Hivi unajisikiaje kushindwa kuwatunza wazazi wako?

Hivi unajisikiaje kushindwa kuwatunza wazazi wako?

Sawa ila kama upo wewe mwanao ni vizuri na hata kama mzazi ni billionea hela ya mtoto ni tamu sana
Mambo ya Kiafrika haya.

Sasa tuseme mzazi bilionea, mtoto kapuku, halafu bado anaona hela ya mtoto tamu?

Huu kama si ubinafsi ni nini?
 
Wazazi huona ufahari kuhudumiwa.

Usipotoa wanakulaani na kukusemea maneno mabaya
Haya mawazo ni ya ubinafsi sana na ndiyo yanatufanya tuzidi kuwa masikini.

Tumefanya watoto kama bima au mafao ya uzeeni.

Badala ya wazazi kuwekeza kwa maisha yao ya uzeeni tangu wakiwa vijana, wanategemea watoto.

Hao watoto wakifa kabla ya wazazi, wazazi watafanya nini?

Mimi sipangi kumtegemea mtoto, labda ajiongeze mwenyewe tu.
Na akitaka kunisaidia sana, nitamshangaa na kuhoji kama anajiwekea akiba yake yeye mwenyewe ya uzeeni ya kutosha.

Zaidi, mimi kama mzazi ni wajibu wangu kumuwezesha mtoto.

Yani, nimsomeshe, nimfikishe sehemu ajitegemee, akifika hapo focus yake iwe kwa watoto wake, si mimi mzazi tena.

Sasa Kiafrika tunamfanya mtu anaanzisha familia yake, watoto wanamtegemea, hapo hapo na wazazi wanamtegemea.
 
Yaan wamekulea kwa shida, wamekusomesha kwa shida ila kaz uliyopata na tayari una familia inayokutegemea then hiyo familia yako ikakufanya ukashindwa kutunza wazazi au kuwasaidia wazazi, huenda kuna muda wanakusaidia wewe kwa kidogo walichonacho kwa sababu wanaona magumu yako.

Unajisikiaje eti? [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Kwa mfano huna hao wazazi nikimaanisha walisha tangulia mbele ya haki je kaka ndie mlezi au jirani, na isitoshe kuna watu hawajui nini maana ya mzazi. Unadhani atasaidia nini?.
 
Haijalishi kidogo ampacho mama yake niraha sana hujui tu
Hata nyonyadamu ujue huwa anaona raha sana.

Kumbe anaua wenzake.

Point si raha yako wewe, huyo anayetoa anaweza?

Kama anaweza sawa, kama hawezi unaweza kumpukuta mtu mpaka nauli ashindwe kupanda daladala, kisa wewe unataka raha tu.
 
Kwa mfano huna hao wazazi nikimaanisha walisha tangulia mbele ya haki je kaka ndie mlezi au jirani, na isitoshe kuna watu hawajui nini maana ya mzazi. Unadhani atasaidia nini?.
Atamsaidie aliyemlea
 
Hali ya uchumi nayo ni ngumu To yeye beybe I love you, nipe hata namba bas .
 
Unakamoyo kauchoyo kimtindo Mkuu...
Hapana.

Mimi nishawafungulia watu biashara hapahapa JF, wala siwajui, wamenililia tu nikawapa msada.
Hivyo, ninapoandika mambo ya principle, si kwa uchoyo.

Na nyumbani juzi nimewatumia wazazi $1,000 washerehekee sikukuu za mwisho wa mwaka vizuri.

Wakasema Krismasi ilikuwa "Fabulous".

Uchoyo hapa ni kumnyenga mtoto.

Yani wewe mzazi umeishi miaka kibao, umepata muda wa kujiandaa na miaka ya uzeeni.

Hujajiandaa, umefeli maisha. Kumnyenga mtoto ni vibaya, ulitakiwa kumuandaa na kumuacha ahudumie watoto wake na yeye ajiandae kwa maisha ya uzeeni.

Kama umeyapatia maisha, uko vizuri, ndiyo kabisaa kumnyenga mtoto vibaya

Badala ya kumuachia mtoto naye ajipange kuhudumia watoto wake, mnamuongezea mzigo awe anahudumia wazazi na watoto.

Kuhudumia wazazi ni optional, si lazima.

Kuhudumia watoto ndiyo lazima.

Wazazi hujawaleta duniani, wamekuleta wao.

Watoto umewaleta duniani.
 
Back
Top Bottom