Hivi unamuitaje mpenzi au mke wako mama?

Hivi unamuitaje mpenzi au mke wako mama?

ntuchake

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
408
Reaction score
1,549
Kuna kitu ambacho sitakielewa hapa duniani basi ni hii tabia ya wanaume kuwaita wapenzi wao au wake zao mama!

Hivi mpenzi wako anaweza kuwa mama yako kweli? Mtu ambae unalala nae uchi na mnamaliza staili zote za mibinuko unamwita mama?

Au mimi mshamba? Hii ni heshima au ndio mapenzi? Na nyie wanawake ambao wapenzi wenu wanawaita mama uwa mnajisikiaje mkiitwa ivo? Hebu nielewesheni wakuu!!
 
Utakuwa unamaelekezo ya dini au vinginevyo masuala ya majina ktk mapenzi hayana fomula unaweza mwita chura, pimbi, mpenzi, switihati, mai wangu, mwezi, jua etc au kuna majina umekaririshwa na shekhe au mchungaji wako? Watu wakiwa katka sarakasi kitandani wanatukana matusi kama yote kwa raha wanazopeana je, nayo hayaruhusiwi mnataka wakati wa kunyanduana watu waimbe nyimbo za kuabudu au kaswida?
 
Majina yote sawa ila kwangu mimi mama NO! Siezi kua mama wa mtu ambae nalala nae!
 
We
Kuna kitu ambacho sitakielewa hapa duniani basi ni hii tabia ya wanaume kuwaita wapenzi wao au wake zao mama!

Hivi mpenzi wako anaweza kuwa mama yako kweli? Mtu ambae unalala nae uchi na mnamaliza staili zote za mibinuko unamwita mama?

Au mimi mshamba? Hii ni heshima au ndio mapenzi? Na nyie wanawake ambao wapenzi wenu wanawaita mama uwa mnajisikiaje mkiitwa ivo? Hebu nielewesheni wakuu!!
Wewe mshamba sana, pia mimi mke wangu huniita Baba. Kwahiyo tunakuwa baba na mama.
 
Mama kwa sababu anachukua nafasi ya mamangu kunilea, baba kwa sababu ninachukua nafasi ya babake kumlea.

Hayo mawazo mengine ni kwa mujibu wa ujinga wako tu. Sioni kama ukitamka mama au baba unamaanisha kulala nae uchi. Huonesha heshima kati ya baba wa watoto na mama wa watoto wetu.

Maneno haya hutumika wakati watu wamevaa nguo zao na hususani mbele ya watu. Huonesha uimara wa ndoa baina ya wana ndoa, ukamilifu wa upendo wa kweli kati yao na heshima kuu kati yao.

Baba Amina au mama Amina, huonesha kifungu cha ukamilifu na uwajibikaji kama wazazi, ishara ya heshimu ya kutumika katika uumbaji mpya kwa uwezo wa Mungu.

Tuelekeze mawazo huku siyo kwenye kuvuana nguo. Ndo maana wakwezo au wazazi wakikutembelea, utawalaza chumba na kitanda kimoja, huwezi kuwatenganisha. Hao ni baba na mama kama ambavyo sisi ni baba na mama.
 
Back
Top Bottom