Hapana.
Mimi nishawafungulia watu biashara hapahapa JF, wala siwajui, wamenililia tu nikawapa msada.
Hivyo, ninapoandika mambo ya principle, si kwa uchoyo.
Uchoyo hapa ni kumnyenga mtoto.
Yani wewe mzazi umeishi miaka kibao, umepata muda wa kujiandaa na miaka ya uzeeni.
Hujajiandaa, umefeli maisha. Kumnyenga mtoto ni vibaya, ulitakiwa kumuandaa na kumuacha ahudumie watoto wake na yeye ajiandae kwa maisha ya uzeeni.
Kama umeyapatia maisha, uko vizuri, ndiyo kabisaa kumnyenga mtoto vibaya
Badala ya kumuachia mtoto naye ajipange kuhudumia watoto wake, mnamuongezea mzigo awe anahudumia wazazi na watoto.
Kuhudumia wazazi ni optional, si lazima.
Kuhudumia watoto ndiyo lazima.
Wazazi hujawaleta duniani, wamekuleta wao.
Watoto umewaleta duniani.