Hivi Waafrika hatuna akili?

Akili tunazo sana. Wapo weusi wamegundua teknolojia muhimu duniani. Wapo weusi wameshirikiana na weupe katika kuvumbua teknolojia. Wapo weusi wameibiwa teknolojia walizovumbua (weupe wameziiba na kudai ni uvumbuzi wao). Hata sasa miongoni mwetu kuna weusi wapo wengi tu ambao wanaweza kufanya makubwa katika mambo mbalimbali au vumbuzi mbalimbali. Tatizo ni kujipanga kwetu katika kutambua vipawa mbalimbali.
 
Hivi unataka kusema Communism imeanzia sehemu fulani na kwenda pengine au nini maana ya Communism ? Kabla ya Industrial Revolution na ukiondoa mfumo wa Kifalme unadhani ni mfumo gani ungeweza kuendana na means of production za wakati husika ? Baada ya kuondoa Monarchy (Ufalme lazima kuna Void na ni jinsi gani unaweza kugawanya mali) Kwahio dunia nzima kwa vipindi tofauti kumekuwa na some sort of communism kulingana na system iliyokuwepo.., Kina Karl Marx kufanya hii kitu kwenda mainstream ni kutokana na Unyonyaji ulioletwa na Industrial Revolution kitu kilichoikumba sana Ulaya na kwa Afrika hio haikusumbua huku sababu watu walikuwa na mifumo yao ya Kifalme na Nyarubanja ambayo iligawanya mali na kila mtu aliridhika na his class (Class Struggle hazikuwa kubwa)


Kwahio I can argue all earlier life of family / villages were communist in nature and with the rise of automation and technology and death of capitalism there would be another system which will neither be capitalism nor Socialism but maybe something similar to what China has which is Market Socialism...
 
Hao Mainjinia wakiafrika ulishawahi kuona kiwango cha barabara walizojenga? Nenda Kigoma kaangalie zile two ways zao utanielewa.
Kwani Kijazi flyover ilijengwa na nani? Bila kusahau ya Mfugale?
 
Oya... endelea kuamini kuna ushirikina.

Siwezi kukushangaa kwani 99 asilimia ya waafrika wanaamini ushirikina, wakiwemo wasomi na madaktari,

Wewe ni nani hadi nikushangae?
 
Level ya pure ignorance inayoonekana kwenye hii thread ni heartwrenching. Tuna safari ndefu sana kama majority ya wananchi wana upeo mdogo namna hii.
Inashangaza sana. Waafrika tuna upeo mdogo wa akili, katika level ya ukichaa.
 
Hamna nyenzo ya usafiri wa njia ya bahari ambayo iliundwa na mwafrika; ndio maana hata ukienda hapo kisiwa cha Madagascar wazawa sio waafrika bali na watu waliotokea visiwa vya Asia huko
Bibadamu wote walitokea Africa (fact), hao walioenda ulaya walipaa? Meli zinaundwa kwa Chuma, nani kagundua chuma?
 
Bibadamu wote walitokea Africa (fact), hao walioenda ulaya walipaa? Meli zinaundwa kwa Chuma, nani kagundua chuma?
Nyinyi sasa ndio mnatupaga waafrika majina mabaya, utasikia "ooh hatusomi", mara "ooh hatufanyi research yoyote ila tunapayuka tu"

Ndugu yangu, ufugaji wa wanyama kwa matumizi ya binadamu kama usafiri na chakula sio jambo la kale sana (inaweza isizidi hata miaka 20,000) na binadamu katoka Afrika kitambo sana zaidi ya hapo (yaweza kuwa hata miaka 50,000 iliyopita), kipindi hicho hakukuwa na nyenzo yoyote ya usafiri zaidi ya miguu na safari hiyo haikuwa ya mara moja bali unakuta ilichukua mamia kama sio maelfu ya miaka maana walisafiri wa kutafuta chakula na kwa msukumo wa tabia nchi , waliingia ulaya kupitia mashariki ya kati na wengine wakielekea Asia (tabia nchi ya mashariki ya kati inaonekana iliruhusu safari hiyo kwa kipindi hicho)

Ugunduzi wa chuma sio wa kale sana (inaweza isizidi hata miaka 5000 kabla ya Kristo), na hata hizo meli/mashua nazo ni kipindi hicho hicho (5000 - 8000 kabla ya Kristo)
 
Hii nilishuhudia kipindi cha Covid-19, wakati dunia ikijaribu kutengeneza vaccine. Kila bara walialikwa the best research scientist katika field hiyo. Africa kuna walio apply kwenda kwenye conference hiyo lakini hakuchaguliwa hata mmoja ila mabara mengine yote walichagua mwakilishi angalau mmoja. Kwa picha hiyo unaona dunia inavyowachukulia waafrika katika masuala ya ugunduzi.
 
Wazungu wanaamini mtu mweusi hana uwezo wa kufikiri...
 
Wewe sasa ndio unaonekana taahira, kwahiyo wakati wazungu wanarudi Afrika kutawala , hapakuwa na Chuma? Kwamba walikuta tunatumia zana za mawe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…