Hivi unamuitaje mpenzi au mke wako mama?

Hivi unamuitaje mpenzi au mke wako mama?

Hahah ila kuna watu mnayachukulia mahusiano very serious sana, yaan mm akisema ufike salama babaa na mm nikimjibu take care mamaa mioyo yetu inamwagika mwamwamwa.

Anyway, endelea kuwa serious mwanetu. Baadae njoo na uzi wa kuitana baby pia, maana baby ni mtoto. Point zako ziwe
1. Ni dharau kwa mkeo kumwita baby
2. Ni kama unamlala mtoto
3. Ni kama umemzaa
4.... utaendeleza point nyingine za userious wako

Ukimaliza huo shusha mwingine wa kuitana "honey" hoja iwe unawezaje kuishi na asali? 🤣🤣🤣
 
Mimi siombagi hela! Nikitaka hela naanza kutengeneza mazingira akipiga simu sipokei akituma meseji leo najibu kesho siku ya pili mwenyewe anatuma hela 😂😂
Maana wanatengenezaga Mazingira Kabisa ya kutokuombwa pesa 😅😅😅utaitwa majina kama yote
 
Kila Kitu Kina Mahara Pake Sasa Kuanzia Leo Anza Kumwita Mama Ako "Mke Wangu"Akikupigia Simu Tu Anza Na Hilo Neno Mwambie Sema Mke Wangu Uone Je Atakuchukulia Vipi?Watu Kama Nyinyi Ndo Mlianzisha Mwanaume Kumla Mwanaume Mwenzie Mkiamini Kwamba Haina Shida Tundu Si Lipo!
Kwahiyo babu anavyomuita mjukuu wa kike mke ni mkewe? Na mume kwa mjukuu wa kiume kwa upande wa bibi ni mumewe?
 
Kuna kitu ambacho sitakielewa hapa duniani basi ni hii tabia ya wanaume kuwaita wapenzi wao au wake zao mama!

Duuh… hilo swali unalojiuliza ni swali la chekechea!

Mpaka umri wako huo bado hujajua kuwa MAMA ni… MWANAMKE ALIYEZAA!

Kama umeshindwa kujua hilo basi utakuwa kweli una UDINI ndani yako juu ya hili.
 

Attachments

  • Screenshot_20250201-220059.jpg
    Screenshot_20250201-220059.jpg
    193.4 KB · Views: 2
Sisi tunaoitwa "Nyau" tuna comment kwenye uzi huu huu au tuna uzi wetu?
 
Potelea mbaliii anaekuhudumia shida zako kwa wakati

Ndio unaemthamini na kuhamisha MAPENZI kwake

Na kusahau ulikoheshimiea
 
Mimi na muita baby mama wangu sababu ni gape letu la umri. Hata ivyo kupanga nikuchagua.
 
Mama kwa sababu anachukua nafasi ya mamangu kunilea, baba kwa sababu ninachukua nafasi ya babake kumlea.

Hayo mawazo mengine ni kwa mujibu wa ujinga wako tu. Sioni kama ukitamka mama au baba unamaanisha kulala nae uchi. Huonesha heshima kati ya baba wa watoto na mama wa watoto wetu.

Maneno haya hutumika wakati watu wamevaa nguo zao na hususani mbele ya watu. Huonesha uimara wa ndoa baina ya wana ndoa, ukamilifu wa upendo wa kweli kati yao na heshima kuu kati yao.

Baba Amina au mama Amina, huonesha kifungu cha ukamilifu na uwajibikaji kama wazazi, ishara ya heshimu ya kutumika katika uumbaji mpya kwa uwezo wa Mungu.

Tuelekeze mawazo huku siyo kwenye kuvuana nguo. Ndo maana wakwezo au wazazi wakikutembelea, utawalaza chumba na kitanda kimoja, huwezi kuwatenganisha. Hao ni baba na mama kama ambavyo sisi ni baba na mama.
Umejibu vyema ila tatizo anayejibiwa bado mvulana, hawa ndio wale anakudai unamwambia njoo kesho nikupe hela yako, saa 1 kamili asubhi yuko mlangoni anataka chake.
 
Back
Top Bottom