Hivi unajisikiaje kushindwa kuwatunza wazazi wako?

Sawa Mkuu....mi naumia sana kuona nashindwa saidia mama yangu
 
Sawa Mkuu....mi naumia sana kuona nashindwa saidia mama yangu
Unaujua msemo wa Kiingereza unaosema "The road to hell is paved with good intentions"?

Unaelewa mana ya msemo huo?
 
Sielewi kabisa mkuu
Kuna mambo mengine unaweza kufanya kwa nia nzuri kabisa, kumbe ndiyo unaharibu.
Unaweza kuwa na nia ya kusaidia, uwezo huna, nia yako nzuri inaweza kukuletea ugonjwa wa moyo buree.

Maisha yana kupata na kukosa, ukiweza ku hustle mpaka ukapata, sawa, saidia unayetaka.

Ukikosa na ushafanya jitihada zote, usijione mnyonge sana kwa kukosa ukajitia jakamoyo litakalokuzidishia simanzi bure bila tija.

Kama una watu waelewa watakuelewa tu, kama wasipokuelewa, hilo ni tatizo lao, si lako.
 
Asante mkuu
 
Ni kazi ya wazazi kulea watoto wao, na siyo kutegemea kwamba hao watoto watawalea wao wakisha kuwa wakubwa. Ila kama watoto wana uwezo siyo mbaya wakilea wazazi wao pia. Jukumu la watoto wakishakua ni kulea watoto wao pia. Forward generational support, not the reverse
 
Sawa mkuu
 
Amen to this! On point
 
Waafrika tulishakosea kitendo Cha wazazi kusomesha Ili mtoto aje kisaidia na ndio maana kuuwa mzizi wa umaskini ndani ya nyumba zetu ni ngumu mnooo utakuta kijana kapata kazi apo apo anatakiwa kusomesha wadogo zake wakati huo huo anatunza wazazi baada ya miaka mitano inabid aoe wakati huo hajajenga inabidi alipe Kodi atunze mke na Bado familia inamwangalia ni ngumu kuuwa chain ya umaskini ndani ya familia kila kizazi kinaanza upya .
 
Mzazi anatamani kukuona wewe ukifanikiwa na sio kua chuma ulete kwako.
Ukiona mzazi anataka ufanikiwe ili umsaifie aisee wewe ni fursa kwake.
 
πŸ™πŸ‘Šmkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…