Hivi vitu ndio vilinifanya nigome kutoka Jiji la Dar es Salaam

Kwa umaskini kama huu hapa wataachaje kuishi kwenye mabonde? πŸ‘‡
 

Attachments

  • Screenshot_20220929-194340.png
    123.6 KB · Views: 9
Siku utakayotoka nje ya DSM na kukutana na watu wa mikoani ndo utaja elewa..yani upate exposure ya mikoani halafu uwe na harakati za kutoka..utaja elewa...
Nimeshaenda nje ya Dar mikoa mitatu tofauti

Miwili kati ya hiyo ni bora kwangu kuliko Dar
 
Hata mi nashangaa,graduate wapo online 24hrs na kazi hawana na wazazi wao ni wbkawaida tu.
MKOMBOZI NI BETTING TU.
 
Pole sana mkuu Natafuta Ajira
 
Nakuunga mkono mkuu mi mwenyewe niko Mwanza ila dar kwa mda nilio kaa huwezi ringanisha na mikoa mingine , DSM is next level like USA and Mexico
 
Endelea kukaa kwa
 
Umezaliwa Manzese umekulia Manzese umesoma Manzese umeanza kazi Manzese hili ndio tatizo hautembei hauwezi kuona kipi ni kipya na kipi ni cha zamani..
🀣🀣🀣🀣 ila JF bhana
 
Nakuunga mkono mkuu mi mwenyewe niko Mwanza ila dar kwa mda nilio kaa huwezi ringanisha na mikoa mingine , DSM is next level like USA and Mexico
Ona sasa mtu kama huyu[emoji23][emoji23]
 
Nimeshaenda nje ya Dar mikoa mitatu tofauti

Miwili kati ya hiyo ni bora kwangu kuliko Dar
Umeenda na kurudi au ulifanya maisha(kwa maana ya kukaa muda mrefu) i.e miezi si chini ya 6...? Ni mikoa gani hio...?
 
Ukiwa na connection sahihi popote unatoboa sio lazima dar tu
Mikoani watu wanakunja sana hawafunguki kama watu wa DSM...watu wa bara wengi ni wakunjaji...mfano unaweza anzisha duka sehemu wenyeji wakijua sio wa kwao raia hawaji...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mikoani watu wanakunja sana hawafunguki kama watu wa DSM...watu wa bara wengi ni wakunjaji...mfano unaweza anzisha duka sehemu wenyeji wakijua sio wa kwao raia hawaji...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Me naona kila mtu na uzoefu wake tu me nimezaliwa dar nimekulia dar ila palinishinda nimekuja kujaribu mkoani sasa ukiniambia dar jiji la fursa inakua ngumu kukuelewa hata hapa wa dar wengi wanatoa ushuuda kwa kutumia mifano ya mawaziri na wafanyabiashara wakubwa ila tukiwakagua wao binafsi si ajabu kukuta wapo hapo dar wanabangaiza bangaiza tu
 
Mkuu uko sahihi kulingana na kazi ya ndoto yako kuifanikisha ukiwa jijin dar.

Mm naamini saana maisha ni popote kulinganana na connection zako.

Kwa maisha ya sasa tuna angalia jinsi gani unaweza kupata pesa haijalishi uko jijin au mikoani.

Sijaona kama kuna uepesi wa kupata mtaji kama huna mtaji wa kuishi dar, ugumu unakuja kwnye makazi,Dar sehemu inayoferisha watu kuishi na kuchukia ni sehemu ya makazi yana gharama kubwa, sasa je mtu anae taka kwenda kuanza maisha atamudu?

Ninge penda sana utoe fursa za kuwa shawishi vijana kwenda dar wakiwa na mitaji ya biashara.

Toa mfano wa biashara fulan then fanya analysis yake ilikusudi vijana waje kuinvest jijin na sio kuja kutaabika tu.

Mm sihami mikoan kwa sababu ya fulsa ya kilimo,kw mfano mm nnalima maharage.

Analysis yake kw mwaka huu.
Kukodi shamba ekari 50000
Kukatua na trekta- 50000
Mbegu kg 40 - 80000
Mbolea CAN -150000
Sumu ya wadudu 60000
Total cost =390000
Kipato cha ekari moja ni kati ya kg600-800
Kuhusu bei inategemea na sehemu ulipo lakin kwa sehemu yetu
Current price 2500 per kg.

Na huwa tuna lima kipindi cha.mvua pia na.kumwagilia kiangazi.

Ko ndo fursa mojawapo vijana mnaweza jikita kwa kilimo,now days is so crucial.
We young let's we look opportunities wherever.
Fulsa ni mpango mzima tupeane chanel za kutoboa maisha na sio za kusuza rungu .
 
Nimependa mchango wako mkuu, me nimeona humu ndani watu wanabishana kwa show-offs tu, na bahati mbaya hatuwajui haya majigambo yote si ajabu wanaushi maisha ya shida kinoma ego yao ni kwa sababu tu wapo dar, hata mtoa mada mwenyewe hajaeleza yeye binafsi anajishughulisha na nini ambacho anafikiri kama angekua mkoani asingeweza kutoboa., kuna wengi wapo hapo dar na wamelost mfano mzuri mimi mwenyewe nimekimbia jiji maana nilipigika nikasema ya nini mie kung'ang'ania sehemu moja.. hapa watu wanasema dar mipango nimejaribu kuwaomba mikakati nilitegemea watanionesha njia labda kwa hali yako fanya hiki kwa namna hii ila badala yake nimeishia kuambiwa sio mjanja, lelema, sina connection inshort sijapata reply yoyote positive
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…