Chanzo kikubwa kinachopelekea hizi network marketing (Business) kuendelea kushamiri, kuleta sintofahamu na kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa kiuchumi kwa wanajamii ni uelewa/ufahamu juu ya mfumo na namna ya uendeshaji wake.
Twendeni na hii; kuna ule msemo usemao "Mjanja wa leo ni mjinga wa jana na Mjinga wa leo ni Mjanja wa kesho". Ukiachilia mbali uhalali wa kisheria pasi na shaka wa hizi biashara, hila;
- mfumo wake kiuendeshaji umejaa ufinyu wa uwazi juu ya ufanyaji biashara husika &
- ushawishi uliojengwa kwa matarajio makubwa ili mtu aweze kujiunga nao,
Hii ndio changamoto kubwa inayopelekea kila kukicha kusikia uongezeko la watu kulalamika juu ya kuingizwa mkenge lakini kiuhalisia ilionekana ni fursa ya kumkwamua mara baada ya kupata hizo taarifa zisizo na ukamilifu, jumlisha matarajio makubwa bila kupewa A to Z juu ya changamoto na ugumu wa kuyafukia hayo matarajio.
Nyongeza ni kuwa; hizi biashara ukifuatilia kwa jicho la kipembuzi hasa utagundua kuwa muundo wake na walengwa haswa ni wale watu kuanzia kipato Cha kati kwenda juu, sasa ugumu unakuja pale wakina sisi wa kipato Cha chini tunapoona fursa na kuchangamkia kujiunga huku network yetu ni wenzetu kama sisi ambao kumudu hizo gharama za manunuzi ya hizo bidhaa tunazobeshwa haupo! Hapo lazima kuvurugwa n kurudishwa nyuma maradufu kutokee, kifuatacho baada ya kushindwa kuuza basi ni lazima ushawishi wengine wajiunge hata kama ukijua wazi kuwa mambo ni magumu ili uambulie commission za ushawishi.
Nawasilisha machache niliyopata kung'amua kwa namna ya hizi biashara.