 
Ukweli ni kwamba hakuna mzazi anayependa Watoto wote wapo watoto kadhaa lazima awapende zaidi. Upendo haugawanyiki wapo utakaowapenda kwakua ni uzazi wako na wapo utawapenda zaid, nitatoa mifano.
-Bibi yangu.
Katika watoto waote 11 mtoto mmoja tu ndio anapendwa zaidi kuliko hata sisi wajukuu hatupendwi kama huyo bamdogo apendavyo. Hivi ukipika uji nani wa kupewa sufuria alambe kama sio mtoto mdogo ila siku hiyo bibi alimpatia mwanae huyo sufuria la uji alambe wakati bamdogo nae ana mtoto mdogo.

-Mimi mwenyewe
Katika wadogo zangu yupo mmoja wa kike ndio roho yangu. Inawezekana ndio binaadamu namba moja ninaempenda zaid kwa ajili yake niko tayari kumfanyia lolote na vile napenda Watoto wa kike hafu kwetu hamna kizazi cha watoto wa kike,picha yake Ndio wallpaper yangu kwenye simu😎😎

-Mungu
Tunaambiwa Mungu hana Upendeleo ni kweli ila kuna viumbe Mungu anawapenda zaidi.
1. Yesu ndio kiumbe namba moja kuliko kiumbe chochote mbele za Mungu.
2. Kwa binaadamu Daudi ndio Mwanadamu aliyependwa na anayependwa na Mungu kuliko mtu yoyote katika hiatoria ya ulimwengu. Zamani ulikua hata ukiongopa hapo hapo unakufa ila Daudi alikua anachezea sharubu za Mungu awezavyo. Kaua watu wengi, kaiba wake za watu wengi, Kasema uongo sana na madhambi mengine kibao
Ila adhabu pekee aliyopewa ni kutokumjengea Mungu Hekalu, sasa hiyo ni adhabu au alipunguziwa usumbufu.
 
Siyo kwa Essau na Yakobo tu ambapo Essau alipendwa na baba, Yakobo akapendwa na mama.

Hata kwa Kaini na Habili... (Habili alipendwa zaidi na Mungu).

Umenivutia sana kwamba at least you know the Bible halafu umesema huna mtoto, vipi kuolewa au kuwa na mchumba?[emoji3]
 
Mambo ya kupendwa au kutokupendwa huwa siyajali,siamini kama kuna mtu ananipenda hata atake kunidhibitishia vipi.
 
Nafanya kila kitu kwa wazazi wangu lakini mama hanikubali kabisa na mimi ndie pekee nina mwekekeo na ni last born. Kidogo mzee alikua hana shida before hajatangulia mbele ya haki, Allah amrehemu.

Kuna mabro chenga, lakin ndio kila kitu. Nikihoji chochote juu ya kutowajibika na kukaa tu pale home kusubiri mim niweke mambo sawa, mama anachukia na sipendi awe anajisikia vibaya.

Licha ya kujitahdi kupambana kwa ajili ya faimilia pale ambapo nitakua sina response nnayoipata ukiwa huna kifua unaweza kulia.

Sijali na wala siwaonyeshi kwamba nahisi hivyo. I'm taking care of them at my best ili kupata baraka za Muumba. Mapenzi ya mtu/mzazi ni hisia binafsi na huwezi lazimisha mpendwe sawa. Maisha yanaendelea.
 
Mimi last born kwenye familia yetu , upendeleo nimepata lkn si ule wa kubagua wengine kwasababu ya ule mtoto wa mwisho hata Kaka zangu na dada zangu walikuwa wananipenda vile vile

mzee alisema yeye hataki kulaumiwa na mtoto yeyote Kama elimu wote nitahakikisha mnasoma na kweli mzee katusomesha watoto wake wote hadi elimu ya dini isipokuwa dada yetu wa kwanza yy alikataaga kusoma alimwambia anataka kuolewa .

Na kitu ambocho nimegundua katika watoto sita wa mzee mm ndio nilikuwa mtoto mtulivu tofauti na ndungu zangu wao walivyokuwa wadogo walikuwa watukutu ,walipiga watoto wenzao kwhy zile shuruba za kipigo kwa mzee sikuzipata hata mabrother walikuwa hawanipigi bali ilikuwa ukinigusa umelikoroga.

Changamoto niliyoipata walikuwa wananichukulia mtoto muda wote hata nilivyo fika 19-20 walini treat Kama bado mtoto😆😆 .
 

Mimi kwetu wa mwisho Kati ya saba, hadi Leo Mabro zangu Wana jelasi na Mimi sababu wao walikulia kipindi cha ukata, halafu mie nilikulia maisha matamu sababu Mama alikuwa kwenye Ajira.

Now Nina watoto watatu, ninaempenda zaidi bint yangu wa pili (3yrs), japokuwa siishi nao, tunaonana kwa mwaka Mara moja (likizo),
Sababu ya kumpenda, ni mcheshi sana.
Wa kwanza wa kiume (12yrs) hatuna ushikaji (analijua Hilo) kutokana Tabia ya uchafu uliopitiliza, hapendi kuoga, kuswaki, kufua ni Mzembe Dunia nzima.
Wa mwisho cha kiume bado mdogo (6 mths), sijamfaidi kabisa nilikaa nae week moja wakati katoka kuzaliwa hadi Leo hatujaonana tena.
 
Basii wanao wana bahati sana kuwa na Mama wa aina yako, maana wengi wanapitia maisha ya upendeleo nje nje maskiini..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…