Hivi unaanzaje kuwashtaki Qnet?

Hivi unaanzaje kuwashtaki Qnet?

Hao waliopigwa pesa ingefaa zaidi na wangeinamishwa iwe funzo kwa wengine hakuna maisha mazuri ya short cut.
Short cut=101% risk.
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Ukiwa sehemu ya Qnet, unapaswa ufanye kazi sana ili upate na wenzako wapate. Hapo short cut inatoka wapi?
 
Kwa mapigo ya hao jamaa ya kupiga suti hadi usiku nimegundua hapa mtaani Kwangu wapo hao jamaa .
Kuna nyumba hapa mtaani Kwangu imepangwa na hao jamaa zaidi ya 30 vijana wa kike na kiume nilikuwa najua ni hosteli ya wanafunzi wa chuo kumbe ndio hawa jamaa. Manake kuna sehemu Kwa mama ntilie mmoj wanaenda kula wanaagiza wali au ugali wa elfu tatu wanawekewa Kwenye sinia moja na mboga kwenye bakuli moja kubwa wanakula hata 7
Ila jamaa wanavitafuna hivyo vibinti
Ngoja nimshtue Kheri James awashukie manake ni wilayani kwake
Kheri james mbona alishaenda tayari aliwakuta maeneo ya kibamba
 
Chanzo kikubwa kinachopelekea hizi network marketing (Business) kuendelea kushamiri, kuleta sintofahamu na kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa kiuchumi kwa wanajamii ni uelewa/ufahamu juu ya mfumo na namna ya uendeshaji wake.

Twendeni na hii; kuna ule msemo usemao "Mjanja wa leo ni mjinga wa jana na Mjinga wa leo ni Mjanja wa kesho". Ukiachilia mbali uhalali wa kisheria pasi na shaka wa hizi biashara, hila;
  • mfumo wake kiuendeshaji umejaa ufinyu wa uwazi juu ya ufanyaji biashara husika &
  • ushawishi uliojengwa kwa matarajio makubwa ili mtu aweze kujiunga nao,
Hii ndio changamoto kubwa inayopelekea kila kukicha kusikia uongezeko la watu kulalamika juu ya kuingizwa mkenge lakini kiuhalisia ilionekana ni fursa ya kumkwamua mara baada ya kupata hizo taarifa zisizo na ukamilifu, jumlisha matarajio makubwa bila kupewa A to Z juu ya changamoto na ugumu wa kuyafukia hayo matarajio.

Nyongeza ni kuwa; hizi biashara ukifuatilia kwa jicho la kipembuzi hasa utagundua kuwa muundo wake na walengwa haswa ni wale watu kuanzia kipato Cha kati kwenda juu, sasa ugumu unakuja pale wakina sisi wa kipato Cha chini tunapoona fursa na kuchangamkia kujiunga huku network yetu ni wenzetu kama sisi ambao kumudu hizo gharama za manunuzi ya hizo bidhaa tunazobeshwa haupo! Hapo lazima kuvurugwa n kurudishwa nyuma maradufu kutokee, kifuatacho baada ya kushindwa kuuza basi ni lazima ushawishi wengine wajiunge hata kama ukijua wazi kuwa mambo ni magumu ili uambulie commission za ushawishi.

Nawasilisha machache niliyopata kung'amua kwa namna ya hizi biashara.
 
Aisee hivi huu upumbavu kumbe ulikuwa bado unaendelea? Nakumbuka nikiwa UDOM enzi hizo hawa jamaa hadi chakula cha mchana na vinywaji waliandaa baada ya kuwasikiliza kwa umakini saana nikagundua Mimi ndo fursa kwao yaaani daah ,wanatoa ushuhuda hao Mara kuna waliofanikiwa hadi wakanunua range (gari) Mara kuna mmoja aliacha ualimu na akajoin akapiga pesa yaan wana maneno hao?
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Ukiwa sehemu ya Qnet, unapaswa ufanye kazi sana ili upate na wenzako wapate. Hapo short cut inatoka wapi?
Sasa kama ni kazi yenye normal procedure kwanini ifungwe na kuonekana ya kitapeli?
Vijana wameingia huko kwa kuaminishwa in very short time watakuwa milionea that's why hata salamu yao wanasema "good morning millionaire"
 
Kuna wale madogo wa mbezi walikuwa wanahojiwa...mmoja akasema yeye amenunua centa kwa million tano, mi nikajua hiyo centa ni gari...
Kumbe chakula!![emoji23][emoji23][emoji23]
Halafu hizo tiba lishe zipo tuu mtaani kwa bei za elfu 50 mpaka laki [emoji12][emoji12]
 
Mimi huwa najiuliza, hii Qnet ya bongo na huko nje ya nchi ni tofauti? Mbona matangazo ya Qnet yanaonekana mpaka kwenye ligi ya England!!!
Ni walewale, ... wameishatengeneza mpunga wa kutosha kwa hiyo kulipia hivyo vi'advertisements' kwao sio issue kiviile!
NB: Wale waliowahi na kushawishi watu wengi kulanguliwa bidhaa za QNET wameonja mafanikio kiasi!
 
Chanzo kikubwa kinachopelekea hizi network marketing (Business) kuendelea kushamiri, kuleta sintofahamu na kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa kiuchumi kwa wanajamii ni uelewa/ufahamu juu ya mfumo na namna ya uendeshaji wake.

Twendeni na hii; kuna ule msemo usemao "Mjanja wa leo ni mjinga wa jana na Mjinga wa leo ni Mjanja wa kesho". Ukiachilia mbali uhalali wa kisheria pasi na shaka wa hizi biashara, hila;
  • mfumo wake kiuendeshaji umejaa ufinyu wa uwazi juu ya ufanyaji biashara husika &
  • ushawishi uliojengwa kwa matarajio makubwa ili mtu aweze kujiunga nao,
Hii ndio changamoto kubwa inayopelekea kila kukicha kusikia uongezeko la watu kulalamika juu ya kuingizwa mkenge lakini kiuhalisia ilionekana ni fursa ya kumkwamua mara baada ya kupata hizo taarifa zisizo na ukamilifu, jumlisha matarajio makubwa bila kupewa A to Z juu ya changamoto na ugumu wa kuyafukia hayo matarajio.

Nyongeza ni kuwa; hizi biashara ukifuatilia kwa jicho la kipembuzi hasa utagundua kuwa muundo wake na walengwa haswa ni wale watu kuanzia kipato Cha kati kwenda juu, sasa ugumu unakuja pale wakina sisi wa kipato Cha chini tunapoona fursa na kuchangamkia kujiunga huku network yetu ni wenzetu kama sisi ambao kumudu hizo gharama za manunuzi ya hizo bidhaa tunazobeshwa haupo! Hapo lazima kuvurugwa n kurudishwa nyuma maradufu kutokee, kifuatacho baada ya kushindwa kuuza basi ni lazima ushawishi wengine wajiunge hata kama ukijua wazi kuwa mambo ni magumu ili uambulie commission za ushawishi.

Nawasilisha machache niliyopata kung'amua kwa namna ya hizi biashara.
Waliojoin mwanzon kipind kampuni inaingia bongo wamepiga pesa Sana... Hao wamekula commission ya wote waliojoin baada Yao na kipind hcho kampuni ilikuwa inagharamia kila kitu ili kujitanua, walikuwa na easy acceleration..
Sasa wale wakrungwa wenzagu walioingia baada ya miez kadhaa kampuni kuwa viral Nchini ndo walikiona/Wanakiona cha mtema kuni 😊
 
Back
Top Bottom