Hivi vitu ndio vilinifanya nigome kutoka Jiji la Dar es Salaam

Mkuu hili swala mbona liko wazi mtu yoyote mwenye utashi na macho anaona na kujua kwa hiyo ni maamuzi yake kutokubaliana na anachokiona ambacho ndio uhalisia wenyewe.

Kinachofanya Dar kuwa special ni mtaji wa watu.
Idadi ya watu wote dar wanahitaji kupata mahitaji yao muhimu kama chakula, mavazi, na makazi na bado pia kuna mahitaji mengine ya kila siku. Kama upo well organized na prepared lazima upige steps.
 
Pamoja na hizo sifa ila Dar ndio Jiji linaongoza kuwa na ufirauni,maisha ya hovyo na kuwa na maskini wengi sana hapa Tanzania..

Kwa misingi hiyo hilo Jiji lilinishinda kiukweli na ambavyo watu ni wengi hadi Kero tupu..
 
Opportunity kwangu ziko Mkoani sio Dar na kiukweli Dar ilinishinda.
 
Pole sana, huijui Dar vizuri mkuu, karibu tena
 
Duh
 
ukiona hivyo we sio mjanja, wewe ni lelemama, mjini mipango mkuu
 
sababu zako ni shallow sana....hayo uliyoorodhesha yanapatikana miji mikuu ya mikoa na ya wilaya na hata midogo nchi nzima kwa sasa. una uchungu tu na baba yako kuhama dar
 
Nimekaa Dar miaka 10 , Pia Arusha . Ni kweli dar ni mkoa ambao umechangamka ila vijana wengi wenye mafanikio wanatoka kaskazin(hususan Arusha na K'njaro) nenda Kariakoo utajionea, Sasa ninyi mnaosema vijana wa Arusha ni washamba nashindwa kuwaelewa wakati ndio walioiteka hiyo dar, Arusha ni mkoa mzuri sana kuishi..Ukiwa Arusha ni kama vile uko mambele.

Acheni chuki binafsi na vijana wa Arusha ilhali ndio wameishika Dar.
 
sababu zako ni shallow sana....hayo uliyoorodhesha yanapatikana miji mikuu ya mikoa na ya wilaya na hata midogo nchi nzima kwa sasa. una uchungu tu na baba yako kuhama dar
Sio kweli mkuu twende taratibu tu,

vijana wanaofanya vizuri katika entrainment umaarufu wao wameupatia wapi?

Ni Mkoa Gani una unafuu wa bidhaa kama Dar es salaam?

Ni Mkoa Gani una ajira nyingi ambazo ni rasmi na hata zile zisizo rasmi kama Dar es salaam?

Mkoa Gani una Taasisi nyingi za elimu za kujiendeleza katika field yoyote zaidi ya Dar es salaam?

Mkoa Gani unamzunguko mkubwa wa pesa kushinda Dar es salaam.?

Mkuu hauitaji hata elimu ya darasa la saba kuziona hizi facts.
 
Eti '..maeneo ya pembeni kama kule Temeke...' natumaini mkuu wewe sio mwenyeji wa Dar, yaani useme Temeke ni pembeni ya jiji? Huwezi kuwa serious labda uwe umejichanganya ulitaka kumaanisha jambo lingine.
Waliopanga wengi hawaishi mbali sana na katikati ya jiji yaani ni ngumu kidogo kukuta mtu ambage mishe zake kila siku ni katikati ya jiji halafu ukute anapanda daladala 3 huyo atakua ni mzembe
 
Hujaelewa point yangu na sina muda wa kuelewesha vilaza. Baki na ukilaza wako.
 
Huko ni pa kutafutia pesa sio kuishi

Dsm kunanuka mavi, pachafu sana
Mo, Rostam, Bakhressa, Balozi wa Uingereza, Marekani, Ufaransa, Japani, Norway, Denmark, na Viongozi wako wote wa chama na serikali, Wastaafu wote wanaishi, wewe Masikini una sema Dar kuna nuka Kaka tafuta pesa Ukiwa dar sawa upo Paris, wewe unatoka Arusha unafikia Kigogo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…