Hivi unajisikiaje kushindwa kuwatunza wazazi wako?

Hivi unajisikiaje kushindwa kuwatunza wazazi wako?

Kukulea kwa shida hayo ni matatizo yao, sidhani kama kuna uhusiano na wewe kuwasaidia.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Kuna tangazo moja la biashara Marwkani.

Baba Mzee kaka na mtoto wake kijana wanataka kuaguza chakula mgahawani.

Baba anataka alipe yeye, akiona huyu kijana bado hajajiimarisha kwenye kazi na kuweka akiba ya kutisha, si sawa alipe yeye.

Mtoto naye anataka alipe yeye, akisema huyu baba ni mstaafu, hana kazi, chanzo chake cha mapato ni pensheni tu.

Wote wanalindana, wanagombea kulipa.

Kila mtu anamfikiria mwenzake na kumuonea huruma.

Hivyo ndivyo inavyotakuwa.

Afrika utakuta mtu kijana hana uwezo, kazi ndiyo kwanza anaanza, hapohapo anabandikwa mzigo wa kutunza wazee ambao wenyewe walicheza ujanani hawakujiandaa na maisha ya uzeeni.
 
Binafsi siwezi msaidia Wazazi kifedha sababu wanajiweza sana kuliko mimi ie si waajiliwa na hawajawahi

Nilichojifunza ni kuwa hata mimi sitakiwi saidiwa na mtoto wangu chochote kile labda kwenye ugonjwa pekee ie kulala hospital etc
 
Kuna wazazi wengine wamewatelekeza watoto wao mpaka ukubwani ndio wakajitokeza, na hao nao watoto wana wajibu wa kuwalipa fadhila?
Hii ndo kizazi cha Leo wamekumbwa mno
 
Binafsi siwezi msaidia Wazazi kifedha sababu wanajiweza sana kuliko mimi ie si waajiliwa na hawajawahi

Nilichojifunza ni kuwa hata mimi sitakiwi saidiwa na mtoto wangu chochote kile labda kwenye ugonjwa pekee ie kulala hospital etc
Huu mpango wa kufanya watoto pensheni kiufupi ni ujima.
 
IMG_3333.jpg
 
Hili la laana naona ni kweli, maana jamaa sasa yupo yupo tu kama kachanganyikiwa fulan. Muda mwingine anakaa peke yake na kuongea ongea mwenyew.
 
Hili la laana naona ni kweli, maana jamaa sasa yupo yupo tu kama kachanganyikiwa fulan. Muda mwingine anakaa peke yake na kuongea ongea mwenyew.
Na wanalaanika kweli mkuu
 
Si afadhali huyo wa familia. Kuna jamaa alishindwa kumtumia mama yake hela ya kufanyiwa oparation ya uvimbe tumboni.

Kisa alikuwa ashamuahidi demu wake kuwa atamkatia ticket ya ndege aende kwao akale Xmass na mwaka mpya.
Mwisho wa siku mama wa watu kafariki kwa kukosa kufanyiwa hiyo oparation baada ya kukosekana mtu wa kumlipia na yule jamaa demu alipoondoka mawasiliano yao au uhusiano wao ukawa umekufa maana demu alikuwa kicheche balaa.
Mapenzi Ni uchizi kweli
 
Kusaidia wazazi ni kitu kizuri.

Ila, kila mtu inabidi ajipange kuweza kujisaidia yeye mwenyewe.

Ukitegemea kusaidiwa na mwanao, vipi mwanao akifariki kabla yako?
Sawa ila kama upo wewe mwanao ni vizuri na hata kama mzazi ni billionea hela ya mtoto ni tamu sana
 
Tusiwaache wazazi wetu wateseke jamani, angalau tuwe tunawasaidia kwa kidogo tulichojaliwa na Mungu atatubariki siku zote.
 
Huu mpango wa kufanya watoto pensheni kiufupi ni ujima.

Wanawatishia ATI watalaanika😂😂😂

Yaani kuna fikra zingine zinachekesha Sana.
Ukisikia Imani potofu ndio hizo SASA.

Yaani mzazi anaona kabisa kijana bado anajitafuta, ndio Kwanza hata Kodi na Pesa ya chakula inampiga Chenga.
Alafu mzazi huyo anakuandama, na kukubagaza na vitisho vya kizamani ati nitakulaani sijui hautapata kamwe, yaani kuna wazazi wapuuzi Sana.

Na watoto wengine Kwa ujinga, wanaingia uoga Kwa kudhani huenda kweli mabaya yatawakuta, kumbe hakuna kitu kama hicho.
Wanakopa atibili wasaidie wazazi wao.

Ninawafahamu Watu wanaofanyiwa ukatili huo na Wazazi wao, Kwa majina na kuwaona Kwa macho hivi. Miaka nenda Rudi ndio Kwanza matatizo yanaongezeka licha ya kutamkiwa maneno ya Baraka na Wazazi wao kisa wanawatumia Pesa 😂😂

MTU atume Pesa Kwa mzazi Kwa sababu ya upendo na uwezo wake. Hiyo Ipo Sawa. Lakini sio ili abarikiwe au Kwa kuogopa kulaanika😂😂 hiyo ni Akili mgando
 
Back
Top Bottom