othiambo
JF-Expert Member
- Nov 15, 2014
- 1,995
- 2,795
Hali zenu waungwana.
Hili swali huwa najiuliza sana na sipati majibu, hivi hawa watu vitambulisho hivi vimekua ndio kimbilio na nguzo ya utemi kwa wananchi?
Sababu ya swali langu ni jana kipindi narudi nyumbani kufika kituoni magari hakuna; ghafla ikaja daladala ikitangaza nauli 500 katikati ya safari, mama mmoja akadai mi mia tano sina nina mia nne wakabishana kidogo ndipo mama alipodakia: Hoo! unajua mimi nani au nitoe kitambulisho changu, nikabaki nastaajabu, maskini konda alinywea hapo ndipo nikajua Watanzania kweli hatujui haki zetu. Nikabaki najiuliza maswali makubwa matatu, hasa swali la tatu.
1. Hivi yule Mama na kitambulisho chake hajui njia hii haina usajili na magari, hata tiketi hatupati ndiyo maana makonda wanatuogelea, mbona wanabadili route na hatung'aki?
2. Hivi yule mama mbona bajaji huwa zinapandwa kwa 500 hadi 1000 njia ikiwa mbovu na hawapingi, ikamuume 100 tu?
3. Hivi hawa wenye vitambulisho mbona kwenye vikao vya maendeleo hatuwaoni wakihimiza kwa vitambulisho vyao, maana kama barabara yetu ingekamilika, hawa makonda wasinge tuogelea kiasi hiki na tungebishana kimantiki.
Maana ilbidi iwe imekamilika kitambo sema watu wameruka judo na wenye vitambulisho wanalijua hili na tunaishi nao mitaani. Watu walishalipwa malipo ya kubomolewa kupisha barabara tangu Jakaya, matokeo yake vikitokea vikao wanafuatwa wazee wetu wasiojua pa kutokea tena wanapewa maswali ya kuwauliza viongozi maana majibu yashaandaliwa.
MSITUTISHE NA VITAMBULISHO VYENU BWANA
.