Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu nimeuliza nipate kusaidiwa kupewa majibu maana nikiangalia na kufuatilia kwa makini naona hatari kubwa Sana iliyopo mbele ya chama hiki, wataalamu wanasema kuwa ukitaka kujuwa urefu wa maisha ya chama chochote Basi huna budi kuangalia uwezo wa kiuongozi wa vijana waliopoo katika chama husika ambao ndio hasa watakao kuwa viongozi wa kesho
Lakini ukiangalia na kutupia jicho kwa vijana waliopoo ndani ya chama hiki na ambao ndio viongozi kwa Sasa kiukweli unasikitika Sana na kuwaza sijuwi wanakula vitu gani huko chamani kwao,
Ni vijana waliokosa adabu hekima busara unyenyekevu na staha, Ni vijana waliojaa matusi utazani wameopolewa kwenye pipa la Pombe ya kienyeji, Ni vijana ambao kwao yoyote na wa umri wowote na wa cheo chochote anaweza kutukanwa matusi yote yanayoandikika na yasiyo andikika, Ni vijana waliojaa mihemuko na kuripuka Kama Moto wa gesi,
Kibaya zaidi vijana Hawa wa chadema Ni Kama hawana mlezi, hawana mtu aliyesimama Kama mzazi wao kimalezi, Hawana mtu wa kuwaongoza na kuwafunda, hawana mtu wakuwapa maelekezo, hawana mtu wa kuwachunga ili wakue kiuongozi, hawana mtu wakuwafunga breki ya midomo yao, Hawana mtu anayeweza Akazungumza wakamsikiliza na kumheshimu, hawana wazee huko, Ni vijana waliozibuka na kuzuzuka, Ni vijana wanao jazana ujinga muda wote, Ni vijana waliokosa muunganiko wa ubongo na midomo yao, hawana muunganiko wa akili na vidole vyao
Ni vijana wanao hisi kuwa huo ndio ushujaa, ukamanda wenyewe, ujana wenyewe. Chadema itafika muda kitakosa viongozi na kwa kuwa Hawa ndio kwa umoja wao wa kujazana ujinga na kukosa adabu na heshima watajikuta mmoja wao anakuwa kiongozi mkuu wa chama, hapa ndipo chama hiki kitakapozidi kupiga mueleka Zaid ya hapa kilipo, ndipo kitazidi kusereleka kuelekea shimoni, ndipo kitakapozidi kusambaratika, ndipo kitakapozidi kupuuzwa Zaid ya hapa
Maana hakuna atakaye kuwa tayari kuwasikiliza watu Kama Hawa waliojaa matusi, watu ambao wapo tayari kumtukana yoyote yule kwa matusi ya nguoni bila kosa lolote kisa tu katofautiana nao, hakuna ambaye yupo tayari na atakuwa tayari kwenda kwenye mkutano wao kusikiliza mimatusi tu, hayupo mtu wa namna hii hata siku moja
Sina cha kuwashauri vijana Hawa waliokosa adabu na hekima maana hiyo siyo kazi yangu, Nachoweza kuwaasa ni kimoja tu kuwa watukanane huko huko lakini ikija kwenye mamlaka ya nchi lazima waiheshimu Sana maana wasije wakafikiri kuwa Rais wa nchi Ni sawa na Rais wa Bao, lazima wajuwe kuwa Rais Ni mkuu wa nchi na kiongozi wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama aliye apa kuilinda nchi hii kwa nguvu zake zote ili iwe na amani na utulivu, hivyo hakuna anayeweza kuwavumilia watu wanao hatarisha usalama wa Taifa, lazima watawajibika na kuwajibishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu